Pages

Monday, August 19, 2013

Nguzo ya Umeme iliyoko makutano ya Barabara ya Mbagala na Mtaa wa Kitomondo eneo la Temeke yashika moto upande wa juu. Gari la ZIMAMOTO lafanikiwa kuuzima moto huo.

Gari la Tanesco na la Zimamoto yakiwa eneo la tukio katika harakati za kuuzima moto huo leo jioni eneo la Temeke mwisho makutano ya barabara ya mbagala na mtaa wa kitomondo.

Askari wa Zimamoto walipokuwa katika harakati za kuuzima moto huo.

Eneo la juu kwenye nguzo hiyo ikiwa inaungua huku maji ya Zimamoto yakiwa yamefika juu ya nguzo hiyo. Moto huo ulifanikiwa kuzimwa.

Gari la TANESCO likiwa limeziba barabara hiyo jioni ya leo kwa ajili ya kuweka usalama katika uzimaji wa moto huo hitilafu hiyo bado haijawekwa wazi imesababishwa na nini.

Askari wa zimamoto wakiwa kazini kwenye harakati za kuzima moto huo.(Picha kwa Hisani ya temeke pamoja).