Pages

Thursday, March 29, 2012

MSETO WA NASH MC

MITIHANI,MCHAWI NDUGU,TUNAIZINDUA MITAA,KWAKO NASH EMCEE, VITA,MAALIM,HOMA IMENIZIDIA NA NYINGINE KIBAO NDANI YA
MZIMU WA SHAABAN ROBERT!KWA ALFU 6 TU!
Pata nakala yako sasa

By: Nash EmCeE
Hip Hop ArtIsT

HAINA MWISHO WA MWEZI

Tuesday, March 27, 2012

HARBOURS CLUB - KURASINI

 Moja wa ukumbi wa burudani uliopo Harbours club Kurasini Temeke
 Mazingira ya Viwanja vya Michezo huu ni upande wa Netball
 Upande wa Basket Ball
Kenny Mwaisabula Kushoto akibadilishana mawazo na baadhi ya wadau

Sunday, March 25, 2012

SIMBA 2 - E.S.S 0

 Washabiki wa Simba waliofika Uwanjani kushuhudia timu yao (HAKUNAGA)
 Moja ya hatari katika lango la E.S.S
 Pass Master Mwinyi kazimoto akiwa kazini
 Haruna Moshi Boban aliyekaa chini baada ya kuchezewa faulo
 Felix Sunzu akijaribu kuukimbilia mpira
 Kutoka kulia: Ngawina Ngawina, Jemedali Saidi, Abuu Mtiro wakifatilia pambano hilo
 Washabiki wa simba wakishangilia ushindi wao wa goli 2-0 mechi iliyochezwa katika uwanja mpya wa Taifa
Shabiki namba moja wa OKWI

CHIMBO

Saturday, March 24, 2012

UNAHITAJIKA MSAADA WAKO

MTOTO Honolata Juma Christian (8), (pichani) mkazi wa Mgeta wilayani Mvomero aliyetelekezwa na ndugu zake kutokana na maradhi ya ajabu yanayo msumbua, anataabika katika hospitali ya rufaa mjini hapa akiomba msaada wa shilingi 1,000,000 ili akatibiwe.
Gharama hizo ni za tiba,usafiri na matumizi katika Hospitali ya KCMC ya mjini Moshi ambako ameshauriwa kwenda na madaktari wa hospitali ya Mkoa wa Morogoro alikolazwa. 
Honolata ambaye tangu kuzaliwa kwake amekuwa akisumbuliwa na magonjwa likiwemo la kuota nywele mwili mzima, nundu mbili kichwani mithili ya pembe na matatizo ya macho.
Mtoto huyo analelewa na mama yake mzazi, Grace Francis (30) ambaye anadai ndugu zake wamemsusia na hawataki kumsaidia.
Akiwa hospitalini hapo wodi namba nne ,  Uwazi lilizungumza na mama huyo  ambaye alisema mtoto wake hivi sasa ameshindwa kuendelea na masomo kutokana na maradhi hayo ya ajabu.
 “Amefanyiwa uchunguzi na kugundulika kuwa jicho moja limekufa na asipopata tiba mapema la pili nalo litakufa, naomba msaada kwenu wasamaria,” alisema mama huyo huku akitokwa na machozi.
Akaongeza: “ Baada ya baba yake , Juma kufariki kwa kugongwa na gari shemeji,wifi na wakwe zangu wakamkataa wakisema sisi hatumtambui huyu mtoto mwache afe…nikaanza kuhangaika mahospitalini ikiwemo CCBRT ambako walimfanyia oparesheni ya jicho la kushoto ambalo anatumia kuonea,” alifafanua Grace. 
Walioguswa na habari hii wanaweza kumsaidia kwa kuwasiliana naye kwa namba ya simu 0713778024.

Walimu Wakuu wavuliwa vyeo udanganyifu matokeo darasa la saba

WALIMU WAKUU watano wa shule za msingi Manispaa ya Temeke jijini wamevuliwa vyeo vyao kwa kosa la kubainika kufanya udanganyifu katika mitihani ya darasa la saba iliyofanywa mwaka jana nchini kote.

Mitihani ilizua migogoro kufuatia kufanana wka matokeo na kuchaguliwa wasiokuwa na sifa wasiojua kusoma wala kuandika kuipita mitihani hiyo hali iliyolazimika Wizara ya elimu kuandaa mitihani ya majaribio kwa wanafunzi hao

Wizara ya elimu iliandaa mitihani ya majaribio kubaini wasiojua kusoma wala kuandika na kutoa ahadi kwa watakaobainika kufanya udanganyifu wa aina yeyote kupitisha wanafunzi hao kuwawajibisha

Afisa Elimu wa Manispaa ya Temeke, Honorina Mumba, aliiambia nifahamishe kuwa tayari walimu hao wameshavuliwa vyeo vyao na kuwa walimu wa kawaida katika shule zingine.

Alitaja walimu waliovuliwa vyeo hivyo walitoka katika shule ikiwemo Keko Magurumbasi, Taifa, Unubini Bokorani na Mgulani.

