Pages

Wednesday, March 30, 2011

JENERALI ULIMWENGU-BAKORA YA WATAWALA NCHINI?


Ukweli kama huu anaoweza kuusema Jenerali Ulimwengu ndio umewafanya watawala wengi kumwogopa mwanaharakati huyu kushinda hata UKIMWI, nani nchi hii asiyemfahamu Jenerali Ulimwengu? Licha ya mwandishi huyu kukumbwa na misukosuko hata ya kutaka kunyang’anywa uraia aah wapi Bwana! Jenerali Ulimwengu hana mpinzani kwa jinsi anavyosimamia ukweli.
     Pengine kwa waandishi wachanga wenye lengo la kufika alipofika Jenerali waanze mapema kukataa rushwa ambazo huwafanya kutumia kalamu zao kusifia uharamia kuliko kukosoa utawala mbovu, Alleluya Mungu Mwenyezi kwa kutupatia Jenerali Ulimwengu mwenye uwezo wa kuwasemea masikini wan chi hii, mwenye uwezo wa kukemea udini na ukabila , mwenye uwezo wa kumhoji hata rais bila uwoga nani kama Jenerali?
     Naam Jenerali Ulimwengu ni bakora ya watawala acha iwachape tu!
         
         Nani kama jenerali, Ulimwengu tumwone
         Nani anayetujali, yu wapi tusemezane
         Nani tumpe kibali, ukweli akawachane
        Jenerali Ulimwengu, kiboko ya watawala.

       Wamesuka njama nyingi, zote zimegonga mwamba
       Jenerali ndio kingi, wanyonge tunampamba
       Wanaoweka vigingi, hao wote ni mafamba
        Jenerali Ulimwengu, bakora ya watawala

   
      Nani asiyefahamu, Jenerali ni shujaa
      Yu wapi tumuhukumu, kwa kuzidi kuzubaa
      Jenerali ni muhimu, Arusha hata kondoa
      Jenerali Ulimwengu, sindano ya mabwenyenye
     

    Wakiwa maofisini, watawala wanalia
     Wakisoma gazetini , hofu inawaingia
     Kwa Jenerali makini, Mwema Raia sikia
     Jenerali Ulimwengu, msome Raia Mwema


    Beti tano nakomea, mengi nimeongelea
    Ulimwengu endelea, uovu kuufunua
    Ukweli tunaujua, wewe unatutetea
    Jenerali Ulimwengu, mtetezi wa wanyonge.



    Nova Kambota Mwanaharakati,
    0717-709618 au 0766-730256
     Tanzania, East Africa
     Jumatano 29 March 2011.


SALAM TOKA INDIA



Asalam alykum sisi ni wanafunzi wa vyuo huku nchini India tunapenda kuwapa salam watu wote wa Kiumeni Tmk pamoja na Tanzania Nzima bila kumsahau babu wa loliondo mungu akijaalia  tunarudi nyumbani mwezi wa sita mwambie babu asimalize (Kikombe)  dawa kwa kuwa huku mishemishe zilikuwa nyingi.
 Temeke pamoja Hongera sana ndg yangu endeleza michakato kwa kuwa tulivyotoka na sasa temeke kuna tofauti kubwa mwana na endelea kutupa habari  za nyumbani hasa hasa za nyumbani

TMK 4 LIFE

Monday, March 28, 2011

TIBA YA LOLIONDO: TAMKO LA WIZARA YA AFYA

TAARIFA YA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
KUPITIA TAASISI ZAKE ZA UTAFITI KUHUSU DAWA YA
MCHUNGAJI MSTAAFU AMBILIKILE MASAPILA WA SAMUNGE - LOLIONDO

MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA), TAASISI YA UTAFITI WA DAWA ASILI YA CHUO KIKUU CHA AFYA YA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI, (MUHAS) MKEMI MKUU WA SERIKALI (CGC), TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU (NIMR)

Taarifa ziliifikia Serikali kuwa, Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, anatibu magonjwa sugu kwa kutumia dawa aliyooteshwa na Mwenyezi Mungu. Inasemekana kuwa, mchungaji alianza tiba hii tangu mwezi Agosti 2010, lakini watu wengi walianza kumiminika kwenda huko Samunge, kuanzia mwishoni mwa mwezi wa pili, mwaka huu wa 2011.

