Pages

Thursday, September 29, 2011

BUNDI HUANZA KURUKA JUA LINAPOZAMA

 
Ndugu zangu,


Bundi  ana kawaida ya kuanza kuruka  jua linapozama. Bundi haoni kwenye mwanga, ndio maana ya kulisubiri giza.

Nchi yetu imeingiwa na giza nene na bundi ameanza kuruka.  Ngoja nikutafunie msomaji, giza hilo ni ufisadi uliotamalaki na hali ya kukosa maarifa.  Ufisadi  chanzo chake ni maradhi ya kuendekeza ubinafsi. Na kibaya zaidi, ubinafsi huo unapofanywa na viongozi.

Ndio,   aliye gizani anamwona aliye kwenye mwanga, lakini aliye kwenye mwanga hamwoni aliye gizani. Na ajionaye yuko kwenye mwanga aweza kabisa kuwa yu gizani na asimwone kabisa aliye kwenye giza jingine. Haiyumkini aliye topeni akajaribu kumwinua mwingine aliye topeni, wote watadidimia topeni!

Waongozwa wengi wako gizani, lakini hata wale viongozi waliodhaniwa kuwa wako kwenye mwanga na wana uwezo wa  kuwasaidia kuwatoa wananchi gizani, nao yaonekana ndio walio  gizani na wanaochangia kutubakisha gizani . 

Hakika, mambo mengine wayafanyao wanayafanya kama vile hawakusoma hata madarasa matano ya Shule ya Msingi, ni ya ajabu, ni mambo yanayofanywa  au kusemwa na watu wajinga. Watu walio gizani.

Ndio,  tatizo kubwa  kwa baadhi ya hao viongozi ni kuendekeza ubinafsi na kupenda sana U-bwana Mkubwa. Ni ushamba fulani hivi.  Na kwa hali ilivyo sasa, wananchi wameanza kuonyesha kuchoshwa na hali iliyopo inayosababishwa na baadhi ya viongozi wao. Wananchi hawa hawawezi kukaa kimya daima, ni mjinga tu atakayeamini kuwa jambo hilo linawezekana. Umma umeanza sasa  kuamka na kusema, ‘ basi, inatosha’. 

Maggid,
Iringa, 
 Septemba, 2011

Wednesday, September 28, 2011

KUZALIWA KWA ZOZO

Siku kama ya leo mmoja wa wanamuziki kutoka kundi la wanaume Family Zozo Wida anatimiza miaka kadhaa toka kuzaliwa kwake tunakutakia maisha mema na marefu na ufanisi mzuri katika kazi yako.
hepi besdei ZoZo

Sunday, September 25, 2011

MBUNGE WA TEMEKE AONGEA NA WANANCHI WAKE

Mb: Abas Mtemvu akijadiliana na baadhi ya viongozi wa kataya azimio





Hii ndio hali halisi ambayo iliyokuwepo Mitaa ya Azimio Tandika ambapo Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu alivyokuwa akiongea na wanachi katika viwanja vya shule vya Azimio Tandika

WIKI YA MAHAFARI KWA SHULE ZA TEMEKE

 Wahitimu wa Shule ya Sekondari Nzasa iliyopo Mbagala

 Picha ya pamoja ya wahitimu wa shule ya Sekondari nzasa

Wakuu wa shule ya sekondari Nzasa

JUMAPILI YA BURUDANI VIWANJA VYA MWEMBEYANGA-BONGO STAR SEARCH

Baadhi ya mashabiki waliohudhuria tamasha hilo katika viwanja vya mwembe yanga-Temeke

Rogers Lucas Kushoto akiwa na mwakilishi wa Temekepamoja Said Sobbo katika viwanja hivyo

Bella Kombo akitoa Burudani

Mashabiki wa Bella Kombo wakicheza pamoja baada kushindwa kuzuia hisia zao

Nyomi


 Wazir Salum (Wazy) mmoja wa washiriki wa Shindano la Bongo Star Search

Chiby Dayo akiwa jukwaani

Haji Ramadhani  mwenye T-shirt nyeupe akiwa na wazir salum jukwaani

MITAA YA YOMBO









Baadhi ya maeneo ya Yombo Buza Mchana huu

Thursday, September 22, 2011

MPINZANI ASHINDA UCHAGUZI ZAMBIA

Kiongozi wa chama cha Patriotic Front, Micheal Sata ametangazwa kwa mshindi wa uchaguzu wa urais nchini Zambia
Bw Sata alipata asilimia 43 ya kura zilizopigwa na kumshinda Rais Rupiah Banda wa chama tawala cha MMD ambacho kimekuwa mamlakani kwa muda wa miaka 20.
Michael Sata
Kiongozi wa Patriotic Front ameshinda uchaguzi wa urais Zambia
Tangazo hilo lilitolewa na Jaji Mkuu wa Zambia Ernest Sakala.
Awali watu wawili waliuawa kufuatia ghasia katika maeneo ambayo ni ngome ya upinzani.
Mkuu wa Polisi wa jimbo hilo maafuru kwa uzalishaji Shaba ameliambia shirika la habari la Reuters watu wamejitokeza katika barabara za mji wa Kitwe na Ndola wakivurumisha mawe.
Mwandishi wa BBC anasema ghadhabu hizi zimechochewa na agizo la serikali kupiga marufuku vyombo vya habari kutangaza matokeo bila ya idhini ya tume ya uchaguzi ya nchi hiyo.
Mwandishi wa BBC Mutuna Chanda akiwa Lusaka kilomita 300 kusini mwa Kitwe, anasema huko Kitwe, waandamanaji waliteketeza soko moja usiku na Polisi wameweka vizuwizi katika mji wa Wusaikile.
Rais Banda alimshinda Bw Sata kwa kura 35,000 katika uchaguzi wa mwaka 2008, matokeo yaliozusha ghasia kutoka upande wa upinzani katika ngome zao za mijini.
Tangu uchaguzi wa mwaka 2008, watu wengine milioni moja wamejiandikisha kuwa wapiga kura,wengi wao vijana wasio na ajira.
BBC

AOTA MAZIWA KWA KUMEZA DAWA ZA UKIMWI.

Mwanaume huyu Mtanzania mwenye maambukizi ya virusi vya ukimwi amejikuta maziwa yake yakikua siku hadi siku na kufikia kama ya mwanamke na hii imetokana na kumeza dawa za kinga zidi ya virusi vya.Amesema amejikuta maziwa yake yakiongezeka siku hadi siku na mwanzo hakujua nini tatizo baadae alipokwenda ktk utafiti zaidi ndio akagundua hizo dawa zinamfanya kuongezeka kwa matiti yake.