Pages

Monday, December 3, 2012

LEO UMEME ULIKATIKA MASAA MATATU KWENYE BAADHI YA MAENEO JIJINI STOCKHOLM(SWEDEN)HII NI MARA YA KWANZA KUONA NA KUSIKIA

    Hii ilitokea leo jijini Stockholm(Sweden) majira ya sa kumi na moja jioni.Umeme ulikatika kwa mara ya kwanza toka niingie nchi hii,Ilifanya kutokua na usafiri wa train ambazo zinatumia umeme.
 Usafiri ulikua mabasi tu,Hata mji ulimulikwa na taa za magari kama unavyoona mdau.Kila mtu alilalamika kivyake kwa kweli ila mm wa uswahilini kwenye mgao wa kudumu bongo hapa nikawa sina shaka nikajua hata ukirudi kesho kutwa kazi kwao.
 Kama unavyoona baadhi ya maeneo ya Stockholm kulivyokua na giza la ajabu,ni mishumaa tu iliokua inatamba ndani ya masaa matatu kabla umeme kurudi.
    Baada ya kusubiri sana train bila mafanikio nikaona na mimi ngoja nipande basi nielekee nyumbani.

 Kituo cha train kulikua giza kama unavyoona mdau kila mtu hakuamini kilichotokea kama ndoto hivi.Sijui nini kitatangazwa kutokana na hali hii iliotokea na je waziri wa idara hii ya nishati atajiuzulu?Jibu litakalopatikana tutawawekea hapa wadau ili tutambue jinsi gani Tanesco hawatutendei haki wateja wake.
Hii ndio hali halisi ya baadhi ya maeneo ya mji wa Stockholm Sweden yaliokatika umeme kwa takribani masaa matatu kabla ya kuru.Watu woote wanatega masikio kusikiliza hasara gani shirika la umeme litakua limepata?Kwani wenye viwanda,sehem za biashara na hata majumbani ambao wamepata hasara kutokana na ukatikaji wa umeme masaa matatu italazimika kulipwa kama sheria zao zinavyosema.Sasa kama mpango huu wakulipana ukiletwa bongo shirika la umeme Tanesco itaweza kuwalipa watu?Jibu wanalo wao.