Pages

Thursday, August 27, 2015

MOTO WATEKETEZA WATU TISA BUGURUNI





Nyumba moja maeneo ya buguruni imeteketea kwa moto na kusababisha watu 9 wa familia moja Kufariki, mpaka sasa haijajulikana chanzo cha moto huo ulikuwa nini.

Monday, August 17, 2015

MANJI AFUNGUKA KUKATWA KWAKE



Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ambaye amekatwa kuwania udiwani Mbagala Kuu, amesema alikuwa ni mgonjwa.


Manji ambaye ameshinda kwa kura nyingi katika kura za maoni, lakini akaenguliwa kwa madai hakuwa katika eneo husika, imesababisha kuzua hasira kwa wananchi wa eneo hilo.

Jana wananchi hao walifika katika Makao Makuu ya CCM jijini Dar es Salaam wakitaka kujua hatma ya Manji.

Wengi walihoji kwamba Manji amekatwa kwa fitna zinazozihusisha Yanga na Simba ambazo ni klabu kongwe za soka nchini.

“Nilikuwa mgonjwa, inajulikana. Hali yangu haikuwa nzuri, hivyo nisingeweza kufika,” alisema Manji alipozungumza na SALEHJEMBE.

Hata hivyo Manji alisisitiza, asingependa kulizungumzia suala hilo kwa kuwa bado linasikilizwa ndani ya chama.


“Nafikiri tuache kwanza, subira ni jambo zuri

BASI ZA MWENDO KASI ZAZINDULIWA LEO DAR



WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia amewataka madereva wanaofanyiwa mafunzo ya kutumia mabasi yaendayo kasi kuyazingatia ili kuwa na ufanisi mzuri wa kazi. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).
Amesema hayo katika uzinduzi wa mafunzo ya uongozaji wa mabasi yaendayo kasi chini ya Kampuni ya UDART kwa madereva uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Ghasia amesema katika kipindi hiki cha mafunzo ya utumiaji wa mabasi ya haraka, hakutakuwa na mfumo kamili wa matumizi uliopangwa kutumika katika mabasi hayo na kwamba, kutakuwa na kamera ndani ya mabasi hayo zitakazoweza kuonesha kinachoendelea ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za dharura.
Aidha amewataka watakaofanya kazi ya kuhudumia abiria ndani ya mabasi hayo kuwa wakarimu kwa abiria ili wafike katika vituo vyao kwa usalama na furaha zaidi.
“Tanzania ni nchi ya pili barani Afrika ikiongozwa na Afrika Kusini kutumia mabasi yaendayo haraka na tunatarajia kuwa na mafaniko zaidi ya Afrika Kusini.”
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki amewataka wananchi kuzingatia na kusimamia miundombinu ya mabasi hayo kuepuka kuchakaa mapema.
Amesema mabasi hayo yenye uwezo wa kubeba watu hadi 500,000 kwa nusu saa yatafanyiwa mafunzo kwa madereva chini ya uongozi wa VETA (Chang’ombe) ili kuleta ufanisi mzuri wa kazi.
Mwakilishi kutoka VETA, Samwel Nganya amesema madereva watakaoendesha mabasi hayo ni wale watakapewa leseni za kimataifa na watakuwa na uwezo wa kufanya kila kitu peke yao pasipo na konda kwani mabasi hayo yanaongozwa na dereva tu.
Nganya ameongeza kuwa, madereva wanaohitajika ni 330 lakini madereva 149 ndio waliopatikana kwa majaribio ya vitendo, hivyo bado kuna uhitaji wa madereva 181 zaidi kufikia idadi kamili.
Licha ya kuwapa mafunzo madereva hao Nganya amesema, wana mpango wa kutoa mafunzo mahususi hasa kwa wahudumu wa wateja (customer care) kuhakikisha huduma zinakwenda sawa.

Sunday, August 16, 2015

MANJI AKATWA UDIWANI MBAGALA KUU


YUSUF MANJI Akatwa UDIWANI MBAGALA!!!


YUSUF MANJI akatwa UDIWANI MBAGALA!!!
VURUGU kubwa zimetokea katika ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam baada ya Wanachama wa chama hicho, kupinga hatua ya uongozi wa CCM mkoani hapa kutengua ushindi wa kura ya maoni kwenye ngazi ya Udiwani kata ya Mbagala kuu aliopata Yusuf Manji, ushindi huo kupatiwa na aliyeshika nafasi ya pili katika ngazi hiyo Abubakari Athumani.Anaandika KAROLI VINSENT

TAMASHA LA DEMOKRASIA MBAGALA ZAKHEIM




Tamasha la democrasia Leo viwanja vya mbagala zakheim