Kufuatia taarifa hii, serikali iliielekeza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa, ufanyike haraka uchunguzi kuhusu dawa hii na itoe ushauri Serikalini ipasavyo. Baada ya kupokea maagizo hayo, wizara iliteua wataalamu kutoka taasisi zake tukiwemo sisi, TFDA, NIMR, Muhimbili kwa maana ya MUHAS, Mkemia Mkuu na tulijumuisha wataalamu wa hapa wizarani, ili kuifanya kazi hiyo muhimu, akiwemo Msajili wa Tiba Asili na Mbadala.

Hapo Machi 7 mwaka huu, sisi TFDA na wenzetu wanasayansi tulifanya safari kwenda Samunge kuonana na kufanya mazungumzo na Mchungaji mstaafu AmbilikileMasapila. Sisi TFDA na wataalam wenzangu wote, tunamshukuru sana mchungaji mstaafu, kwa ushirikiano na msaada mkubwa aliotupa sisi watafiti wote. kwa kuwa, tulifanya mazungumzo kwa masaa kadhaa kuhusu dawa hiyo jinsi alivyoanza, pia, alituonyesha mti unaotumika na alitupa sehemu mbali mbali za mti huo, kwa uchunguzi zaidi. Kadhalika, alituonyesha jinsi anavyotayarisha dawa hiyo na kutupatia sampuli yake iliyokwishategenezwa, tayari kwa matumizi. Sisi TFDA na wataalamu wenzetu tuliondoka nayo, kwa ajili ya uchunguzi zaidi, kwenye maabara zetu.

Baada ya kurejea kituoni Dar es Salaam, kazi ya utafiti wa dawa hiyo ilianza:

Jambo la kwanza kama watafiti, ilikuwa ni kuangalia na kuhakikisha usalama wa dawa ya Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila kwa watu. Uchunguzi uliofanyika, umetoa matokeo ambayo tumeridhika kuwa, dawa kwa kipimo anachotumia Mchungaji mstaafu AmbilikileMasapila, haina madhara yoyote yanayotambulika kwa sasa, kwa matumizi ya binaadamu.

Kazi inayofuata kwetu sisi watafiti baada ya matokeo haya, ni kuchunguza na kubaini, kama kweli dawa hii inatibu magonjwa hayo matano (5), kama anavyoeielezea yeye Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila. Uchunguzi huu utakapo kamilika, matokeo yake yatatolewa mara moja kwa wananchi wote!.

Hata hivyo, ninaomba kuwatahadharisha kuwa, hatua hii ya uchunguzi, si ya muda mfupi. Kwa mujibu wa kanuni na taratibu za kisayansi duniani, tafiti za namna hii zina mchakato unaohitaji muda wa kutosha kukamilisha hatua zake mbali mbali, na pia, kufikia viwango na vigezo vinavyokubalika Kitaifa na Kimataifa. Tunafanya hivyo kwa kuzingatia kuwa, dawa hii ni kwa ajili ya matumizi ya binadamu, na inafuatiliwa na wananchi wetu na mataifa mbalimbali.

Sambamba na utafiti katika hatua hii, pia tunafanya uchambuzi wa kisayansi, katika maabara zetu, kwa sampuli tuliyoichukua kwa Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, kwa kuangalia mambo mengine mawili muhimu kama ifuatavyo:


1. Kwa hatua tuliyofikia na taarifa tulizo nazo za dawa hii mpaka sasa, tumeandaa na tunakamilisha taratibu, ili tuweze kufuatilia maendeleo ya kiafya ya wagonjwa 200, ambao wamekubali kwa ridhaa yao wenyewe, kushiriki katika utafiti huu, ili kuona maendeleo yao kiafya, baada ya kunywa dawa ya Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, kwa maradhi walionayo. Hatua hii, inafuata vigezo vyote vya Kitaifa na Kimataifa.

