Pages

Thursday, May 31, 2012

HALI TETE

MAFUTA YA NAZI

Habari ndugu zangu wapendwa

kwa na shukuru kwa kupata huu muda niweze kutoa niliyonayo moyoni nimesoma matumizi ya mafuta ya nazi kwa ajili ya kuongeza CD4 lakini haijaainishwa matumizi yake kwamba kiasi gani na ni mara ngapi kwa siku kwa kipimo kipi ningeshukuru kama nitaweza kupatiwa maelezo  kweli ninashida CD4 haziongezeki pamoja na kuwa kwenye second line ya dawa

asanteni sana


Mdau

Monday, May 28, 2012

TATIZO LA UMEME KIGAMBONI NA MBAGALA

Hivi karibuni nimekuwa nikipokea malalamiko mengi ya kukatika mara kwa mara kwa umeme katika maeneo ya Kigamboni na Mbagala.

Matatizo haya yanatokana na sababu kuu mbili: Moja, miundombinu ya umeme kuzidiwa na mahitaji na pili, uchakavu wa miundombinu.

Kwa hivi sasa, watumiaji wa umeme wa Kigamboni, Mbagala na Mkuranga wanapata mahitaji toka kwenye kituo kidogo kilichopo Ilala. Umeme unaotoka kwenye kituo hautoshelezi mahitaji ya maeneo yote yaliyotajwa hapo juu. Hali hii imepelekea baadhi ya maeneo kuwa na umeme ndogo na baadhi ya maeneo kukatika hususan nyakati za usiku.

HATUA ZINAZOCHUKULIWA KUTATUA TATIZO HILI
Hatua za muda mrefu:: Tanesco inatarajia kujenga Sub-station kubwa maeneo ya Mbagala ambayo itahudumua maeneo ya Kigamboni na Mbagala. Kazi hii inatarajia kuanza karibuni baada ya kukamilisha zoezi la fidia kwa wananchi waliobaki.

Hatua za muda mfupi: Tanesco inaendelea na ukarabati wa mfumo uliopo ili uweze kuihimili mahitaji ya sasa. Katika wiki hii, Tanesco ilikata umeme tarehe 22, 24 na leo 27 kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni ilikufanya kazi hii. Kwa mujibu wa Tanesco kazi hii inatarajia kukamilika wiki mbili zijazo.

Naomba tuvute subira wakati Tanesco wanalifanyia kazi tatizo la umeme kukatika mara kwa mara.

Ahsanteni.

Dkt. Faustine Ndugulile
Mbunge Kigamboni

DrFaustine.com

Sunday, May 27, 2012

AKUTWA GESTI AMEKUFA

 Mwili wa Marehemu ukitiwa kwenye gari na kupelekwa hospitali
Dada mmoja amekutwa amekufa kitandani katika nyumba ya kulala wageni iitwayo ANNA INN iliyopo Temeke Wailes, Mjumbe wa eneo hilo Bi. Mwanaisha kwenye picha alisema huyo mtu hakumkuta na jeraha lolote na hakuna chochote kilichochukuliwa vitu vyake vyote vilikuwepo, na wafanyakazi wa hapo walisema mtu huyo aliingia siku ya Jumamosi usiku na baada ya kuona kimya, wakaamua kwenda kugonga ndio wakamkuta tayari keshakufa, Askari walifika na kuichukua maiti kuipeleka hospitali ya temeke kwa uchunguzi zaidi.

Thursday, May 24, 2012

MAISHA KUSAIDIANA

Mkurugenzi Temeke aipongeza APEC

MKURUGENZI wa Manispaa ya Temeke, Magreth Nyalile amelipongeza shirika lisilo la kiserikali la Kukabiliana na Umasikini na Kutunza Mazingira (APEC), kwa kupunguza matukio ya uporaji na mauaji ya waendesha pikipiki na baiskeli ya magurudumu matatu maarufu bodaboda katika Wilaya ya Temeke.