Awali Wizara ya Elimu ilitangaza kuwafutia matokeo jumla ya wanafunzi 458 katika shule za msingi za serikali

Hata hivyo Wizara ya elimu bado inaendelea na uchunguzi kubaini wale wote waliohusika kufanya udanganyifu katika mitihani hiyo

msaada toka 
nifahamishe

Monday, March 19, 2012

DUNIA YA SOKA YAUNGANA


 Wapenzi wa Mpira Miguu Duniani wameonyesha hisia zao na kuwa kitu katika kumuombea mchezaji wa Bolton Fabrice Muamba ambaye alianguka ghafla uwanjani kutokana na matatizo ya moyo. Hii ni moja wapo ya hisia za Gary Cahill mchezaji wa chelsea ambaye msimu uliopita walikuwa wote Bolton
Wachezaji wa Real Madrid wakionyesha ushirikiano wao
Washabiki wa liverpool nao ge
kushoto: Shauwn Wright akiwa na Ashley Cole wakiingia katika Hospital aliyelazwa Muamba
Tuncay mchezaji wa Bolton akimsalia uwanjani
Mchezaji wa Totenham Jemain Defoe akiwasili hospital pamoja na mama yake
Mchezaji wa Arsenal Djorou akiingia Hospital
 Mawazo ya baadhi ya wachezaji katika mitandao tofauti


INAHUUUUUU HII NDIO MBAGALA

Usipopitia haya we bado hujakaa Mbagala, baadhi ya wakazi wa Mbagala wakipanda basi kwa kupitia dirishani
Hii huku kwetu kawaida tu

BANDARI MABINGWA TEMEKE

Timu ya Bandari imetwaa ubingwa wa wilaya ya Temeke baada ya kuifunga Zakheim FC bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa katika Uwanja wa chuo cha Bandari jijini Dar es Salaam
Ushindi huo uliiwezesha Bandari FC kujinyakulia kitita cha Tshs. 500,000, seti mbili za jezi kombe pamoja na mipira miwili kutoka kwa uongozi wa chama cha soka wilaya ya Temeke TEFA ambao ndio walikuwa waandaaji wa mashindano hayo.
Zakheim FC walijipatia zawadi ya Tshs. 300,000 seti mbili za jezi pamoja na mipira miwili wakati timu ya Panama Fc yenyewe ilishika nafasi ya tatu na kuondoka na Tshs. 150,000 pamoja na mipira miwili.

Saturday, March 17, 2012

SHEREHE ZA MAULID MSIKITI WA AL-MAJUMUWAT-TEMEKE MWISHO

Sheikh  Sharif Hussein wa Mombasa akitoa nasaha zake katika hafla hiyo ya Maulid
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Al had Mussa Salim (Nakshiband) akimsikiliza kwa makini Sharif Hussein Al Badawi wa Mombasa
 Baadhi ya waumini waliohudhuria sherehe hizo za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S.A.W katika viwanja vya msikiti wa Temeke Mwisho

 Msomaji wa Qur-an kutoka Misri katika chuo cha Markaz akisoma Qur-an tukufu katika Sherehe hizo.
  Miongoni mwa wageni waliohudhuria katika sherehe hizo kutoka kushoto ni jaji mstaafu Msumi na Prof. Juma Kapuya wakibadilishana mawazo
 Mkuu wa majeshi Tanzania Gen. Davis Mwamunyange nae alikuwa  mmoja wa waalikwa katika shughuli hiyo pamoja na Dr. Idrissa Mtulya
 Mgeni rasmi Dr. Hussein Ally Mwinyi akitoa nasaha zake
Kadhi Mkuu wa Tanzania Mufti Shaban Idd Simba akihutubia katika sherehe hizo za Maulidi, pembeni yake ni Naibu Mufti Ally Muhidin Mkoyogole

Saturday, March 10, 2012

TOBOA TOBO SIJUI KWELI

 Mfuko ambao aliwekewa Paka na baadae huyu paka kuuliwa kwa kuchinjwa na meno

 Toboa tobo mmoja wa mganga wa jadi maarufu maeneo ya Mtoni na Tandika akiwa katika baadhi ya maeneo ya Mtoni kutafuta wachawi wa mtaa
Wakazi wa maeneo hayo wakifatilia kwa makini mganga wa huyu

Tayari hapa kishakamatwa hicho kitu na ndio kinachomwa moto hu

ALBADIRI YA KIHINDI

Mmoja ya vijana ambaye akutambulika jina lake, huyu ni mmoja wa waathirika wa matumizi ya madawa ya kulevya ambayo huku kwetu tunaita albadiri ya kihindi akiwa hajitambui 

Monday, March 5, 2012

MSIONE KIMYA WADAU


Najua wadau wengi muda mwingi umepita bila kuwapa habari zozote zinazojili uswahilini kwetu hali kidogo ilikuwa sio shwari nilistua enka katika harakati nyingine, naomba tuendelee kuvumiliana mambo yatakuwa mazuri hivi karibuni na kutafakari kitu kipya kipi tuanze nacho katika kuzidi kutia nakshi blog yetu.
Teme