Pages

Tuesday, March 22, 2011

MAJINA YA WASANII WA FIVE STAR WALIOKUFA NA KUJERUHIWA YATAJWA

Bi Mwanahawa ally akiwa hospitali baada ya ajali kutokea
Lori lililosababisha ajali na kukiwa na baadhi ya wasamalia wema wakisaidia

Costa iliyobeba wanamuziki wa five Star baada ya kupata ajali

Majina ya wanataarabu wa bendi ya Five Star waliokufa katika ajali mbaya ya gari Mikumi mkoani Morogoro yamefahamika akiwemo Issa Kijoti, kiongozi wa bendi hiyo Nasoro Madenge, Mapande, Fembe Juma, Omary Hashim, Tizo ,Omari Tall,Ngeleza Hasan,Hamisa Omari,Maimuna , Haji Msaniwa na mcheza show wa kundi la Kitu Tigo Ilala

Kwa mujibu wa taarifa hii ya uhakika uliyothibitishwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro (RTO) zinadai kuwa waliokufa ni 13 majeruhi 8 na kuwa baadhi ya waliokufa wapo waimbaji ,wapiga vyombo ,mcheza show na mafundi mitambo japo majina ya majeruhi yatakuja hivi punde.
Kwa mujibu wa jeshi la polisi majeruhi mmoja amekufa akiwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro akipatiwa matibabu na kufanya idadi kufikia watu 13
Hivi sasa ndugu wa marehemu hao wapo katika Hospitali ya mkoa wa Morogoro wakiendelea kutambua miili ya wanamuziki hao .
Mtandao huu kwa niaba ya wadau wote unaendelea kuwaombea afya njema majeruhi nane katika ajali hiyo na kumwomba mwenyezi Mungu kuzilaza roho za marehemu wote mahali pema peponi Amina
 
Picha kwa msaada wa blog mbalimbali.

1 comment:

  1. poleni sana wafiwa, Mwenyezi Mungu awape subira katika kipindi hiki kigumu.
    Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi.
    AMIN

    ReplyDelete