Akifunga mafunzo ya usalama kwa waendesha pikipiki Kata ya Yombo Vituka, Buza na Makangarawe iliyosoma kwa niaba yake na Ofisa Afya Usafishaji Manispaa ya Temeke, Ernest Mamuya, Mkurugezi huyo alisema kazi inayofanywa na APEC ni ya kupongezwa.


“Tunawashukuru APEC kwa kupunguza mauaji ya waendesha pikipiki kutoka watu watano mwaka 2009 hadi watatu mwaka 2011,” alisema.


Pia alipongeza kazi nzuri ya kufundisha Polisi Jamii na uanzishwaji wa vikundi vya Ulinzi Shirikishi ilivyosaidia kupatikana kwa bunduki 18 Wilaya ya Temeke na risasi 1,309 kwa Kanda maalumu ya Dar es Salaam zote zikitumika katika uhalifu.


Awali Mkurugenzi Mtendaji wa APEC, Respicius Timanywa alisema tangu kuanza mafunzo ya ulinzi shirikishi mwaka 2010 mauaji na matukio ya uhalifu wa uporaji wa pikipiki yamepungua kwa kiasi kikubwa Timanywa aliomba Polisi kusaidia kufunga vituo vya pikipiki ambavyo vinaongoza kwa vitendo viovu kama uchomaji wa magari ya watu na kubeba mshikaki.


Alisema mwaka 2009 pekee takwimu zinaonesha watu 120 walifariki dunia na wengine 1,073 kupata ajali mbaya na baadhi kukatwa viungo vyao wengi wao wakiwa waendesha pikipiki. Na mpaka sasa kwa kushirikiana na polisi wameshafundisha vijana 1,000.


 

Miss Kigamboni waanza kujifua

MAZOEZI kwa ajili ya kushiriki shindano la kumsaka malkia wa kitongoji cha Kigamboni
mwaka huu 'Miss Kigamboni City 2012' yameshaanza mapema wiki hii imefahamika.

Shindano hilo limepangwa kufanyika Juni 15 kwenye ukumbi wa Navy Beach ulioko Dar es Salaam.


Akizungumza jana jijini, Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu, alisema kuwa maandalizi ya kinyang'anyiro hicho yanaendelea na warembo tayari wameshaanza mazoezi kwenye

ukumbi wa Break Point ulioko Posta jirani na Club Billicanas.

Alisema, bado milango iko wazi kwa warembo wenye sifa kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini wanakaribishwa kushiriki kuwania taji hilo.


Aliongeza kuwa kampuni yake imejipanga kuhakikisha shindano la mwaka huu linakuwa bora na kuwapata washiriki watakaokwenda kutwaa taji la Kanda ya Temeke na hatimaye taji la taifa la Redd's Miss Tanzania baadaye mwaka huu.


"Kila kitu ni maandalizi, tumejiandaa katika kufanya mchakato wa kupata warembo wenye sifa ili waweze kuiwakilisha vyema Kigamboni katika mashindano ya Kanda," alisema

Somoe.

Aliwataja warembo ambao wameshaanza mazoezi ni Caroline Peter, Theopisther Wenso, Sophia Martime, Amina Aboubakar, Aisha Rajab, Rosemary Peter, Mariam Mbulilo, Julieth Phili na Doreen Kweka.


Warembo hao wanafanya mazoezi chini ya Hawa Ismail ambaye alikuwa mshindi ya shindano la Kanda ya Temeke mwaka 2003.


"Bado tunakaribisha wadau wa sanaa ya urembo kutudhamini shindano hili, tunaamini uwepo wao ndio utafanikisha ubora na hadhi ya shindano letu mwaka huu kama tulivyodhamiria," aliongeza.