2. Pia tumeweka utaratibu madhubuti, wa kufuatilia matumizi ya mti huu, kama “mmea tiba”, katika sehemu nyingine za nchi yetu, kwani tuna taarifa kuwa, makabila mbali mbali yamekuwa yakitumia mti huu kama tiba. Makabila hayo ni pamoja na; Wagogo, Wamasai, Wabarbaig na Wasonjo kule Samunge.

Kwa niaba ya watafiti na wataalam wenzangu, ninaomba nimalize kwa kusema kwa muhtasari kuwa:

1. Sisi sote tumeridhishwa kuwa, dawa anayotoa Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, haina madhara yeyote yanayotambulika kwa sasa kwa matumizi ya binadamu. jambo hili mwazoni lilitia wasiwasi Serikali, Wataalam mbalimbali na wananchi kwa ujumla.

2. Kazi hiyo ya utafiti inaendelea ili kubaini magonjwa inayotibu,

3. Katika hatua hii, ninapenda kuwashukuru wataalamu wenzangu wote wa kikosi kazi cha wataalam wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya mkuu wa wilaya, Ngorongoro na ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha na wananchi wote kwa kufanikisha zoezi hili mpaka sasa.

4. Pia sisi tunamshukuru sana Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, kwa ushirikiano alioutoa, kwa timu ya watafiti waliofika kumuona, kuanzia siku ya kwanza mpaka leo hii..

Mwisho ninachukua fursa hii, kuwaomba wananchi wawe na subira katika kipindi hiki ili watupe nafasi tuweze kufanya kazi hii ya utafiti na uchambuzi zaidi, kwa utulivu na umakini wa juu kwani duniani kote, tafiti za aina hii, hazina njia ya mkato, nasi tunaahidi kwamba, tutatoa taarifa ya kina mara utafiti utakapo kamilika.

Asanteni na Ninawashukuru kwa kunisikiliza.(Msaada mjengwa Blog)

Thursday, March 24, 2011

AJALI NYINGINE MOROGORO

Basi la Osaka likiwa limepinduka baada ya kugongana na Fuso kijijni Maseyu barabara ya Morogoro -Iringa. Katika ajali hiyo watu 27  walijeruhiwa. Ajali hii ni pili ambayo hata wiki tokea ilipotokea ajali ya wasanii wa five Star.

Lori la mizigo aina ya Fuso lililogongana na basi hilo. (Picha:Juma Mtanda)Mjengwablog

Tuesday, March 22, 2011

USIKU WA MWISHO WA ISSA KIJOTI wa FIVE STAR

Hii ilikuwa nyumbani kwa Marehemu Issa kijoti Mtoni kwa kabuma alishindwa kujizuia

Hapa baada ya maiti kutoka msikitini na ikiwa njiani kupelekwa makaburini saa 3.00 usiku

kila mtu alitaka kuligusa jeneza lake
Watu wengi sana walijitokeza kwenda kuzika japokuwa ilikuwa usiku
eneo la makaburini
Mwili wa marehemu ukiwa tayari kuhifadhiwa

Baadhi ya ya wananchi waliojitokeza KR Mullah mwenye kofia

watu wakiweka mchanga katika kaburi


Babu Ayoub, Zozo Widda, na Mode Kilindo

Kwa Nyumbani hali haikuwa nzuri wadogo zake wawili waliweza kupoteza fahamu hapa mama mzazi wa Issa Kijoti akijaribu Kumsaidi mwanae aliepoteza fahamu
Mtoto wa Issa Kijoti aliebebwa

Mbele yake Nyuma yetu Mungu amsamehe makosa yake na amlaze mahala pema peponi aminn

