Pages

Monday, March 19, 2012

BANDARI MABINGWA TEMEKE

Timu ya Bandari imetwaa ubingwa wa wilaya ya Temeke baada ya kuifunga Zakheim FC bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa katika Uwanja wa chuo cha Bandari jijini Dar es Salaam
Ushindi huo uliiwezesha Bandari FC kujinyakulia kitita cha Tshs. 500,000, seti mbili za jezi kombe pamoja na mipira miwili kutoka kwa uongozi wa chama cha soka wilaya ya Temeke TEFA ambao ndio walikuwa waandaaji wa mashindano hayo.
Zakheim FC walijipatia zawadi ya Tshs. 300,000 seti mbili za jezi pamoja na mipira miwili wakati timu ya Panama Fc yenyewe ilishika nafasi ya tatu na kuondoka na Tshs. 150,000 pamoja na mipira miwili.

No comments:

Post a Comment