Tuesday, May 22, 2012

MOTO WAUNGUZA MADUKA TEMEKE MWISHO

                                                 Watu wakitaharuki baada ya tukio la moto kuzidi
Moto Mkubwa umezuka asubuhi ya leo maeneo ya Temeke Mwisho karibu na kituo kikuu cha mabasi ya abiria, Moto huo ulianza kuwaka mnamo majira ya saa 5 asubuhi, chanzo cha moto huo inasemekana ni mafundi wa uchomeaji ambao walikuwa wakichomea moja ya Makontena ambayo yalikuwa karibu na maduka hayo na kusababisha ajali hiyo.
 Mashuhuda wakishudia tukio zima la moto ukiendelea kuwaka na wasijue nini la kufanya.
 Baadhi ya maduka ambayo yaliweza kuteketea kabisa kwa moto.
 Huyu jamaa mwenye gari aliamua kujitolea baada ya kuona kikosi cha zimamoto wamepigiwa simu kwa muda mrefu bila kufika
 Kadri mda ulivyokuwa unakwenda na hali ikawa mbaya zaidi walifanikiwa kuuzima lakini si kwa kiasi kikubwa sana
 Baada kama ya saa nzima hiki cha zima moto ndio kikaingia

Wananchi wakifukuzwa na askari waliokuwepo katika eneo hilo

Saturday, May 19, 2012

DROGBA AIBEBA CHELSEA

 Didier Drogba akifunga penati ya ushindi iliyowawezasha Chelsea kuchukua ubingwa wa UEFA
 Didier Drogba akifurahi baada ya kufunga penati ya ushindi
Chelsea imeweza kutengeneza historia mpya katika klabu baada ya kufanikiwa kuchukua kombe la UEFA, Goli la ushindi alilofunga Drogba liliwezesha kuipa Chelsea ubingwa wao katika uhai wa Timu, Chelsea ni timu ambayo ilikuwa haijawahi kufanikiwa kuchukua kombe hilo

Friday, May 18, 2012

ROYAL GIRAFFE HOTEL YAKABIDHIWA RASMI

Hotel ya kisasa ya Royal Girrafe iliyopo Temeke Sudan ambayo imekabidhiwa rasmi leo
 Baadhi ya wasimamizi wakuu wa Hotel hiyo Idrissa na Rajabu
Mkurugenzi Mkuu wa Royal Girrafe Hotel Yusuph (Timbwa) akiwa na familia yake
 Baadhi ya watu walioalikwa katika ufunguzi huo
 Ukumbi wa Disco Full kiyoyozi
Dan



 Eddy madishi ndie aliyefunga camera na vyombo vyote vya viburudisho mwenye suti nyeusi pamoja na Roja Boy

MAFISANGO ALIVYOAGWA VIWANJA VYA TCC LEO

Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Shabaan Nditi, Juma Nyosso, na Bocco wakiwa wamebeba jeneza la mchezaji mwenzio Patrick Mafisango wakati likiingia katika viwanja vya TCC kwa ajili ya kuagwa kabla ya kusafirishwa kwenda kwao DRC Congo kwa ajili ya mazishi.
Haruna Moshi Boban akiwa mwenye huzuni mkubwa leo wakati wa kuaga mwili wa Mafisango. Pole Boban mwenyezi mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu.
Kipenga wa kati akiwa na rafiki zake
Juma Kaseja
Mh. Ismail Aden Rage akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
 Haji Mboto mwenye flana nyeusi na Geogre
KR MULLAH
 Aliyekuwa kocha wa Moro Utd Hassan Banyai akiwa na baadhi ya wachezaji wake
 Mdau Sossy akiwa na baadhi ya wadau wa Temeke Nchimbi(Hamidi) pamoja na Humud
MBELE YAKO NYUMA YETU PUMZIKA KWA AMANI