MAJERUHI WA FIVE STAR WAWASILI

Hali ilivyokuwa nje ya ukumbi wa Equator Grill watu wengi walijitokeza

Omary Tego akimsindikiza ndani mmoja wa majeruhi katika ajali hiyo

Baadhi ya majeruhi wakiwa eneo la Equator grill baada ya kuwasili kutoka morogoro

akijaribu kuelezea kilichotokea lakini hakuweza kuzungumza

Juma Nature mmoja waliohudhuria

Ankal akiongea na simu pamoja na Saidi fella meneja wa kundi la wanaume family pamoja na baashi ya waandishi wakijaribu kutafakari
Wananchi waliojitokeza katika ukumbi wa Equator grill
Mama Asha Baraka alikuwa kiongozi wa mbele kuhamasisha suala la zima la watu kutoa rambirambi kwa walichokuwa nacho alifanya kazi nzuri mungu ampe nguvu na  kuwasaidia wengine
/>

MAJINA YA WASANII WA FIVE STAR WALIOKUFA NA KUJERUHIWA YATAJWA

Bi Mwanahawa ally akiwa hospitali baada ya ajali kutokea
Lori lililosababisha ajali na kukiwa na baadhi ya wasamalia wema wakisaidia

Costa iliyobeba wanamuziki wa five Star baada ya kupata ajali

Majina ya wanataarabu wa bendi ya Five Star waliokufa katika ajali mbaya ya gari Mikumi mkoani Morogoro yamefahamika akiwemo Issa Kijoti, kiongozi wa bendi hiyo Nasoro Madenge, Mapande, Fembe Juma, Omary Hashim, Tizo ,Omari Tall,Ngeleza Hasan,Hamisa Omari,Maimuna , Haji Msaniwa na mcheza show wa kundi la Kitu Tigo Ilala

Kwa mujibu wa taarifa hii ya uhakika uliyothibitishwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro (RTO) zinadai kuwa waliokufa ni 13 majeruhi 8 na kuwa baadhi ya waliokufa wapo waimbaji ,wapiga vyombo ,mcheza show na mafundi mitambo japo majina ya majeruhi yatakuja hivi punde.
Kwa mujibu wa jeshi la polisi majeruhi mmoja amekufa akiwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro akipatiwa matibabu na kufanya idadi kufikia watu 13
Hivi sasa ndugu wa marehemu hao wapo katika Hospitali ya mkoa wa Morogoro wakiendelea kutambua miili ya wanamuziki hao .
Mtandao huu kwa niaba ya wadau wote unaendelea kuwaombea afya njema majeruhi nane katika ajali hiyo na kumwomba mwenyezi Mungu kuzilaza roho za marehemu wote mahali pema peponi Amina
 
Picha kwa msaada wa blog mbalimbali.

Thursday, March 17, 2011

WANA TEMEKE WAJITOKEZA KUMUAGA MODIBO UK.

Mh Mbunge wa Temeke ABASS MTEMVU na Mke pamoja na watoto wa marehemu wakiweka maua pamoja na mashada kwenye Kaburi la MODIBO.
Baada ya kutoa sala za mwisho Padre akimwaga mchanga

Baada ya ibada Rafiki wa Karibu Saidy Akida  na Ndugu wakibeba jeneza la Marehemu kwenda kuzika.
Mwenyekiti ya kamati ya msiba Bw SIGSBERT akiwa na mtoto wa marehemu baada ya kuzika

Mwili ukiwekwa Kwenye gari.

RBAN PULSE CREATIVE inawaletea Matukio katika picha ya Kumuaga Marehemu MODIBO KEITA DENISS mjini Manchester UK. Leo Jumatano 16.3.10 ndugu, marafiki na jamaa walijumuika katika kanisa la OUR LADY'S CHURCH huko Manchester kwenye Ibada iliyofanyika ya kumuombea na kumwaga marehemu. Baada ya huduma ya kanisa umati wote ulieleka Makaburini kwa ajili ya Maziko.

Watu mbalimbali walijitokeza leo akiwepo kaka wa marehemu Mbunge wa Temeke MH ABBASS MTEMVU , mwenyekiti wa TANZ UK JOHN LUSINGU, MWENYEKITI WA CCM UK MAINA OWINO, JUMUIYA YA KISOMALI Na mataifa mengine.

