Pages

Saturday, August 31, 2013

Mchezo wa Pool table washika kasi maeneo ya Temeke na vitongoji vyake. Hapo ni CCM kata ya 15 maeneo ya Temeke.

Wachezaji wa pool wakiwa maeneo ya CCM kata ya 15 wakicheza mchezo huo ambao umekuwa maarufu kwa watu wa rika zote.

Moja ya shot iliyokuwa ikipigwa kwenye mchezo huo wa pool.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) Askofu Dokta Moses Kulola afariki Dunia 29-08-2013 kwenye Hospitali ya AMI jijini Dar es Salaam. Mazishi yatafanyika Mwanza siku ya Jumatano.

Baadhi ya waumini wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) Temeke jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye uwanja wa kanisa hilo nyuma ya ofisi ya CCM Wilaya ya Temeke, katika maombelezo na kuaga mwili wa Askofu Moses Kulola.

Umati wa watu uliohudhuria Ibada ya kuaga mwili wa marehemu Askofu Dokta Moses Kulola kwenye viwanja vya kanisa hilo.

Umati wa watu uliohudhuria Ibada ya kuaga mwili wa marehemu Askofu Dokta Moses Kulola kwenye viwanja vya kanisa hilo.

Gari la Makamu wa Rais Dokta. Gharib Bilal likiwasili kwenye viwanja hivyo vya Temeke kwenye Kanisa la EAGT kuhudhuria Ibada ya Maombolezo.

Gari la Makamu wa Rais Dokta. Gharib Bilal likiwasili kwenye viwanja hivyo vya Temeke kwenye Kanisa la EAGT kuhudhuria Ibada ya Maombolezo.

Moja ya magari ya Ikulu yaliyokuwepo kwenye Msiba huo wa Askofu Moses Kulola jana jijini Dar es salaam maeneo ya Temeke kwenye viwanja vya EAGT.


Matukio Mbalimbali yaliyofanyika Mwezi wa 8 ndani ya Wilaya ya Temeke.

Wadau wa Temeke maeneo ya Wailes wakiwa kwenye Uwanja wa Bandari ulipo Tandika jijini Dar es Salaam wakiangalia moja ya mechi ya mpira wa miguu iliyokuwa ikifanyka kwenye Uwanja huo hivi karibuni.Kutoka kushoto ni David Chonde ni shabiki wa Simba s.c, Abed shabiki wa Ndala ama Yanga na Said Mzirary ni shabiki wa simba s.c.

Rajab Kiazi "Ticha" katikati akiwa na wadau wake wakiangalia mpira wa miguu uwanja wa Bandari Temeke hivi karibuni.

He!!! Hivi haya mambo bado yapo!!! Najua utakuwa unajiuliza ni Uwanja gani haya mambo yanafanyika. Huu  ni Uwanja wa Bandari ulipo Temeke jijini Dar es Salaam. Vijana wakuruka ukuta kuingia Uwanjani kwa nia ya kushuhudia moja ya mechi zilizokuwa zikifanyika kwenye Uwanja huo.

Uwanja mkubwa wa Taifa wa mpira wa miguu ambao una uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000. Timu ya Yanga iliahidi wanachama wake kujenga Uwanja utakaochukua watu 45,000 mpaka leo kimya kulikoniiiiiiiiiii.


Chuo kikuu cha ualimu Dar es Salaam DUCE, ni moja ya chuo kikuu kulichopo Temeke pembezoni mwa Uwanja wa Taifa.

Hawa ni walinzi waliopo Uwanja wa Taifa wakikagua baadhi ya tiketi kwenye Uwanja huo.

Bajaj ya Temeke pamoja ikiwa kwenye Uwanja Bandari Tandika. Ukitaka usafiri wa Bajaj ndani ya Temeke piga simu zilizopo hapo juu kwenye blog hii. (Picha kwa hisani ya Temekepamoja blog).

