Pages

Tuesday, July 5, 2011

SIMBA YATINGA NUSU FAINALI



Timu ya Simba imeweza kuanza vizuri katika hatua ya robo fainali ya kagame Cup, Simba ilikuwa ya kwanza kuandika bao katika dakika ya nane ya mchezo huo kupitia kwa Ronald Seku wa Bunnamwaya kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa mpira wa Haruna Moshi, lakini badala yake akajikuta akiujaza wavuni mwake mpira huo.

Bao hilo liliamsha 'hasira' za Bunamwaya ambapo waliliandama goli la Simba na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 19 kupitia kwa Mike Mutyaba.

Mutyaba alifunga bao hilo kwa shuti kali lililomshinda kipa wa Simba Juma Kaseja na kujaa wavuni.

Dakika ya 83 Simba ilipata bao la pili na la ushindi kupitia kwa Jerry Santo baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Bunnamwaya kabla ya kuujaza mpira wavuni.

Kwa ujumla katika mechi hiyo ya pili ya robo fainali timu zilishambuliana kwa zamu na Simba kuonekana kuwa na tatizo la wafungaji huku ikiwa imara sehemu ya kiungo na kwenye safu ya ulinzi.

No comments:

Post a Comment