Marehemu MODIBO atakumbukwa na wengi kwa jinsi alivyokuwa mstari wa mbele kwa kujitolea kwake mhanga kwa ajili ya kusaidia wengine, hayo yalisemwa na watu mbali mbali kuanzia watoto pamoja na mataifa mengine mara baada ya kuzika katika hafla fupi ilioandaliwa na wanakamati.

Hivyo Basi kwa kumuenzi marehemu Jumuiaya ya kitanzania Manchester imeahidi kuendeleza yale yote mema aliyoanzisha na kuwahamasishwa wengine. Mwisho kwa Niaba ya Familia na rafiki wa marehemu inapenda kutoa shukrani zao za dhati kwa wale walijitolea kusaidia kwa namna moja au nyingine wakati wa kumuuguza marehemu na kufanikisha shughuli ya leo. Mungu awabariki wote.

ASANTENI

SHABIKI No. 1 MAN UTD

Saidy Akida akiwa nje ya Uwanja wa Manchester Utd kabla ya Mechi ya UEFA dhidi ya Marseile kutoka Temeke mpaka Manchester

Ndani ya Uwanja wa OT unavyoonekana. Ila huyu jamaa ni mbishi mno

Huyu singasinga sidhani kama kuna mechi kakosa

Red Devil na Saidy Akida katika Picha ya pamoja
Sir Alex akisaini

Saturday, March 12, 2011

KINOMA NOMA- YAKAMILIKA

Pichani: Temba, Linah & Chege kwenye location ya video hiyo mpya

Baada ya kutoka na wimbo wa mwisho Fungeni Mikanda, Chege na Temba sasa wanakuja na mwanadada anayeiwakilisha THT anajulikana kwa jina la Linah. 
Wimbo mpya wa Chege na Temba ukijulikana kwa jina la KINOMANOMA ambao umetoka hivi karibuni kwenye radio station za Bongo , Chege amesema kaeni tayari kwa video hiyo na anaamini hawezi kuwaangusha kwani yeye na Temba kila siku ni kuwaumiza tu mpaka wataje makwao. 
Nyimbo hiyo imekamishamilika na wanaowaomba wadau waweze kuwapigia kura katika tuzo za mwaka
 wimbo bora wa mwaka 
Mkono Mmoja  F158 tuma Kwenda 15747
Video Bora ya Mwaka
Mkono Mmoja S 158
Wimbo bora wa Kushirikisha
Mkono Mmoja W 158

Wanahitaji kura zako







Baadhi ya Vipande vya Picha katika wimbo mpya wa Chege na Temba Kinomanoma

Sunday, March 6, 2011

SIMBA AZUA TAHARUKI MBAGALA


Na Charles Lucas

ALFAJIRI ya jana haikuanza vizuri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, eneo la Mbagala Rangitatu na maeneo mengine ya karibu ambao walikumbwa na taharuki kubwa na kuanza kukimbia hovyo huku na huko kuokoa maisha yao, baada ya kusikia ngurumo za kutisha, za simba jike aliyevamia maeneo hayo.

Harakati hizo za wakazi hao, akiwemo mwandishi wa habari hii anayeishi eneo hilo, kuokoa maisha ziliwalazimu baadhi yao kujifungia ndani ya nyumba, huku akiwa tayari ameshamjeruhi mmoja wa wananchi wa eneo hilo.

Taarifa za kuwepo kwa simba huyo jike zilianza kuvuma kutokana na ngurumo hizo lakini pia baada ya kuonekana na mmoja wa wakazi hao aliyefahamika kwa jina moja la Abdallah aliyepishana naye alfajiri alipokuwa akienda kisimani kwenye mtaa wa Kimbangulile, karibu na mto Mzinga eneo ambalo lina nyumba zilizozungukwa na msitu mdogo.

"Awali baadhi ya watu waliomuona hawakubaini kama ni simba kutokana na giza lakini kadri kulipokuwa kunapambazuka na ngurumo zake tulibaini kuwa ni mnyama huyo hatari ameingia mtaani kwetu," alisema Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Bw. Abdul Kessy.

