Pages

Thursday, December 27, 2012

KUMBUKUMBU

LENDA SILAS MABECHE
03-06-1970-----28-12-2008
Siku,wiki,miezi na sasa ni miaka 4 tangia ututoke,
Unakumbukwa sana na baba yako Silas Mabeche,Mama yako Grace Sambay,
wadogozako Eric,Irene,Sarah na Evah Wanao Shawn na Baraka,kwa ucheshi na upendo uliokua nao,
Pia unakumbukwa sana na ndugu ,jamaa na marafiki zako.
Bwana alitoa na bwana ametwaa
Jina lake lihimidiwe
AMEN

Monday, December 24, 2012

TEMEKE SQUAD WAKUTANA KUJADILI LIGI DARAJA LA II

 Wanachama wa Temeke Squad wakiwa katika Makao makuu ya klabu kujadili ligi daraja la pili inayoendelea kwa sasa
 Wanachama na wapenzi waliohudhuria katika mkutanao huo

LORI LAPINDUKA MTONI KWA AZIZI ALI

 Lori ambalo lilikuwa limebeba mzigo wa mahindi likiwa liepinduka maeneo ya mzunguko wa barabara ya Kwa Azizi Alli leo mchana
 Hali ya Lori ilivyokuwa
 Lazima tushangae shangae kidogo


MISHEMISHE ZA X-MAS

 Baadhi ya maeneo ya kariakoo watu bize na maandalizi ya sikukuu ya X-mas
 Baadhi ya maeneo ya Kariakoo leo

MDAU SAID WA BUNGARA AUWAGA UKAPERA

 Ndio mwenyewe kweli Said Bungara akimfunua shera mkewe Bi. Rehema,
 Said Bungara akiwa na Mpambe wake kabla ya kufungwa kwa ndoa.

 Bw. Said Bungara na Mkewe Bi. Reheama wakina nyuso za furaha baada ya kufunga ndoa hiyo katika ukumbi wa Kilamuu Mbezi Beach
 hayawi hayawi sasa yamekuwa
Bi. Rehema katika mapozi tena

Friday, December 21, 2012

JABIR SALEH JEMBE LA TEMEKE LINALOTUWAKILISHA VYEMA BONGO KWENYE UPANDE WA RADIO PRESENTER

     Hapa kati mtu mzima Jabir Saleh akiitendea vyema kazi yake, alipokua sambamba na Diamond kwenye mahojiano nae alipofika studio kutambulisha ngoma yake mpya ya kesho.Big up bro unatuwakilisha vyema temeke.
      Hapa Diamond akienda sawa na maswali ya mtu mzima Jabir Saleh
     Nimeipenda hii Macbook pro ndio habari ya mjini ila jiandae kwenye bei haiuzwi uchochoroni hii.Jamaa yupo kisasa zaidi anatupia kazi zake humo hana tabu na mtu.Hapo mzuka umepanda alipokua anadondosha mashairi ya nyimbo kesho.
    Picha zote kwa hisani ya thisisdiamond.com chungulia kwa mapicha zaidi.

Tuesday, December 18, 2012

GLOBEN NI SEHEMU AMBAYO NIKIIONA HUKUMBUKA MENGI SANA.SI MIMI TU NA HATA WADAU WENGINE WA STOCKHOLM WANAKUMBUKUMBU KUBWA JUU YA GLOBEN.

    Huu ni uwanja wa ndani mfano wa mtungi uliopo hapa Stockholm ambao hutumika kwa shughuli nyingi za burudani.
 Hapa msanii yeyote mkubwa anapokuja Stockholm hasa kipindi cha baridi hutumia uwanja huu kwa kutolea burudani.
 Pembeni yake pia kuna Hovet hapa hutumika sana kwa michezo kama ice hockey na matamasha ya mziki pia.
                                                               Hovet kwa nje

            Hapa sasa ndio nikakumbuka kitu baada ya kuona haya maandishi.
                           Hii ni njia niliokua naitumia wakati nimeshuka kwenye train.
          Njia nyingine hii pia nilikua naitumia nikishuka kwenye train kuelekea Globen.

