Pages

Wednesday, February 15, 2012

WANAOSEMA LOWASSA NI FISADI KWA SABABU YA RICHMOND SAGA, HAMKUONA HII TAARIFA NILIYOIONA MAHALI? EDWARD LOWASSA ALISAFISHWA NA MWAKYEMBE

Sasa ni wazi kwamba baada ya waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa kujitetea mbele ya kikao kilichopita cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) mjini Dodoma, wajumbe wengi wa kikao hicho, na wachambuzi wa mambo ya kisiasa nchini wanakubaliana kwamba mbunge huyu wa Monduli amekuwa akisakamwa na baadhi ya viongozi ndani ya chama chake na watu wengine, si kwa sababu yeye ni fisadi au kuna tuhuma za ukweli za ufisadi dhidi yake, bali ni kwa sababu ya mbio za urais za mwaka 2015.
Ingawa yeye mwenyewe hajakubali wala kukanusha nia yake ya kugombea urais mwaka 2015 kupitia chama chake, lakini zimejengeka hisia kwamba ana nia hiyo, lakini kinachoumiza wengi si hiyo nia tu, maana na wengine wengi tu ndani ya chama hicho wanaelezwa kuwa na nia hiyo. Kinachowasumbua watu wasiompenda ni kwamba kati ya hao wanaodhaniwa kuwa na nia
Inawezekana kumbukumbu za watu wengi zimechakachuliwa kiasi cha kutokumbuka kwamba Kamati Teule ya Dr. Harrison Mwakyembe iliyokuwa inachunguza sakata la mkataba wa kufua umeme baina ya TANESCO na kampuni ya Richmond ilimsafisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kwamba hakuwajibika na kujiuzulu kutokana na ufisadi wake katika sakata hilo, bali aliwajibika kisiasa kwa makosa ya watu waliokuwa chini yake.
Inashangaza pia kwamba hata wajumbe wa Kamati hiyo, akiwemo mwenyekiti wao, Dr. Mwakyembe, wanashindwa kumtetea Bw. Lowassa anapoendelea sasa hivi kusakamwa na baadhi ya wanasiasa na wanajamii kwamba ni fisadi kutokana na kashfa ya Richmond, na hawajitokezi kumtetea na kurejea hitimisho la ripoti yao ndani ya Bunge. Lakini mbaya zaidi hata baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu kabisa wa chama chake hawakumbuki hitimisho la ripoti hiyo na wameng’ang’ania kwamba kujiuzulu kwa Lowassa uwaziri mkuu hakutoshi na inabidi chama kimtose zaidi kutokana na kashfa ya Richmond.
Kwa kweli suala la tuhuma dhidi ya Edward Lowassa kwamba ni fisadi kutokana na tuhuma za Richmond, mtu unaweza kusema huu ni unafiki na chuki za kisiasa zilizopita kipimo. Suala la Richmond ni moja kati ya kashfa hapa nchini ambazo zilichunguzwa kwa makini sana na Bunge kupitia Kamati Teule na matokeo na hitimisho la uchunguzi huo yakamsafisha Lowassa kwamba alijiuzulu siyo kwa sababu alihusika moja kwa moja na kashfa hiyo bali aliwajibika kwa makosa yaliyotendwa na watu wa chini yake.
Tarehe 15 Februari 2008, kwa mujibu wa taarifa rasmi za majadiliano Bungeni (Hansard), Dr. Harrison Mwakyembe, wakati akihitimisha hoja ya Kamati Teule iliyochunguza suala la Richmond, alisema:
“Mheshimiwa Spika, ninaomba nianze na utangulizi mfupi na rahisi; uwajibikaji kwa viongozi waandamizi katika nchi zinazolinda na kuenzi demokrasia kama vile Tanzania, una sura mbili; sura ya kwanza, kiongozi anawajibika kwa makosa yake mwenyewe ya kiutendaji. Kiongozi anafanya maamuzi mabaya, pengine kwa kishawishi cha pesa, maamuzi yake yakaleta hasara au kiongozi ameshindwa kutoa ushauri mzuri kama kiongozi, kwa kukiuka kanuni, kukiuka taratibu na kadhalika, matatizo yakatokea, anawajibika. Sasa sura hii ya uwajibikaji, inahusisha uvunjwaji wa maadili, kanuni, sheria, miiko ya uongozi na kadhalika. Chini ya uwajibikaji wa aina hii, kiongozi anaweza akashitakiwa, akaadhibiwa mbali na kuachia ngazi. Nitarejea kwenye sura hii hivi punde. Suala la msingi hapa ni kuwa, kuna element ya adhabu katika sura hii ya kwanza.
“Sura ya pili; kiongozi anawajibika kwa makosa ambayo si yake moja kwa moja ila yaliyofanywa na watendaji chini yake. Kitendo cha kuwajibika kwa aina hii, kunaijengea Serikali au taasisi heshima na imani ya pekee katika jamii, kunatoa picha ya kwamba, uongozi unajali, unalielewa tatizo kwa kubeba lawama wao wenyewe. (Makofi)
