Pages

Tuesday, May 31, 2011

YA BABU WA LOLIONDO NA USHAURI WA WAMAREKANI


Na Maggid Mjengwa,

INAYODAIWA kuwa tiba ya Babu wa Loliondo, badala ya kuwa msaada kwa taifa, imeanza kuonyesha madhara zaidi ya kiafya, kijamii na kiuchumi. Tuliandika kutahadharisha na kushauri. Tumepuuzwa; maana, kwa wengine, tiba ya Babu sasa ni mradi, na kwa kweli umeanza kugeuzwa kuwa mradi wa kitaifa.

Na kilichojikita katika kuwaacha watu wetu wakitaabika ni unafiki wetu. Tuna maradhi mabaya, na ni sugu. Ndio, miongoni mwetu kuna wenye kusumbuliwa na maradhi ya unafiki. Nitatoa mfano wa juzi tu; nilikaa na wasomi wawili, tena wana digrii zao. Tukazungumzia ya Babu wa Loliondo.

Mimi na wasomi wale tulikuwa na misimamo ya kufanana, tulipinga upotoshaji unaoendelea katika jamii kuwa Babu wa Loliondo, Ambilikile Mwasapile , anatibu ukimwi, kansa, kisukari na mengineyo. Na kwa vile wote tumekwenda shule, hoja kuu ilikuwa hii; kuwa hadi sasa hakuna hata wagonjwa watatu wa ukimwi waliothibitishwa kitaalamu kuwa wamepona ukimwi kwa dawa ya Babu. Badala yake, kuna wengi wamekufa baada ya kuacha kutumia madawa waliyoelekezwa na madaktari watalaamu waliosomea tiba.

Wakati tukiendelea kuzungumza, mara akatokea mheshimiwa fulani, naye akaingia moja kwa moja kwenye mjadala. Alimtetea Babu na kusisitiza kuwa Babu ni lulu ya taifa, lazima aenziwe. Wasomi wale afadhali wangekaa kimya, hapana, walianza kumuunga mkono mheshimiwa kwa hoja nyepesi.
Hawakuwa wapumbavu, walijifanya tu wapumbavu wakiniacha mimi nikipambana peke yangu kuziponda hoja za mheshimiwa yule. Kwa kiasi fulani, niliogopa kuona hulka hii ya wasomi wetu. Wasomi ambao, kwa unafiki, wanashindwa kutetea na kusimamia katika hoja zao za msingi. Na hii, bila shaka, ni moja ya majibu ya swali la kwa nini Tanzania ni masikini?

Hakika, ya Babu wa Loliondo ni aibu yetu kitaifa. Katika karne hii ya 21 nchi yetu inatumia raslimali zake kufanya promosheni ya ndoto ya Mtanzania mmoja kati ya Watanzania milioni 42! Ndio, tunafanya promosheni ya jambo lisilo na uthibitisho wa kisayansi. Si tunaona, haipiti siku bila kusikia habari za Babu wa Loliondo?

Kwa sasa, tunaweza kabisa kusema, kuwa habari za huduma za Babu wa Loliondo zinatangazwa na kuufikia umma kuliko habari za Wizara yeyote ile katika Serikali ya Awamu ya Nne. Babu wa Loliondo si mchezo bwana, ana ‘maafisa habari wake’ wanaowafunika hata maafisa habari wa Wizara za Serikali.

Na katika mzaha huu wa mambo ya msingi kitaifa, tuna maelfu kwa maelfu ya Watanzania wanaotaabika na hata baadhi kufa kwa kuamini kuwa Loliondo kuna tiba, na iko Loliondo tu! Leo, kuna Watanzania walioweka rehani mavuno yao ya mwaka mzima ili wapate nauli ya kwenda kwa Babu. Si wameambiwa, kuwa hata mawaziri wanapanga foleni ya kwenda kupata kikombe cha Babu!
Na wakishapata kikombe wanapiga picha ya ukumbusho, au labda ya kisiasa. Asubuhi yake ’maafisa habari’ wa Babu wameshatundika picha ya waziri ukurasa wa kwanza gazetini! Jimboni kwa mheshimiwa wapiga kura wake watamwona au kusikia kuwa Mheshimiwa naye anaumwa kama sisi, na amepata kikombe cha Babu!

Kikombe cha Babu ni abrakadabra, nilipata kuandika hilo. Na Watanzania, baadhi, kwa hiyari yetu, tumekubali kujifanya, wajinga na hivyo kuwapumbaza wengi wengine. Kwanini? Tulitafute jibu kwa kufikiri kwa bidii.

Hebu jiulize; wakati Shirika la Afya Duniani (WHO), ifikapo Juni mwaka huu, litaadhimisha miaka 30 ya mapambano dhidi ya ukimwi, je, Tanzania, kama nchi, tutakuwa na banda la maonyesho likielezea ugunduzi wa tiba ya ukimwi iliyotokana na ndoto ya Babu?!

Labda ndio maana, magazeti yetu ya lugha ya Kiingereza hayafanyi sana promosheni ya tiba ya Babu. Maana, kama habari za Babu zingepewa uzito kama ilivyo kwenye magazeti yetu ya lugha ya Kiswahili, basi, wana jumuiya ya Kimataifa, wakiwamo wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, huenda wangeshindwa kuamini wanachokisoma.

Maana, wawakilishi wa mashirika kama PSI na FHI yenye miradi ya kupambana na ukimwi nchini na mengineyo wangejiuliza; nini hasa wanachokifanya katika nchi yetu. Na pengine wameshatafsiriwa tunachooandika juu ya Babu kwa Kiswahili chetu!