Wednesday, December 12, 2012

WATOTO WA MITAANI

Baadhi ya watoto wa mitaani waliokutwa wamelala pembezoni mwa barabara, idadi ya watoto hao inaongezeka siku hadi siku

WAKONGWE

Kushoto: Mohamed Husein  Chinga, Papa Temu, Mopelo na Tamba maeneo ya Harbours Club Kurasini

Friday, December 7, 2012

NISHATI

Mpaka leo huku mkaa na sie, sie na mkaa

KALI YA LEO

Mwalimu wa History Darasani akiwauliza Wanafunzi
Mwalimu: Enhee, Ni Nani Aliyemuua Chifu Mkwawa?
Mwanafunzi 1: Aku Sio Mimi!
Mwanafunzi 2: Wallah !Sihusiki !
Mwanafunzi 3: Kwanza Mimi Jana Sikuja Shule !
Mwalimu Alipoona Kuwa Wanafunzi Wote Ni Majuha Akaamua Kumuita Mkuu Wa Shule, Mkuu Wa Shule Alipoenda Kuwauliza Lile Swali Mambo Yakawa Vlevle. Ndipo Mkuu wa shule Alipomuita Mwalimu Pembeni Na Kumnong'oneza "Lakini Una Uhakika Muuaji Yupo Darasa Hili?

Wednesday, December 5, 2012

HALI YA BARIDI KALI YENYE KUAMBATANA NA BARAFU YASABABISHA HASARA KUBWA STOCKHOLM

                      Hali ya nje ilikua hivi kiukweli sijui bora nini kati ya joto na baridi

                       Barafu ilikua inaanguka kwa kasi ikiambatana na upepo
 Cha ajabu nikakutana na hawa watoto wao ndio kwanza wanaendeleza michezo kwenye barafu na huku wakifurahi.Kweli kila shetani na mbuyu wake.
 Kwa upande wa mitaa ya mjini hali ilikua hivi.Kwa habari zilizokua zinatangazwa nikwamba hakukua na ndege ilioruka wala kutua leo sweden yote.




 Hapa nadhani mwenye gari yake akitoka atajua ameibiwa maana imefunikwa karibu yote na barafu.



 Kiukweli hali ilikua mbaya sana leo,matrain tabu hata mabasi nayo yalikua tabu sana.
 Hapa kidogo yalipita magari yakutoa barafu ili kufanya magari yaweze pita.Kama unavyoona katikati ya balabala kumejaa barafu.



 Mi nadhani kuna haja yakuitafuta temeke kwa mapumziko ili kupisha hali hii iishe au kupungua kabisa .

Monday, December 3, 2012

DIAMOND-NATAKA KULEWA


LEO UMEME ULIKATIKA MASAA MATATU KWENYE BAADHI YA MAENEO JIJINI STOCKHOLM(SWEDEN)HII NI MARA YA KWANZA KUONA NA KUSIKIA

    Hii ilitokea leo jijini Stockholm(Sweden) majira ya sa kumi na moja jioni.Umeme ulikatika kwa mara ya kwanza toka niingie nchi hii,Ilifanya kutokua na usafiri wa train ambazo zinatumia umeme.
 Usafiri ulikua mabasi tu,Hata mji ulimulikwa na taa za magari kama unavyoona mdau.Kila mtu alilalamika kivyake kwa kweli ila mm wa uswahilini kwenye mgao wa kudumu bongo hapa nikawa sina shaka nikajua hata ukirudi kesho kutwa kazi kwao.
 Kama unavyoona baadhi ya maeneo ya Stockholm kulivyokua na giza la ajabu,ni mishumaa tu iliokua inatamba ndani ya masaa matatu kabla umeme kurudi.
    Baada ya kusubiri sana train bila mafanikio nikaona na mimi ngoja nipande basi nielekee nyumbani.

 Kituo cha train kulikua giza kama unavyoona mdau kila mtu hakuamini kilichotokea kama ndoto hivi.Sijui nini kitatangazwa kutokana na hali hii iliotokea na je waziri wa idara hii ya nishati atajiuzulu?Jibu litakalopatikana tutawawekea hapa wadau ili tutambue jinsi gani Tanesco hawatutendei haki wateja wake.
Hii ndio hali halisi ya baadhi ya maeneo ya mji wa Stockholm Sweden yaliokatika umeme kwa takribani masaa matatu kabla ya kuru.Watu woote wanatega masikio kusikiliza hasara gani shirika la umeme litakua limepata?Kwani wenye viwanda,sehem za biashara na hata majumbani ambao wamepata hasara kutokana na ukatikaji wa umeme masaa matatu italazimika kulipwa kama sheria zao zinavyosema.Sasa kama mpango huu wakulipana ukiletwa bongo shirika la umeme Tanesco itaweza kuwalipa watu?Jibu wanalo wao.