“Mheshimiwa Spika, katika suala hili la Richmond, viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini na Waziri Mkuu, walikuwa wanakabiliwa na uwajibikaji wa aina hizo mbili. Kwanza, uwajibikaji unaotokana na makosa ya viongozi wenyewe katika maamuzi yao, maelekezo yao, maagizo yao na kadhalika. Mawaziri wote wawili wa Nishati na Madini; aliyetangulia na aliyefuatia baadaye, Katibu Mkuu na Kamishina wa Nishati, wote tukawaona wana makosa ya moja kwa moja, waliyoyafanya wao kwa njia moja au nyingine. Kwa kuwa uwajibikaji wa aina hii, unatokana na ukuikwaji wa kanuni, taratibu, maadili, sheria na kadhalika, Kamati Teule ikahakikisha inawahoji wote ili kusikia their side of the story kabla ya kutoa pendekezo la kuwawajibisha kwa makosa waliyofanya. Ndiyo maana baada ya kuwahoji, tumependekeza hatua za kuchukuliwa dhidi yao.
“Hali haikuwa hivyo kwa Waziri Mkuu; Kamati teule ilikuwa na ushahidi wa mawasiliano ya karibu kati ya Waziri Mkuu na Uongozi wa Wizara. Ushahidi huo haukutosha kwa uwajibikaji wa sura ile ya kwanza wa kiongozi kukutwa na makosa ya moja kwa moja, aliyoyafanya yeye mwenyewe kwa njia moja au nyingine, lakini ushahidi huo ulitosha kwa uwajibikaji wa sura ya pili, ambao hauhitaji mahojiano, kusikilizwa wala utetezi. Unawajibika kwa makosa ya watendaji walio chini yako. Hiyo ndiyo demokrasia. Wabunge wengi wametoa mifano mingi hapa, ukiwemo wa Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi, alipokuwa waziri wa Mambo ya Ndani; aliwajibika kwa makosa ya askari huko Shinyanga wakati yeye alikuwa Dar es Salaam; hatukumsikia akidai apewe nafasi ya kusikilizwa na hata kama angepewa, bado angewajibika yeye mwenyewe. (Makofi)
“Mheshimiwa Spika, Kamati Teule inatamka ukurasa wa 37 wa taarifa yake kuwa, ninanukuu ‘Ushiriki huu wa karibu wa Waziri Mkuu katika kila hatua ya zabuni ya umeme wa dharura si lazima uwe ushahidi wa kwamba, kiongozi huyo wa Kitaifa alihusika katika kuibeba Richmond. Unaweza pia ukawa ushahidi wa style yake ya kawaida kabisa ya Waziri Mkuu katika kufuatilia masuala yote ya Kitaifa kwa karibu sana, tukizingatia kwamba, nchi wakati huo ilikuwa katika kipindi kigumu sana cha ukosefu wa umeme…..”
Nina wasiwasi kwamba baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa na wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM ama wamesahau kauli hii ya Dr. Harrison Mwakyembe, ama kwa makusudi wanataka kupotosha watanzania. Akina Nape Nauye na John Chiligati wanamjumuisha Edward Lowassa kwenye kundi la mafisadi kutokana na suala la Richmond. Lakini Chiligati alikuwa Bungeni wakati Mwakyembe akihitimisha hoja ya Kamati yake Teule, na alimsikia Mwakyembe akimsafisha Lowassa kwamba makosa yake hayakuangukia kwenye sura ya kwanza ya uwajibika, ya kiongozi kuwajibika kwa makosa yake mwenyewe. Sura hii ndiyo unayoweza hata kumwita mtu fisadi. Lakini Lowassa aliwajibika kwa makosa ya watendaji walio chini yake, hata kwa mujibu wa Dr. Mwakyembe. Anayewajibika kwa aina hii ya pili huwezi kumwita fisadi. Akisifu aina hii ya Edward Lowassa kuwajibika, Dr. Mwakyembe anasema, “…Kitendo cha kuwajibika kwa aina hii, kunaijengea Serikali au taasisi heshima na imani ya pekee katika jamii, kunatoa picha ya kwamba, uongozi unajali, unalielewa tatizo kwa kubeba lawama wao wenyewe”. (Makofi). Mwakyembe anakwenda mbali na kuhusisha uwajibikaji huu wa Lowassa na ule wa Mzee Ali Hassan Mwinyi.
Naye Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiwasilisha utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu suala hilo tarehe 28 Agosti 2008 alisema yafuatayo kuhusu azimio na. 16 la Waziri Mkuu kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huo, “Mheshimiwa Naibu Spika, hatua zilizochukuliwa ni kwamba, Azimio hili lilitekelezwa mwezi Februari, 2008 kwa kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu aliamua kujiuzulu kwa kuwajibika kisiasa kwa maslahi ya Taifa.” Hivyo ni wazi hata Serikali inakubaliana na Kamati Teule kwamba Mhe. Lowassa aliwajibika, siyo kama fisadi bali aliwajibika kisiasa kwa maslahi ya Taifa. Ndiyo maana Azimio na. 16 linalomhusu Waziri Mkuu halikuendelea kujadiliwa Bungeni. Hata wanaodai kwamba baadaye Spika aliondoa hoja hii Bungeni kabla halijakamilika, wajue kwamba suala la Waziri Mkuu kuwajibika (Azimio na. 16) halikuwemo tena, na kwa hiyo hata hoja ingeendelea kuwa Bungeni Lowassa asingeguswa tena.
Sudi Mnete 