Si ajabu basi, Ubalozi wa Marekani umekuja na tamko lake Mei 5 mwaka huu. Wamarekani hawa, kwa kuwaonea huruma Watanzania, wameshauri watu wanaotumia tiba mbadala wasiache kutumia dawa walizopewa na madakatri na vile vile waendelee kujikinga na maambukizi.

Na wakaweka msisitizo kuwa, kuacha kutumia dawa hizo za madaktari watalaamu kunafanya dawa hizo zinapotumiwa tena kushindwa kufanya kazi ipasavyo (drug resistance). Na ajabu ya habari ya tamko lile la Wamarekani ilichapishwa katika gazeti moja tu kwa lugha ya Kiingereza - The Citizen, jina la gazeti hilo lina maana ya Mwananchi; ingawa wananchi wengi hawakupata habari hiyo kwa lugha yao!

Kwa hakika, hatuhitaji kuambiwa na Wamarekani juu ya ukweli huu na wajibu wetu. Huu ni wakati kwa wizara inayohusika kufanya jitihada za dhati kutoa tamko litakaloweka bayana kuwa tiba inayodaiwa kutolewa na Babu bado haijathibitika kitalaamu kama inaponya maradhi sugu kama vile ukimwi, kansa na kisukari.

Wakati utafiti huo ukiendelea, umma ukumbushwe kuwa, dawa zinazotambulika kitalaamu kwa sasa ni zile zinazotolewa na madaktari wetu watalaamu. Kwamba wanaokwenda kwa Babu wana ruhusa ya kufanya hivyo, lakini, kikombe cha Babu kinaweza kunywewa pamoja na dawa za hospitalini.
Tufanye hivyo sasa, na ujumbe huo usambazwe kwa nguvu zote na maafisa wa habari wa wizara husika. Ndio, maofisa habari wa Wizara ya Afya nao washindane na ‘maafisa habari’ wa kujitolea wa Babu wa Loliondo!

Watanzania tunapita kwenye kipindi kigumu sana. Na huu ni wakati wa kutafakari kwa kina. Na nimepata kumwuliza jamaa yangu swali hili; mwanadamu unafanyaje unapoamka na kukuta dunia unayoishi ardhi yake imeanza kumegeka na kuchotwa na bahari? Naye akanijibu; ” Huo ndio utakuwa mwisho wa dunia!” Aliyenijibu alikuwa amechoka kufikiri. Nilidhani angetamka kuwa, angeanza kujifunza kuogelea. Maana, kwa kuogelea majini angeweza kukutana na kisiwa, au nchi kavu.

Wanadamu tumejaliwa akili ili tuweze kufikiri. Na kufikiri ndio njia mojawapo ya kuiteka kweli. Kufikiri kunahamisha milima na hata kuiweka kando kuruhusu mwanga upite. Inakuwaje basi mwanadamu anapoacha kufikiri?

Haya ya kwa ‘Babu wa Loliondo’ ni kielelezo cha Watanzania kuamua kuacha kufikiri. Kuna umma uliojifunika vilemba vya ujinga. Umma uko gizani, unahitaji mwanga.

Yumkini wakatokea Watanzania wenzetu wakaoteshwa na Mungu juu ya dawa za tiba kwa mwanadamu. Na hapo wakaingiza suala la imani. Lakini, jambo hilo halituzuii wanadamu kuhoji na kudadisi. Ndio, kuuliza maswali. Na kwa Serikali, jambo hilo haliizuii kufuata taratibu zake za kawaida ikiwamo kufanyia utafiti jambo hilo na kutoa msimamo wa kiserikali.

Hata kama Watanzania watakuwa na uhuru wa kwenda kwenye tiba za imani, lakini msimamo wa Serikali uwepo. Na kwa wengi utabaki kuwa ndio mwongozo; maana, watakuwa wameufanyia utafiti. Nahitimisha.

Sunday, May 29, 2011

Unamfahamu Oprah Winfrey?

Oprah Winfrey, Rais Obama na mkewe Michelle
Moja ya vipindi vinavyotazamwa sana katika historia ya Marekani, The Oprah Winfrey Show, kinamalizika baada ya miaka 25. Kipindi chake kimegusa wengi na kuvuka mipaka ya televisheni.
Kipindi chake cha kwanza, kilichoitwa Namna ya Kumwoa au Kuolewa na mtu wa Chaguo lako, kilipendekezwa kiwe kipindi kinachorushwa mchana kama kipindi chengine chochote cha kawaida.
Lakini baada ya vipindi 4,560, watu maarufu kama Madonna, Beyonce na Tom Hanks wanatarajiwa kutokea kwenye kipindi chake cha mwisho cha kuagwa, kinachorushwa hewani siku ya Jumatano.
Wakati wa miaka hiyo 25, Winfrey limekuwa jina maarufu sana, anayekubalika na wengi na ni mmoja wa matajiri katika ulimwengu huu.
Akimaliza na kuendelea kufanya kazi katika televisheni yake mwenyewe, uwezo wa kupata wageni wanaovutia kwenye habari haliwezi kudharauliwa.
Mwezi huu, Rais Obama alizungumzia kwanini alihitaji kutoa cheti chake cha kuzaliwa hadharani.
Na Sarah Ferguson alizungumzia kwanini hakualikwa kwenye harusi ya kifalme Uingereza.
Kwahiyo ni namna gani ambavyo Winfrey ameweza kufanikiwa? Mambo 10 yanajumuisha ushawishi wake.