Alisema baada ya kuhakikisha ukweli huo alipiga simu polisi kwa msaada zaidi ambapo askari watano wa Kituo cha Polisi Kizuiani walifika saa 1:30 na kuanza kumsaka kwenye maficho yake na kumpiga risasi bila mafanikio kutokana na bunduki aina ya SMG kuonekana kutomudu kumuua mpaka zilipotumika silaha 'kubwa' zaidi.

Hata hivyo wakati akiwapigia simu polisi tayari simba huyo alikuwa ameshamjeruhi vibaya mkazi mmoja wa eneo hilo aliyefahamika kwa jina la Nassor Ally, baada ya kumrukia shingoni, hivyo akakimbizwa Hospitali ya Temeke kwa matibabu.

Shambulizi hilo la simba lilitokana na Bw. Ally kumfurumusha mafichoni kwenye gofu la nyumba ambayo ujenzi wake haujaisha alipokuwa amejificha.

Upigaji wa risasi kumdhibiti, uliendelea kwa muda mrefu, ambapo takribani risasi 40 zilitumika kutokana na simba huyo kujicha kwenye vichaka na kutoonekana vema, pia zilipigwa kwa tahadhari ili kuepusha madhara mengine katika eneo hilo la makazi ya watu.

Hatimaye Simba huyo aliuawa majira ya saa 2 asubuhi hivyo kulipua shangwe kwa wakazi wa eneo hilo huku wengine wakitaka kumgawana kwa ajili ya kitoweo, ingawa wengine walionekana kuhitaji viungo vyake kwa shughuli ambazo hazikujulikana mara moja, wakidai 'mnyama huyo ana mambo mengi'.

Polisi wakiongozwa na Inspekta Abdallh Omary walilazimika kupiga risasi hewani ili kuwadhibiti wananchi hao, baada ya hali ya kugombea nyama na viungo vya mnyama huyo, kuanza kuashiria fujo, baada ya watu kulizingira gari la polisi lenye namba PT 2068 Landrover Deffender, wakitaka kupora simba huyo.

Baada ya hali hiyo kutulizwa kwa risasi ya hewani, polisi waliondoka kwa kasi hadi Kituo cha Polisi Kizuiani.

Hata hivyo wakazi hao walifika kituoni hapo kwa maandamano huku wakiimba 'tunamtaka simba wetu', wakijaribu kumchukua kwa nguvu simba huyo. Kutokana na hali hiyo, polisi walilazimika kumhamisha kwa haraka, wakimpeleka kusikojulikana.

Mmoja wa wakazi wa siku nyingi wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Mzee Mahuta aliliambia gazeti hili kuwa ujio wa mnyama huyo katika eneo hilo ni moja ya mwendelezo wa tabia za wanyama kufika kwenye maeneo waliyopata kuishi zamani.

Alisema kuwa katika sehemu hiyo, hapo zamani walikuwapo wanyama hao kwa wingi, ambao walihama kutokana na mabadiliko ya kimazingira, ikiwemo kujengwa kwa makazi ya watu na kuongeza kuwa pamoja na kuuawa kwa simba huyo, anaweza kutokea mwingine tena, kwa kuwa wana tabia ya kutafutana mmoja anapopotea.

Akizungumza na Majira, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, David Misime, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, akisema kuwa hali ya majeruhi haikuwa nzuri hivyo akahamishiwa Hospitali yaTaifa Mhimbili, kwa matibabu zaidi.

TMK MAJITA ORIGINAL-MAZINGIRA

Saturday, March 5, 2011

YANGA 1 vs SIMBA 1

Jangwani
Mnyama
nje ilikuwa shazi
Watu waliambiwa tiketi zimeisha lakini nafasi bado zikawepo
Mchezo ukiendelea
Juma Kaseja akifungwa goli la penalti na Mwasika

Rashid Gumbo akisaliamiana na kocha wake
Kocha wa simba akitoka baada ya kupewa adhabu na refaree
Samatha na Ochan mara baada mchezo kwisha
Kipa wa yanga akitoka nje mara baada ya mchezo kumalizika