YALIYOMKUTA MWENZENU HOSPITAL TEMEKE

 Fauz Seif Hapa alipokuwa South African katika chuo Uhasibu Pretoria
 Hapa akarudi nyumbani kwa likizo akapata ajali ya pikipiki barabara ya Pugu karibu na Airport, na hapa akapelekwa hospital ya Temeke kwa matibabu zaidi.
 Hapa baada ya kufanyiwa Operesheni ya mguu katika hospital ya Temeke lakini hali ikawa tofauti kadri siku zilivyokuwa zinaenda mguu ukawa unazidi kujaa ikaja kugundulika kuwa chuma alichowekewa kilikuwa na kutu ikabidi wampasue tena lakini hali ikawa mbaya zaidi
 Na kwa sasa yuko India akipata matibabu ya mguu huo na hivi ndio hali ya mguu wake ulivyo
 Baadhi ya madaktari wakimshughulikia mguu ambao umeleta tatizo
Hivi sasa hali ya mguu wake ulivyo kwa sasa nchini India  na maendeleo yake ni mazuri

Monday, February 13, 2012

WAWILI WAFA WAKISHEREHEKEA UBINGWA



Wakati timu ya Taifa Zambia (Chipolopolo) wamewasili Jumatatu huku wakipokewa na maelfu ya mashabiki baada ya kufanikiwa kuchukua kwa mara ya kwanza ubingwa wa Afrika
Wakati hayo yakiendelea inasemekana kwamba kuna watu wawili wamefariki katika kusheherekea ushindi huo.