ATOA MADAI YA KUDHALILISHWA KIJINSIA, 1986

Oprah Winfrey
Katika hatua yake ya kukiri ambapo baadae ikaja kuwa namna ambavyo anafanya kazi, Oprah aliwaambia watazamaji wake kuwa alibakwa alivyokuwa mtoto.
Si kwamba tu ilisababisha mwanzo wa kampeni isiyo rasmi kuhusu udhalilishaji, iliweka njia kwa msururu wa watu-maarufu wenye mtawaliwa, watu wa kawaida wenye mambo ya kueleza- kukaa kwenye kochi lake na kukiri.
Mwandishi wa vitabu Bonnie Greer, aliyeondoka kwao Chicago mwaka huo huo ambao Oprah alianza kupanda chati mjini humo, alisema: " Amefanya mawazo yaliyo ya wengi yakubalike kirahisi lakini anaielezea kama inamhusu moja kwa moja mwanamke wa Kimarekani mweusi.
"Imekuwepo siku nyingi katika utamaduni wa Kimarekani, lakini Oprah aliileta kwenye televisheni wakati wa mchana. Alianzisha utamaduni wa "mwathirika" kwa mantiki ya uzuri na ubaya.
"Aliingia wakati wa msukosuko wa uchumi katikam iaka ya mwisho ya 80 na mwanzo wa 90, jambo ambalo Wamarekani walitaka kuhakikishiwa: namna ya kuhimili na uzuri wetu.
"Oprah alizungumzia vitu kwa waliokuwa wakitazama vipindi vyake kwasababu alitaka kuonyesha 'uzuri' na 'uaminifu' yana malipo yake hapa duniani.

MKOKOTENI WA MAFUTA, 1988

Akiwa amevaa jeans ya saizi 10, Winfrey aliyekuwa mwembamba aliingia kwenye jukwaa wakati wa kipindi chake na mkokoteni wa mafuta kuonyesha namna alivyopoteza kilo 30 kwa kipindi cha miezi minne kwa kutokula kitu zaidi ya Optifast.
Lakini uzito ukaanza kurudi na ikawa mwanzo wa miongo miwili ya kupunguza kiwango cha kula na kupambana ili kukifanya kiuno kiwe kidogo.
Tim Teeman, mwandishi wa Marekani wa gazeti la Times, alisema: " Ikiwa Oprah atakumbukwa kwa lolote, basi ni umbo lake."
"Unaweza kusema haitoi ujumbe wa kweli lakini unatoa ujumbe sahihi. Jinsi Oprah alivyozungumzia uzito ni hali halisi ya namna watu mbalimbali wanavyopambana na uzito wao.

MICHAEL JACKSON ATOBOA, 1993

Idadi kubwa ya waliokuwa wakiangalia kipindi cha Winfrey illiongezeka alipomhoji Michael Jackson wakati umaarufu wake ulipozidi kupamba moto.
Takriban watazamaji milioni 62 walimwona ndani ya Neverland mtu aliyenaswa kwenye utoto wake, kabla ya madai ya kudhalilisha watoto kuibuka na kumharibia sifa yake.
Wakati wa mahojiano yaliyochukua dakika 90, alimwambia alikuwa akiumwa maradhi ya ngozi na alikana kuwa alilala kwenye chumba chenye gesi ya oksijeni.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Michael kuzungumza kwa muda mrefu katika kipindi cha miaka mingi na ilionekana kuwa jambo la kipekee kwa kipindi cha Winfrey, na kuandikwa kwenye vichwa vya habari vya vyombo mbalimbali duniani na kusaidia kuimarisha sifa yake.

ELEN DEGENERES AJITOA HADHARANI, 1997

Mchekeshaji wa Marekani, mwendesha kipindi kwenye televisheni na muigizaji Ellen DeGeneres alisema hadharani kuwa anafuata mapenzi ya jinsia moja kwenye kipindi hicho.
Mahojiano hayo yalifungua mlango upya kwa kazi ya DeGeneres ambaye alianzisha kipindi chake mwenyewe cha mahojiano.
Mvuto wa Winfrey kwa wanawake wengine umejadiliwa sana.
Greer alisema, " Ni mtetezi wa wanawake kwa minajil ya kwamba amejenga milki yake mwenyewe na mfano wake umesababisha wanawake wengine kuiga."
"Ni wazi kwa hakika anakupa msukumo, hodari sana na mwerevu na amefanya mambo mazuri. Kila mmoja anamtakia kheri, pamoja na mimi.
Licha ya kukiri kuhusu masuala yake ya uzito na udhalilishaji, na uwezo wake wa kufanya wengine kama DeGeneres kuwa wazi, inashangaza namna ambavyo tunajua machache kuhusu Winfrey mwenyewe, alisema Greer.
" Kila mmoja aliye karibu yake hazungumzii mambo yake. Ni miongoni mwa watu maarufu Marekani ambao tunajua kila kitu na hatujui kitu vile vile.

TOM CRUISE JUU YA KOCHI, 2005

Huenda wakati utakaokumbukwa zaidi kwa Oprah ni pale Tom Cruise alipoanza kuchekacheka, akiruka juu na chini kwenye kochi lake alipoelezea penzi lake kwa mpenzi wake mpya, Katie Holmes, ambaye kwa sasa ni mke wake.
Teeman alisema tangu wakati huo tendo lake hilo limekuwa likifanyiwa dhihaka na kuigwa kwa kubezwa. Huu ni wakati ulioainisha kazi yake, baada ya filamu kama Top Gun, Cocktail au Mission Impossible.
"Oprah alionekana kumahanika, akifikiria 'Anafanya nini?' Kazi yake iliporomoka kwa muda lakini amerudi."
Watu maarufu hushiriki kipindi cha Oprah kuondosha pepo mbaya au kukiri jambo la kimapenzi, alisema, na wanajua hatowapa wakati mgumu.