Thursday, May 17, 2012

MAFISANGO KUAGWA KESHO TCC CHANG`OMBE

MWILI wa kiungo mahiri wa SImba SC, Patrick Mutesa Mafisango (32), sasa utaagwa kwenye Uwanja wa TCC, Chang'ombe, Dar es Salaam, kuanzia saa 3:00 asubuhi badala Leaders Club, Kinondoni, kama ilivyotangazwa awali.
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange 'Kaburu' ameongea  jioni hii kwamba wamehamishia shughuli ya kuuga mwili huo Uwanja wa Siga ratiba nyingine zote zinabaki kama ilivyotangazwa awali.
Mafisango amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika eneo la Keko jirani na Chuo cha VETA jijini Dar es Salaam.
Mafisango alikufa kutokana na ajali iliyotokea wakati gari alilokuwa akiendesha lilipogonga mti ulio pembezoni mwa barabara ya Chang’ombe majira ya saa kumi kasorobo alfajiri. Marehemu alifariki papo hapo.
Kwenye gari aliyokuwamo Mafisango, kulikuwapo na abiria wengine wanne lakini ni Mafisango pekee ndiye aliyefariki dunia.
Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tayari kwa kusafirishwa kwenda kwao Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako atazikwa.
Ingawa alikuwa na uraia wa Rwanda na akiichezea timu ya taifa ya nchi hiyo (Amavubi), Mafisango alikuwa ni mzaliwa na raia wa DRC na uamuzi wa kuzikiwa huko ni wa familia yake.
Msiba wa Mafisango uko katika eneo la Keko Toroli jirani na kituo cha Chang’ombe Maduka Mawili (Njia Panda Sigara).
Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa kesho Ijumaa saa nne asubuhi katika viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es Salaam kabla ya mwili wake kusafirishwa kwenda Kinshasa majira ya saa kumi jioni.
Mafisango alizaliwa Machi 30, 1980 huko Kinshasa Zaire wakati huo na ameacha mke na mtoto mmoja wa kiume, Chris Paul, mwenye umri wa miaka mitano.
Mafisango ameichezea Simba kwa msimu mmoja tu akitokea Azam ya Dar es Salaam lakini kabla ya hapo alichezea pia TP Mazembe ya DRC, APR ya Rwanda na pia aliwahi kuwa nahodha wa Amavubi kwa takribani miaka mitano.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, Makamu wake, Geofrey Nyange Kaburu na wajumbe wa kamati ya watendaji wameeleza kusikitishwa kwao na msiba huu mkubwa kwa klabu na wamewataka wana Simba wote kuwa watulivu na kumwombea marehemu Mungu amlaze mahali pema peponi.
Uongozi wa Simba unaahidi kuwa utatoa taarifa nyingine zozote muhimu kwa wananchi ili wafahamu kuhusu msiba huu pale itakapotokea.

Wednesday, May 16, 2012

MAFISANGO AFARIKI DUNIANI

Nikiwa bado nimelala asubuhi hii mida ya saa 12.00 dada yangu ananigongea mlango na ananiuliza eti mafisango amefariki nikawa sina la kumjibu kwa kuwa sijui kinachoendelea ila katika pitia pitia glory Ngayoma akanitumia msg katika page yangu ya face book hivi
KWAHERI PATRICE MUTESA MAFISANGO, MUNGU AIWEKE ROHO YAKO MAHALA PEMA PEPONI, SIMBA FANS R REALLY GONNA MISS U BRO! TULIKUPENDA SANAA MUNGU AMEKUITA GHAFLA JEMBE LETU, REST IN PEACE PATRICE MAFISANGO.
Mpaka sasa chanzo cha ajali yake inasemekana ni ajali ya pikipiki

MAPOZI

GOMBA

watu hawalali ukiwauliza wanasaga, mirungi ambayo kwa sasa inauzwa sana Dar kwa kipindi hiki na sijui inafikaje kutoka huko inakotoka

NJOO TEMEKE MWANA YAPO KIBAO

Mfanyakazi wa Radio Clauds FM, Said Mohamed 'Said Bonge' akipanda migomba kwenye mashimo ya barabara ya Mwananyamala Hospitali Dar es Salaam leo huku gari likipiata kando yake. Bonge alisema amechukua uwamuzi huo baada ya wahusika kushindwa kuyafukia mashimo hayo ambayo yamekuwa yakileta usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo.
kwet jamejaa kibao

MNYAMA ANAPOAMUA LAKE












Hadi mwisho simba 1- kiboko 0