Wednesday, August 28, 2013

YANGA 1 - COAST UNION 1

 Timu zote zikiwa ndani ya uwanja kujiandaa na mechi ya pili ya ligi kuu Tanzania Bara
 wachezaji wa Coast wakiendelea kupasha miili moto
 wachezaji wa Yanga wakijiandaa na mchezo wao
 washabiki waliohudhuria pambano hilo
 Timu zikikaguliwa kabla ya mchezo
 Wadau

 Kipa wa Coast Shaban Kado akiokoa moja ya hatari katika lango lake
 Beki wa coast Juma Nyoso akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga Kavumbagu
 Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli lililofungwa na Kavumbagu
 Wapenzi wa Yanga wakishangilia ushindi

 Kapten wa coast Jerry Santo akiisawazishia timu yake ya Coast kwa penati
 Wachezaji wa Coast wakishanglia
wapenzi wa coast wakishangilia

Tuesday, August 27, 2013

Mashindano Ngumi ya Temeke Open Championships yaanza rasmi ukumbi CCM kata ya 15 Temeke Jijini Dar es Salaam

Mashindano hayo ya wazi ya ngumi za ridhaa yameanza leo ukumbi wa CCM kata ya 15. JUmla ya timu zinazoshiriki ni 22.


Timu 20 zinatoka Temeke na nyingine zilizoalikwa ni mbili tu nazo ni timu kutoka Mpwapwa Dodoma na moja kutoka nje ya Kenya.


Mpenzi wa ngumi Mashindano hayo ni Maweeeee tupu, kiingilio ni Tshs. 2000/= tu. Usikose.


Mchezaji wa timu iliyoalikwa ya Mpwapwa akiwa na kocha wake, mchezaji huyo alichezea kichapo leo kwenye pambano lake.

Vijana wa timu za ngumi za ridhaa wa Temeke wakipambana na kuonyeshana umwamba katika mchezo huo.

Aziz Binzoo au Fadhil ambaye ni Meneja wa Pub ya CCM kata ya 15 akiwa na Mwanachama wa Temeke Jogging wakijadili mambo muhimu yaliyokuwa kwenye Kompyuta Mpakato (Laptop) yao na huku wakiifuatilia kwa umakini Blog ya Temeke pamoja.

Mabondia wakiwa ulingoni wakichapana katika kutafuta Medali.

Bondia akikwepa konde zito kutoka kwa mwenzake kwenye Mashindano hayo ya ngumi jioni hii.

Mwamuzi wa mchezo huo akiinua mkono wa mmoja washindi kwenye mchezo huo.

Mabondia wakiviziana katika moja ya Mapambano ya mashindano hayo.

Viongozi wa mashindano hayo wakiwa kwenye meza kuu wakiangalia mashindano yanavyoendelea.



Saturday, August 24, 2013

ASHANTI YAKARIBISHWA KWA 5 NA YANGA

Timu ya Yanga S.C ikiwa inapasha misuli moto kabla ya mechi yake na Ashanti United ya Ilala, Dar es Salaam.

Timu ya Ashanti United ikiwa inapasha misuli moto kabla ya mechi yake na Yanga S.C ya Jangwani, Dar es Salaam.

Timu zote mbili Yanga S.C na Ashanti United zikiwa zinasalimia Mashabiki kabla ya kuanza mchezo wao.

Purukushani kwenye mechi baina ya Yanga S.C na Ashanti United watoto wa Ilala. Mechi hiyo Yanga ilishinda goli 5-1. Mwanzo mzuri kwa wana Jangwani.(Picha kwa Hisani ya temeke pamoja).

Wachezaji wa Yanga na Ashanti wakiwa wanasubiri kona ipigwe kwenye lango la Ashanti united, Yanga ilishinda goli 5-1.

Moja ya hatari kwenye mechi hiyo.

Mlinda malngo wa Ashanti United akijaribu kuondosha moja ya hatari zilizoelekezwa langoni kwake na washambuliaji wa Yanga.

Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli walilofunga dhidi ya watoto wa Ilala Ashanti United. Poleni Ashanti ndio soka hilo.

Mabeki wa Yanga wakujaribu kuondosha mpira golini kwao.

Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli walilofunga dhidi ya watoto wa Ilala Ashanti United. Poleni Ashanti ndio soka hilo.

Shabiki wa Ashanti United akijipa moyo kwenye mechi yao na Yanga S.c.

Mlinda Mlango wa Yanga Ally Mushafa "Barthez" akiondoa moja ya hatari zilizoelekezwa kwake na washambuliaji wa Ashanti United.

Mabeki wa Ashanti wakimzuia Haruna Niyonzima wa Yanga kuumiliki mpira. Picha kwa Hisani ya Temeke pamoja.

Kipa wa Ashanti akishangaa bao la Yanga kujipatia goli baina ya timu zao.