JAMES FREY ALAANIWA, 2006

Moja ya ushawishi mkubwa aliokuwa nao Winfrey umekuwa katika ulimwengu wa uchapishaji vitabu, klabu yake ya vitabu imekuwa kisifiwa kwa kutengeneza mamilioni kwa waandishi ambao vitabu vyao hujadiliwa kwenye klabu yake.
Hakuna pahala ambapo ushawishi wake ulionekana kama katika kesi ya James Frey. Kitabu chake cha A Million Little Pieces, iliyoelezea hadithi yake ya kujikw

KIAMA CHA KWELI OCTOBA 21


Kiama hakikutokea jumamosi mei 21 kwakuwa Mungu aliwaonea huruma watu wake lakini oktoba 21 mwaka huu kiama kitatokea kweli na kuua watu wote ambapo watu wema watapaishwa mbinguni kuonana na Yesu. Baada ya kujichimbia hoteli akiwakimbia watu waliokuwa wakitafuta ukweli kwanini kiama hakikutokea mei 21 kama ilivyotangazwa, Mchungaji Harold Camping amejitokeza na kusema kuwa kiama cha kweli kitakuwa oktoba 21 na dunia yetu hii itaangamizwa miezi mitano baadae.

Mchungaji Camping mwenye umri wa miaka 89 alijitokeza toka machimboni na kutangaza kwenye radio yake ya Family Radio kuwa walikosea mahesabu ya biblia wakati wa kutabiri mwisho wa dunia.

Lakini Camping aliongeza kuwa kiama cha kweli kitatokea mnamo oktoba 21 mwaka huu.

Mchungaji huyo wa California alisema kuwa kutotokea kwa kiama mei 21 kumetokana sana na nguvu za kiroho na wala si nguvu za asili.

Camping aliongeza kuwa Mungu aliwaonea huruma watu kuwaangamiza kwa matetemeko makubwa ya ardhi lakini hiyo oktoba 21 hakutakuwa na huruma ya Mungu na kiama kitatokea kweli.

Akiongea kwa muda wa lisaa limoja na nusu, mchungaji Camping alisema "Hakutakuwa na sababu za kiroho ifikapo oktoba 21, dunia itaangamizwa na itatoweka ndani ya muda mchache".

Thursday, May 26, 2011

SAMATTA ATAMBULISHWA RASMI MAZEMBE


Baadhi ya wachezaji wa TPMAZEMBE wakishuhudia utambulisho huo.

Wapenzi waliojitokeza kumpokea Samatta

Rais wa wa mazembe akiingia ndani ya uwanja

Samatta akijitambulisha mbele ya Wapenzi wa TPMAZEMBE

Wednesday, May 25, 2011

BAISKELI YAMUWEKA PABAYA

Huyu Kijana ni mtoto wa maeneo ya Temeke Wailes kwa kifupi jina lake Kobelo alikutana na balaa Morogoro alipotaka kujaribu kuiba baiskeli yaliyomkuta sidhani kama anaweza kurudia ila tunamuombea Mungu ampe utambuzi na ajijue yeye ni nani na ana thamani gani.

Kobelo Omary Kwa Temeke alikuwa anakaa Mtaa Ngarambe maeneo ya Wailes sijui nini kilimkumbuka.

Polisi akijaribu kuwazuia wananchi wenye hasira.

Wananchi hawakutaka aondoke hivihivi
Hali ilivyokuwa baada ya kupata kipigo
Jitambue ndugu yangu kijana wetu wa Temeke usije ukakukuta umauti wako kwa sababu ya vitu vidogo.
Asante Kessy Karama. darstockholm

Vuvuzela "huenda inaeneza maradhi"

Vuvuzela chombo kilichotumika kwa kushangilia hasa na mashabiki wa soka kwenye Kombe la Dunia la soka mwaka jana- sio tu inasababisha uchafuzi wa mazingira kwa kelele, lakini huenda pia ikasababisha maradhi, kwa mujibu wa wataalamu.
Vuvuzela likipulizwa
                                                                    Vuvuzela likipulizwa
Upulizaji kidogo tu wa Vuvuzela hutoa mate mengi sawa na yanayotoka wakati mtu akipiga chafya, yakisafiri kwa mwendo wa kasi ya mara milioni nne kwa sekunde moja kwa kila tone, hii ni kwa mujibu wa jarida la PLoS One.
Katika eneo lililofurika watu, mtu mmoja akipuliza vuvuzela linaweza kuwaathiri watu wengine wengi kwa magonjwa yanayosambazwa kwa kuvuta hewa kama mafua na kifua kikuu.
Waandalizi wa michezo ya Olympiki mjini London mwaka 2010 bado wanafikiria iwapo waruhusu vuvuzela kutumika au la.
Dr Ruth McNerney, aliyeendesha utafiti wa hivi karibuni katika shule inayohusika na masuala ya usafi na maradhi ya nchi za joto ya London - London School of Hygiene & Tropical Medicine, amesema "upulizaji wa chombo cha vuvuzela" huenda kinahitajika kuliko kukipiga marufuku.
"Kama ilivyo wakati wa kukohoa na kupiga chafya, hatua zinapaswa kuchukuliwa kuzuia uenezaji wa maradhi, na watu wenye maradhi ya kuambukiza washauriwe wasipulize vuvuzela zao karibu na watu", alisema.
Kamati yake iliyochunguza hatari zinazoletwa na upulizaji wa vuvuzela, waliwatumia watu wanane waliojitolea kupuliza vuvuzela.
Kwa wastani chembechembe zinazotoka kwenye mapafu, 658,000 kwa lita ya hewa zilitolewa kutoka kwenye vuvuzela.
Matone hayo ya mate yaliruka angani kwa kiwango cha mara milioni nne kwa sekunde.
Kwa kulinganisha, wakati watu hao waliojitolea walipotakiwa kupiga kelele, waliweza kutoa mate kiasi cha chembechembe 3,700 tu kwa lita kwa kiwango cha 7,000 kwa sekunde.BBC

Monday, May 23, 2011

RAHA NA KARAHA YA MAPENZI

Bi harusi akijaribu kuokolewa

Ni ukweli usiopingika kuwa mapenzi ni matamu sana pale panapokuwa na maelewano na maridhiano baina ya wapendanao lakini mapenzi hayo hayo huwa sawa na sumu kali inayoua pale mambo yanapokuwa kinyume, mfano halisi ni mwanamke huyu wa nchini China ambaye aliokolewa sekunde ya mwisho kabla ya kujiua kwa kujirusha toka ghorofa ya saba baada ya bwana harusi wake kumkimbia na kwenda kumuoa mwanamke mwingine siku moja kabla ya harusi yao. Maandalizi yote ya harusi yakiwa yamekamilika, siku moja kabla ya harusi kufungwa bwana harusi alimtosa bi harusi na kwenda kumuoa mwanamke mwingine siku hiyo hiyo.

