Pages

Wednesday, March 30, 2011

JENERALI ULIMWENGU-BAKORA YA WATAWALA NCHINI?


Ukweli kama huu anaoweza kuusema Jenerali Ulimwengu ndio umewafanya watawala wengi kumwogopa mwanaharakati huyu kushinda hata UKIMWI, nani nchi hii asiyemfahamu Jenerali Ulimwengu? Licha ya mwandishi huyu kukumbwa na misukosuko hata ya kutaka kunyang’anywa uraia aah wapi Bwana! Jenerali Ulimwengu hana mpinzani kwa jinsi anavyosimamia ukweli.
     Pengine kwa waandishi wachanga wenye lengo la kufika alipofika Jenerali waanze mapema kukataa rushwa ambazo huwafanya kutumia kalamu zao kusifia uharamia kuliko kukosoa utawala mbovu, Alleluya Mungu Mwenyezi kwa kutupatia Jenerali Ulimwengu mwenye uwezo wa kuwasemea masikini wan chi hii, mwenye uwezo wa kukemea udini na ukabila , mwenye uwezo wa kumhoji hata rais bila uwoga nani kama Jenerali?
     Naam Jenerali Ulimwengu ni bakora ya watawala acha iwachape tu!
         
         Nani kama jenerali, Ulimwengu tumwone
         Nani anayetujali, yu wapi tusemezane
         Nani tumpe kibali, ukweli akawachane
        Jenerali Ulimwengu, kiboko ya watawala.

       Wamesuka njama nyingi, zote zimegonga mwamba
       Jenerali ndio kingi, wanyonge tunampamba
       Wanaoweka vigingi, hao wote ni mafamba
        Jenerali Ulimwengu, bakora ya watawala

   
      Nani asiyefahamu, Jenerali ni shujaa
      Yu wapi tumuhukumu, kwa kuzidi kuzubaa
      Jenerali ni muhimu, Arusha hata kondoa
      Jenerali Ulimwengu, sindano ya mabwenyenye
     

    Wakiwa maofisini, watawala wanalia
     Wakisoma gazetini , hofu inawaingia
     Kwa Jenerali makini, Mwema Raia sikia
     Jenerali Ulimwengu, msome Raia Mwema


    Beti tano nakomea, mengi nimeongelea
    Ulimwengu endelea, uovu kuufunua
    Ukweli tunaujua, wewe unatutetea
    Jenerali Ulimwengu, mtetezi wa wanyonge.



    Nova Kambota Mwanaharakati,
    0717-709618 au 0766-730256
     Tanzania, East Africa
     Jumatano 29 March 2011.


No comments:

Post a Comment