DAIMA USIPENDE

Daima usipende kusikiliza habari za watu utajikuta una dhima ya kuwasimulia habari zako,Usimlaumu mtu kukunyima mwaliko katika jambo lake ni dhahiri jambo hilo halikuwa na kheri kwako,usipende kuuliza kila jambo kwani majibu mengine yaweza kuhuzunisha moyo wako,usipende kusimulia furaha yako kwa kila mtu kwani mahasidi hujifanya kufurahi nawe kumbe mioyo yao yawauma,usipende kukaa sana kwa watu kwani kukaa kidogo hudumisha hamu ya kutaka kukuona tena,usimtegemee binadamu mwenzio kwa jambo lolote mtegemee Mola kwa yote kwani binadamu ameumbwa kwa wivu,choyo,chuki na husda...

Sunday, February 12, 2012

NASH MC ATUA MWANZA

 Nash Mc akiwa katika kituo cha mabasi cha buzuruga Mwanza akisambaza album yake ya Hazina

 Hapa Nash Mc akifanya mahojianao na moja ya kituo cha radio cha chuo kikuu cha saut
NaSh Mc akiwa na mmoja wa wasambazaji wa Album yake Mwanza

Friday, February 10, 2012

MBAGALA KINGUGI

 Hapa ni baadhi ya makazi ya eneo la watu ni Mbagala Kingugi eneo hili limejengwa pasipo kuwekwa na utaratibu maalum ambao hata ikitokea janga lolote hatari inakuwa ngumu kwa waokoaji kufanya dhughuli zao.

Na hiki ni baadhi ya choo vinavyotumika katika maeneo hayo

Saturday, February 4, 2012

Sinema kwa wasioona

 
 Wakati Bw Aziz Bouallouchen akiingia katika jumba la sinema katika mji wa Marrakesh nchini Morocco, tofauti na ilivyo katika majumba mengi ya sinema siku hizi ambapo wateja wanapewa miwani maalum za picha ya 3D, yeye anapewa vipokea sauti vinavyobanwa kichwani (headphones).

Bw Bouallouchen, ambaye umri wake ni kama miaka 20 hivi, si mwendaji sinema wa kawaida, na hili sio jumba la sinema la kawaida. Kila kiti ndani ya jumba la sinema kina vifaa maalum vya kusaidia wapenda filamu wasioona.
Filamu inayoonesha hapa inaitwa Lalla Hoby, filamu maarufu ya vichekesho nchini Morocco kuhusu mtu ambaye anavuka bahari ya Gibraltar ili kumsaka mke wake aliyemkimbia na kwenda kuishi na mwanaume mwingine nchini Ubelgiji.