Kwa uchungu wa kuyakosa mapenzi ya aliyekuwa bwana harusi wake, bi harusi akiwa amevalia shela la harusi alipanda kwenye dirisha la ghorofa ya saba akiwa na nia ya kujiua kwa kujirusha hadi chini.

Hapa tunamzungumzia mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Li mwenye umri wa miaka 22 ambaye alisababisha mtafaruku mkubwa alipojaribu kujirusha toka ghorofa ya saba akiwa amevalia shela lake la harusi.

Uamuzi huo wa Li ulitokana na machungu ya kukimbiwa na mumewe mtarajiwa ambaye siku moja kabla ya harusi alivunja uhusiano wao na kwenda kumuoa mwanamke mwingine siku hiyo hiyo.

Li kabla hajajirusha chini mwanaume mmoja aliyewahi kufika ghorofa ya saba alimng'angania Li na kumvuta ndani huku watu wengine wakimsaidia kumvuta ndani mrembo huyo aliyeonja chachu ya mapenzi ili kunusuru maisha yake.

Tukio hilo lililochukua dakika kadhaa liliwavuta watu wengi ambao walijazana chini wakisubiria kuona kitakachojiri.

Baada ya dakika chache za patashika hilo, polisi kwa kushirikiana na raia walifanikiwa kumvuta ndani ya jengo hilo na hivyo kunusuru maisha ya mrembo huyo.
WANAFUNZI wa shule ya Sekondari Kigogo ya jijini Dar es Salaam, wameadhimia kuandamana hadi Ikulu kumuona Rais Jakaya Kikwete kwa kupinga uwepo wa nyumba ya kulala wageni iliyokuwandani ya eneo la shule


hiyo Wanafunzi hao ambao mwishoni mwa juma walionekana kufanya fujo shuleni hapo kupinga uwepo wa nyumba hiyo bubu iliyopo katika maeneo ya shule hiyo iondolewe kwa kudai inawachanganya katika masomo yao ya kila siku.

Nyumba hiyo ya kulala wageni ipo pembezoni mwa madarasa ya shule hiyo ya kata ambapo wanafunzi hao wamedai kuchanganywa kutokana na miziki na pilikapilika za watu za kila siku zinazofanywa katika nyumba hiyo jambo ambalo linaenda kinyume na na sheria za haki elimu na kudai kuwapotezea usikivu wawapo darasani ikiwemo na kuwafunza maadili mabovu wawapo shuleni

Hata hivyo wanafunzi hao walishafika ngazi za chini kuripoti tukio hilo lakini imeonekana taratibu za kisheria zinakwenda taratibu na kuonekana watendaji kushindwa kuifungia nyumba hiyo.

Hivyo wanafunzi hao wameadhimia kufanya maandamano ya amani kwenda kwa Rais Kikwete kumweleza kero hiyo ili aweze kuwasaidia.

Wakilalama wanafunzi wamedai “makelele ya wateja wa gesti yanatusumbua wakati wa masomo, mana ni vurugu badala tumsikilize mwalimu wakati mwingine wateja wanagombana vyumbani na kutupigia makelele, mara nyingine mavazi yanayovaliwa na baadhi ya wateja si stahili yanatuletea maadili mabovu.

Kwa kuwa madirisha ya gesti yanatizamana na madirisha ya shule mara nyingine ni rahisi kuona yanayotendeka ndani ya vyumba kwa kuwa madirisha hayana pazia, walilalama wanafunzi hao kwa jazba

Vilevile walilalamikia tabia ya kuona wasichana wenye umri mdogo wakiwa wanaingia na watu wenye rika kubwa mithili ya baba zao ni hali ambayo wanadai kuwaumiza kisaikolojia.

Hata hivyo wanafunzi hao wameadhimia kufika kwenye kituo wanachoshughulikia haki za watoto ili kupata msaada zaidi wa suala hilo

Nyumba hiyo ya kulala wageni ’Gesti bubu’ iliyopo ndani ya eneo la shule hiyo imedaiwa na mmoja wa wahusika kuwa hulipiwa kodi kihalali na imesajiliwa kwa mujibu wa sheria zote za Serikali ya Tanzania kwa jina la The Queen Guest House.

Kiama Hakijatokea, Mchungaji Aingia Mitini

Kiama kilitakiwa kiwe jana saa 12jioni lakini hakikutokea kama kilivyotabiriwa na mchungaji wa nchini Marekani ambaye alitumia pesa nyingi sana kuwaonya watu kwa miezi kadhaa kuwa kiama kingetokea jana mei 21 kwenye majira ya saa12jioni.

Wafuasi na waumini wa Mchungaji Harold Camping wamebaki hawajui la kufanya baada ya kuhubiriwa kwa miezi mingi kuwa kiama kingetokea jana jumamosi saa 12 jioni.
Mwanaume mmoja na familia yake walisafiri kilomita 4830 toka Maryland hadi California mbele ya ofisi ya radio ya mchungaji Camping na kusubiri kupaishwa mbinguni kwenda kuonana na Yesu kama walivyohubiriwa na mchungaji huyo.

