Pages

Tuesday, August 27, 2013

Mashindano Ngumi ya Temeke Open Championships yaanza rasmi ukumbi CCM kata ya 15 Temeke Jijini Dar es Salaam

Mashindano hayo ya wazi ya ngumi za ridhaa yameanza leo ukumbi wa CCM kata ya 15. JUmla ya timu zinazoshiriki ni 22.


Timu 20 zinatoka Temeke na nyingine zilizoalikwa ni mbili tu nazo ni timu kutoka Mpwapwa Dodoma na moja kutoka nje ya Kenya.


Mpenzi wa ngumi Mashindano hayo ni Maweeeee tupu, kiingilio ni Tshs. 2000/= tu. Usikose.


Mchezaji wa timu iliyoalikwa ya Mpwapwa akiwa na kocha wake, mchezaji huyo alichezea kichapo leo kwenye pambano lake.

Vijana wa timu za ngumi za ridhaa wa Temeke wakipambana na kuonyeshana umwamba katika mchezo huo.

Aziz Binzoo au Fadhil ambaye ni Meneja wa Pub ya CCM kata ya 15 akiwa na Mwanachama wa Temeke Jogging wakijadili mambo muhimu yaliyokuwa kwenye Kompyuta Mpakato (Laptop) yao na huku wakiifuatilia kwa umakini Blog ya Temeke pamoja.

Mabondia wakiwa ulingoni wakichapana katika kutafuta Medali.

Bondia akikwepa konde zito kutoka kwa mwenzake kwenye Mashindano hayo ya ngumi jioni hii.

Mwamuzi wa mchezo huo akiinua mkono wa mmoja washindi kwenye mchezo huo.

Mabondia wakiviziana katika moja ya Mapambano ya mashindano hayo.

Viongozi wa mashindano hayo wakiwa kwenye meza kuu wakiangalia mashindano yanavyoendelea.