Pages

Friday, November 30, 2012

MVAMIZI ANAPOVAMIWA

 Hii imetokea leo maeneo ya Tandika karibu na shule ya msingi Mabatini baada ya watu wanaosadikiwa ni wezi mtego wao kunasuliwa na askari, watu hao wanakawaida ya kuvamia maduka na hutumia bodaboda au pikipiki baada ya kumaliza uharifu wao
 Mmoja wa watuhumiwa waliokamatwa baada ya mipango yao kufeli
 Askari waliofanikisha sakata lote la waharifu hao kukamatwa

Vijana wanaotumika kama madereva wakiwa chini ya ulinzi baada ya kuingia katia mtego wa polisi
Picha: Mdau Qasim Talib

KAMERA YA TEMEKE PAMOJA ILIPOFIKA HOLLAND KWA MARA YA KWANZA

                       Hapa tayari kabisa kwa kuelekea kwa kuelekea Holland,dua muhimu

                      Hapa nikiwa na mdau wa temeke ambae anaishi Holland Nico
    Kamera ya temekepamoja ilitembelea mazoezi ya academy kwa upande wa mpira wa miguu.
    Kwa mchakato huu lazima watokee akina Van persie humu umri huu ndio wakuandaa wachezaji.
                                   Mshambuliaji wa miaka ya baadae huyu hapa

     Hili eneo ilinibidi nitumie usafiri wa baiskeli hili kupata taswira nzuri.Wadau wetu wa kule bongo anaeendesha baiskeli huku si kama hana gari ni sehemu tu ya usafiri,Lakini Kc au Rado akiendesha baiskeli temeke wataanza wamefulia.
                          Vikwangua anga vya maeneo ya Den Haag hivi
                                                   Nikaelekea Rotterdam kidogo



     Nikaona sitowatendea haki watu wa mpira(soccer) kama sikufika uwanja wa Ajax Amsterdam.
                                                Nikafika uwanjani kama unavyouona .




  Hii ni katika picha nilioipenda sana hapa nje ya uwanja wa Ajax kumbe na wenyewe wanamapenzi na Manchester United .Kwa sababu hii kuanzia sasa sisi wote wana temekepamoja tunapenda Ajax.


                              Hapa nilijaribu mpira kabla ya kununua nikaona unafaaa.

               Kiukweli nilitamani kubeba kila kitu hapa kwenye duka la Ajax vyote vizuri

     Hapa nikiwa na mdau Nico yeye ndio alinipeleka hapa maana mtu huwezi jua kila kitu,Kama sehem huijui unaomba upelekwe na huku si kama kule kwetu.Kuuliza 500 kupelekwa 1000 huku bule.


 Nikilipa tayari kwa kua mmoja ya Mtanzania aliewahi kuingia duka la Ajax na kununua bidhaa za Ajax.Na huu mpira nilionunua unasign za wachezaji wote wa Ajax wa sasa hvi.Ukija temekepamoja classic wear utaukuta umekaa kama kumbukumbu.
 Hapa nikiwa katika pozi na mdau wa Holland jamaa nilimkubali sana alinipa ushirikiano mkubwa sana .Na nikamuhaidi kurudi tena Holland kwa matembezi Inshallah.

Huku hakuna kukeep change ingekua timu flani pale kati uswazi wangeanza zengwe kwenye kurudisha change.

 Jamaa nimewakubali sana maana kila unachotaka kujua unafafanuliwa bila shaka.Ila dah maduka yetu kwele kwetu mnaona mteja kama msumbufu badilikeni.
 Baada ya kupata maelezo juu ya kila kitu ikiwepo zile mashine nyuma zakuprint jina na namba kwenye jezi nikaona nizitafute kwa ajili ya temekepamoja classic wear,muda si mrefu huduma iyo itakuwepo dukani kwetu.


                                              Hapa ni central Amsterdam
                   Katikati ya jiji la Amsterdam usiku kama mchana hakuna kulala.
          Kazi na dawa wadau ilifika muda nikazama mitaa ya kati nikaeda kujiuguza.Hawaruhusu kupiga picha huku ila kiubishi nikapata taswira.
 Sikutaka kuondoka Holland bila kufika Eindhoven ambapo kunapatikana timu ya PSV na ndio Ruud Van Nistelrooy alitokea hapa ampaka akapata umaarufu mkubwa akiwa Manchester.Pia Van Bommel
                                      Uwanja wa PSV kwa nje kama unavyoonekana
                                              Uwanja wao unaitwa Phillips Stadio


      Hii ni gari ya mmoja ya mchezaji wa PSV Eindhoven likiwa nje ya uwanja.Nilipewa maelezo yupo ndani nikajaribu kusubiri japo nipate picha sikufanikiwa wadau.
 Kama kawaida nikaingia dukani kushangaa pia kuchukua chochote kitu cha kumbukumbu ili niwe miongoni mwa Watanzania walionunua dukani hapo.
 Kitu cha kwanza kukimbilia ni kupiga picha kwenye jezi na viatu alivyotumia Ruud Van Nistelrooy.Kiukweli huyu jamaa alipokua pale Manchester alikua ananipa sana furaha na leo nimepata kumbukumbu fulani.
       Hii hapa ni jezi na viatu alivyotumia Van Bommel akiwa PSV nikapata picha ya kumbukumbu pia

 Muda wakutafuta kitakachonifaa dukani hapo na kufanya niwe mmoja wao walioingia na kununua hapo.
                       Nikajichukulia kilichonifaa na kunipendeza ila hiki kitambaa chenye picha ya wachezaji wote wa PSV nitakiweka pale temekepamoja classic wear.
                    Hii ni kumbukukumbu ya mechi kati ya PSV na Inter Milan
                                 Viatu na jezi ya Van Bommel