Kiama hakikutokea kama walivyotarajia, walibaki kwenye gari lao masaa yakikatika na sasa wakiwa na kazi nyingine ya kusafiri kilomita zingine 4830 kurudi nyumbani kwao.

Mwanaume mwingine mwenye umri wa miaka 60, Robert Fitzpatrick kwa kuamini kuwa mwisho wa dunia umefika na kwa kuamini mafundisho ya mchungaji Camping, alitumia dola $140,000 toka kwenye akiba yake ili kuchapisha mabango na vipeperushi vya kuwaonya watu kuwa mwisho wa dunia ni mei 21.

Akiwa amesimama kwenye viwanja vya Times Square jijini New York akiwa amezungukwa na wapita njia, Fitzpatrick, alikuwa akisoma mistari ya biblia huku akigawa vipeperushi akiwataka watu wajiandae kwa kiama ambacho kingeanza saa 12 jioni ya mei 21.

Masaa yalikatika na kiama hakikutokea, Fitzpatrick kwa mshangao alisema "Siwezi kukwambia ninavyojihisi hivi sasa, saa 12 imekuja na kuondoka haraka haraka, sielewi kwanini hakuna kitu chochote kilichotokea".

Mchungaji Camping mwenyewe hajaonekana tena na amekaa kimya na hadi sasa hajasema chochote kwanini kiama hakikutokea kama alivyotabiri na kuwahabarisha watu kwa miezi kadhaa kabla.

Hata hivyo bado waumini wengine wa mchungaji Camping wanaendelea kumuamini mchungaji huyo wakisema kuwa kuchelewa kutokea kwa kiama ni mtihani mwingine toka kwa Mungu juu ya imani zao.

Wakati huo huo watu wasioamini kuwepo kwa Mungu wameendelea kujirusha wakihoji hicho kiama kiko wapi?.

HUKUMU YA EPA



Habari zinasema imetangazwa katika taarifa ya habari mchana huu, Radio One Stereo kuwa watuhumiwa wawili wa kesi ya kwanza ya wizi wa fedha kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ndugu wawili, Rajabu Maranda na Farijala Hussein imetolewa na wamehukumiwa kwenda jela miaka 5 na kuilipa Serikali fedha iliyoibwa la sivyo, mali zao zitafilisiwa kwa mujibu wa sheria.
Jopo la mahakimu watatu ndilo lililotoa hukumu hiyo ambayo awali ilikuwa na jumla ya miaka 21 lakini kwa kuwa watatumikia adhabu hizo kwa wakati mmoja, basi ikaamriwa kuwa watatumikia miaka 5 kila mmoja.

Mahakimu hao ni Ilvin Mgeta, Saul Kinemela na Focus Bambikye na waliitoa hukumu hiyo katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, baada ya watuhumiwa kupatikana na hatia.

Awali, watuhumiwa walikuwa wakikabiliwa na mashitaka 8 lakini walikutwa na hatia katika mashitaka 6 miongoni mwao yakiwemo ya kughushi na kuwasilisha hatia za uongo ambazo ziliwapatia ingizo la shilingi bilioni 1.8 mali ya BoT kwa njia ya udanganyifu wakonyesha kuwa, Kampuni ya Kiloloma and Brothers imepewa idhini ya kukusanya deni la kampuni ya BC Cars Export ya Mumbai, India.

Mojawapo ya makosa yaliyofutwa ni lile la kula njama kwa nia ya kutenda kosa na wizi.

Wakili Mkuu wa Serikali Boniface Stanslaus aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa washitakiwa kwa kuzingatia kiasi kikubwa cha fedha kilichochukuliwa na madhara yaliyotokea kwa wananchi.

Wakili wa watuhumiwa, Majura Magafu, amesema wateja wake wanakata rufaa.

Maranda na Hussein wanakabiliwa na kesi nyingine tatu za EPA, zikiwa ni miongoni mwa kesi kadhaa za EPA zilizofunguliwa katika Mahakama ya Kisutu. Kesi hizo zinawakabili wafanyabiashara maarufu na waliokuwa watumishi wa BoT.
Farijala Hussein na Rajabu Maranda

Saturday, May 21, 2011

BUZA NA NAULI ZA DALADALA

Hali ilivyo katika kituo cha Tandika 

BAADHI ya wakazi wa Buza wilayani Temeke, wamelalamikia kutozwa nauli kubwa za usafiri wa daladala kinyume cha  viwango vilivyowekwa kisheria.

Wakizungumza  kwa nyakati tofauti jana, wananchi hao walisema wamekuwa wakitozwa nauli ya kati ya Sh500 na Sh1,000 badala ya Sh300 iliyowekwa kisheria.Mmoja wa wananchi hao, Abdallah Zimbwe, alisema ni miezi miwili sasa tangu waanze kutozwa viwango hivyo vya juu.

"Wanatutoza nauli kubwa na tukigoma kulipa, basi wanakataa kuleta magari yao Buza. Sasa kwanini tulipe kiwango tofauti na kile kilichopendekezwa kisheria ambacho ni Sh300,"alihoji Zimbwe.

Mkazi mwingine aliyejitambulisha kuwa ni Neema Samson, alisema hali inakuwa mbaya zaidi hasa nyakati za jioni wanapolazimika kulipa hata Sh1,000 kwa safari.
Licha ya watu wazima kutozwa viwango hivyo vikubwa, wanafunzi nao wamelalamikia kutozwa hadi Sh 200 badala ya Sh 50 iliyopendekezwa kisheria.
"Na hata hiyo Sh200 unalipa mlangoni kabla hujapanda gari na wakati mwingine tunakataliwa kabisa kupanda magari, utakuta unatoka shule mapema unakaa kituoni zaidi ya saa nne ukisubiri usafiri,"alisema Anjela Joseph, anayesoma katika Shule ya Sekondari Kibasila.
Kwa upande wao, madereva waliozungumza n, walisema wanatoza viwango hivyo kutokana na ubovu wa barabara waliodai kuwa unasababisha magari yao kuharibika.