Mwelekeo wa filamu

Filamu hiyo ilitoka mwaka 1996, na ni filamu pekee kutoka Afrika kaskazini kuwekewa maelezo ya maneno ndani yake.
Akiwa amevaa vipokea sauti ambavyo vimeunganishwa katika vinasa sauti katika vishikio vya kiti, Bw Bouallouchen anasikiliza sauti inayoelezea mfululizo wa matukio, ishara za watu na matukio ambayo usiposikia unapoteza mwelekeo wa filamu.
"Ni wazo zuri sana," anasema Bw Bouallouchen. "Sijaweza 'kutazama' filamu tangu nilipopatwa na maradhi yaliyosababisha kupoteza uwezo wa kuona."
Sauti kutoka vipokea sauti maalum kuelezea matukio ya filamu
"Lakini sasa nahisi kama sehemu ya ulimwengu wa filamu," anasema. Bw Bouallouchen alipoteza uwezo wa kuona mwaka 2005 baada ya kupatwa na maradhi yaitwayo Behcet's syndrome yaliyoshambulia mishipa ya macho.
Miaka saba baadaye, amejikuta akiwa amekaa sambamba na watu wanaoona, "wakitazama" filamu pamoja.
Na hiyo ni kutokana na maelezo ya maneno, kila mmoja anacheka wakati muafaka katika vichekesho vya Lalla Hoby, akionekana kuanguka katika boti ndogo katika bahari ya Gibraltar.
Morocco inaongoza njia barani Afrika katika matumizi ya teknolojia hii mpya. Sauti inazungumza "sambamba" na matendo katika filamu na hutoa taswira njema zaidi kwa watu ambao hawawezi kuona.

Viwango

"Sisi ni nchi pekee barani Afrika na katika mataifa ya Kiarabu ambao tunatoa huduma hii kwa wasioona," anasema Nadia el-Hansali wa Wakfu wa Tamasha la Filamu la Marrakesh.
Wakfu huo, ambao unaandaa matamasha mengi makubwa ya filamu, ambapo filamu zenye maelezo ya sauti kwa wasioona zimekuwa zikioneshwa kwa miaka miwili, unatenga fedha kwa ajili ya filamu zote ziwe na viwango vya kuonekana na watu wasioona.
Filamu nane mpaka sasa zina maelezo ya sauti, ikiwemo L'Atlante ya mwaka 1934, The African Queen (1951) na East of Eden (1955).
Katika kipindi cha miezi 18 ijayo, filamu nyingine sita zitawekewa huduma hiyo ya maelezo ya sauti.
"Tumetazama kuona kiasi gani cha kusema na kipi ni muhimu kwa ajili ya filamu nzima kueleweka"
Nadia el-Hansali
Bi el-Hansali huandika mswada (script) kwa ajili ya wacheza sinema ili wasome sambamba na matukio katika filamu.
Iko kamilifu kabisa, na sauti huingia katikati ya mapengo kati ya mazungumzo ya wacheza sinema.
"Tumetazama kuona kiasi gani cha kusema na kipi ni muhimu kwa ajili ya filamu nzima kueleweka," amesema Bi el-Hansali.
"Naepuka kutoa taarifa nyingi kupita kiasi ambazo zitawachanganya wale wasio na uwezo wa kuona skrini."
Lengo ni kuondokana na mtindo wa zamani wa kutumia watu kutoa maelezo ndani ya sinema, huku wakiwa wamesimama, wakijaribu kuelezea kinachoendelea, lakini mara nyingi hutoa maelezo hayo wakati mazungumzo muhimu katika filamu yakiendelea.

Sinema

Mohamed Doukkali, mhadhiri asiyeona wa falsafa katika chuo kikuu cha Rabat nchini Morocco, ni mshabiki mkubwa wa teknolojia na yeye hutumia kompyuta maalum katika kazi zake za kila siku.
"Moja ya mambo muhimu ya teknolojia mpya ni kuwa huondoa vikwazo vinavyokukabili," Anasema Bw Doukkali.
Anajielezea kama mtu "mpenda filamu", lakini mara nyingi hutazama DVD akiwa nyumbani pamoja na mtu anayemuelezea kinachoendelea.
Amefurahishwa sana sasa kuwa hatimaye anaweza kwenda sinema.
"Pongezi kwa sauti ambayo inatoa maelezo ya kinachoendelea na tunaweza kufiatilia filamu katika njia ambayo hatukuweza kufuatilia zamani," amesema.
"Unafurahia zaidi kutazama filamu ukiwa umejumuika na watu wengine wengi, kitu ambacho ndio hasa lengo la sinema."
 BBC.