"Yaani unaweza kwenda safari moja ukarudi unajikuta unapeleka gari gereji , barabara ni mbovu sana inaharibu magari yetu,"alisema Juma Abdallah ambaye ni mmoja wa madereva hao.

Friday, May 20, 2011

MAPENZI SHULENI

Vurugu kubwa ziliibuka jana baada ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mbagala kuvamia shule ya Nzasa na kuanza kuwashambulia baadhi ya wanafunzi kwa fimbo na mawe.

Tukio hilo limetokea jana saa 7 mchana ambapo chanzo kikubwa inadaiwa  kuwa, ni mahusiano ya kimapenzi ambapo kuna mwanafunzi wa kike mmoja alikuwa akiwachanganya wanafunzi hao wa Mbagala na Nzasa.

Akizungumza na gazeti Dar Leo kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Missime, amesema kuwa, hadi sasa jeshi lake linawashikilia wanafunzi wanne kuhusiana na vurugu hizo.  Akasema wanafunzi wa Mbagala mmoja wao alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na msichana ambaye pia alibaini kuwa ana mahusiano na mvulana mwingine anayesoma Nzasa ambapo aliamua kwenda na kundi lake kumfanyia vurugu.

Kutokana na vurugu hizo, wanafunzi sita walipata mshtuko na walikimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Kamanda Missime amesema waliokamatwa katika vurugu hizo ni Shana Reagan wa kidato cha nne 'D', Twahir Sultan kidato cha 3 katika sekondari ya Nzasa, Said Muhibu mkazi wa Zakhem alijiingiza kwenye vurugu hizo na Reuben Hosea, kidato cha 3 katika Sekondari ya Mbagala.

"Tumeamua kuwashikilia hawa watuhumiwa kwa kuwa wanaonekana kama ni wahuni na si wanafunzi kwani wamewezaje kujiingiza kugombea mwanamke wakati bado wapo shuleni? Hivyo tukijiridhisha tutawafikisha Mahakamani," amesema Kamanda Missime.

Mazungumzo baada ya habari...
Hawa yaelekea hawajawahi kusikia nyimbo zenye mafunzo kama huu wa Mbaraka Mwinshehe na kufuata mafunzo yake. Sijui wanasikiliza nyimbo zinazochochea kuwakiana tamaa ya mapenzi tu? Ndiyo shida yake.

SHEIKH YAHYA HUSEIN AFARIKI

Mnajimu wa Afrika Mashariki Shkh Yahya hussein amefariki dunia leo nyumbani kwake saa 4 asubuhi mwembe chai jijini Dar es salaam. Alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo.Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amin

Wednesday, May 18, 2011

DAR ES SALAAM HII! TANDIKA, POSTA HAKUNA TOFAUTI



Baadhi ya Maeneo ya katikati ya jiji picha za juu




Huku ndio tunakokaa sisi tandika

Hii ndiyo Bongo isiyokuwa na ubongo!

Ukitoka foleni, mchana foleni, ukirejea nyumbani foleni. Mvua ikinyesha ndiyo kabisa vuta shuka ulale garini na wasiokuwa na magari binafsi wenzangu na mimi wa daladala, basi unauchapa hadi unapitiliza kituo, salama yako umtaarifu konda na mapema tu akustue ukifika kwenu. Omba naye "asiboreke" alale. tehe!

Mgao wa umeme

*Nchi gizani tena
*Mikoa 12 kukosa umeme


WANANCHI wa mikoa 12 wataendelea kupata machungu ya mgao wa umeme, baada ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kutangaza tena ratiba ya mgao huo.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo asubuhi kwenye vyombo habari
kutoka kitengo cha mawasiliano Makao Makuu TANESCO, na kusainiwa na Ofisa Uhusiano, Badra Masoud.

Imeeleza kuwa, mgawo huo utahusisha Mkoa wa Dodoma, Morogoro, Mara, Tabora, Pwani, Arusha, Kilimanjaro, Shinyanga, Iringa, Mbeya, Manyara na Dar es Salaam katika wilaya zote za Temeke, Ilala na Kinondoni.

Taarifa hiyo imesema kuwa, umeme huo utaanza kukatika saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni, ambapo katika maeneo mengine, utakatika kuanzia saa 12 jioni na kurejea saa 5, usiku.

Hata hivyo, taarifa hiyo imesema kuwa, maeneo mengine mgawo utakuwa ukianzia saa 10 jioni hadi saa 5 usiku, wakati maeneo mengine yatakuwa giza kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni.
 

Monday, May 16, 2011

SOKO LA SAMAKI

Soko la samaki kigamboni mmoja wa wachuuzi samaki akiwatengeneza samaki katika soko la Kigamboni

Kitu cha Pweza na Ngisi

Saturday, May 14, 2011

MWANAUME KAZINI

Man United mabingwa wa Ligi ya England

Bao la mkwaju wa penalti lililoonekana la utata lililofungwa na Wayne Rooney lilitosha kuipatia Manchester United ubingwa na kuvunja rekodi ya kunyakua ubingwa wa Ligi ya Soka ya England kwa mara ya 19 katika uwanja wa Ewood Park.

Sir Alex Ferguson
Sir Alex Ferguson


Pointi moja ilitosha kwa meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya England kwa mara ya 12 tangu aanze kuifundisha timu hiyo katika pambano dhidi ya Blackburn.
Manchester United ilionekana ingepoteza mchezo huo hadi mlinda mlango wa Rovers Paul Robinson alipofanya makosa ya kumuangusha chini Javier Herndandez na wageni wakapatiwa nafasi ya kupiga mkwaju wa penalti.
Rooney alifunga mkwaju huo wa penalti na kuisawazishia timu yake na kuwafanya mashabiki wa timu hiyo kuhanikiza kwa shangwe za ubingwa.
Blackburn walikuwa wa kwanza kupata bao lililopachikwa na Brett Emerton baada ya ngome ya United kujichanganya akiwemo mlinda mlango wake Thomas Kuszczak.
Lakini bao la mkwaju wa penalti katika dakika ya 73 lilitosha kuibua shangwe za ubingwa kwa mashabiki ambapo sasa Manchester United imepata pointi 77 ambazo timu inayofuatia Chelsea hata ikishinda mechi zake zote mbili zilizosalia haitaweza kufikisha pointi hizo.

Friday, May 13, 2011

WEMA+UJINGA=CHUKI

WEMA NI KITENDO CHA DHATI, KINACHOTENDWA NA MAPENZI YA MOYO WA NAFSI HUSIKA. SIKU ZOTE WEMA JAMBO JEMA HUTENDWA NA NAFSI KWA MAPENZI YA MOYO WAKE. ILI MTU AWEZE KUTENDA WEMA, NILAZIMA AJUWE SABABU, UMUHIMU, FAIDA NA HASARA ZA WEMA HUSIKA. WEMA UNATOKANA NA FAHAMU YA NAFSI JUU YA MSINGI WA MSAADA WA WEMA HUSIKA.

UJINGA NI KIFAA CHENYE UKOSEFU WA FAHAMU, KILICHOMO NDANI YA NAFSI YA MTU HUSIKA. UJINGA MSINGI WAKE NI KIZA KINENE. USICHOKIJUWA UNAHITAJI KUKIJUWA, ILI UWE NA FAHAMU JUU YAKE. ELIMU NDIO DAWA YA UJINGA, KWA SABABU UFUNGUO WA MLANGO WA UJINGA NI ELIMU, HUWEZI KUFUNGUWA MLANGO WOWOTE BILA UFUNGUO, NDIO MAANA TUNASEMA UKITAKA KUFUNGUWA MLANGO WA UJINGA, ILI UPATE MWANGA WA FAHAMU, UNAHITAJI ELIMU YA KUTOSHA.

CHUKI, NI KIFAA CHENYE SUMU NDANI YA NAFSI HUSIKA.
KIFAA HICHO (CHUKI) KINAKAA NDANI YA MOYO WA BINAADAMU. MOYO WA BINAADAMU SIKU ZOTE HUPENDA YULE ANAEUPENDA NA HUMCHUKIA YULE MWENYE KUUCHUKIA, NDIO MAANA NI RAHISI KWA KILA NAFSI KUWA NA ADUI AU RAFIKI. KUWA NA ADUI AU RAFIKI, KUNATOKANA KANA NA MATENDO NA MANENO YA KILA UPANDE (WEWE AU RAFIKI YAKO).
LICHA YA KUWA NAFSI NDIO YENYE MAAMUZI YA KUTENDA KAZI ZOTE ZA MWILI, LAKINI HUJIKUTA KATIKA KAZI NGUMU YA KULAZIMISHA MOYO WAKE, KUMPENDA ADUI WAKE. IKIWA NAFSI ITAJILAZIMISHA KUONGEA NA ADUI WAKE, KUNA DALILI AMBAZO MOYO WAKE(NAFSI) UTAZITOA ZA KUTORIDHIKA NA MATENDO NA MANENO VYA NAFSI ADUI.
• WEMA + UJINGA

WEMA TUMEONA KWAMBA NI MTINDO WENYE HEKIMA KATIKA MATENDO YAKE. NA MSINGI WAKE NI ELIMU, YENYE UKUTA BORA WA MATUMIZI YA MSAADA JUU YA MHITAJI.
UJINGA, TUMEONA KWAMBA MSINGI WAKE NI KIZA KINENE. HAKUNA MTU MWENYE KUPENDA AU KUPENDELEA KUISHI KATIKA KIZA KINENE, LA BALI KILA MTU ANAPENDA AISHI KWENYE MWANGA ILI AWEZE KUTENDA KAZI YAKE KWA UFANISI ZAIDI.
MTU MJINGA ANAPOKUTANA NA MTU MWEMA, HUPATA FARAJA YA MATENDO MAZURI NA MANENO YA BUSARA, LAKINI KWA UPANDE WA MTU MJINGA, HUWA KAMA KIPOFU KATIKA MTAZAMO WA MATENDO AU USIKIVU WA MANENO.

SIKUZOTE MTU MWEMA ANAJITAHIDI KULINDA HESHIMA YAKE, KATIKA MANENO(HUTUMIA MANENO YA BUSARA) NA MATENDO
( HUTUMIA MATENDO YENYE UNAFU KWA KILA UPANDE)

MTU MWEMA NJIA YAKE HUWA NI KUTAFUTA AMANI NA KUHAKIKISHA KWAMBA MLANGO WAKE WA UTULIVU UPO KATIKA NYANJA. BALI MTU MJINGA HAWEZI KUONA KWAMBA AMETENDEWA WEMA, BALI ATAONA KWAMBA MTU MWEMA ANAMNYIMA HAKI YAKE YA KUTENDA UJINGA.

MTU MJINGA HUWA NI MWEPESI WA KUPOTEZWA KWASABABU HAIJUI NJIA VIZURI, HATAKAMA ATAAMBIWA KWAMBA NJIA HIYO NDIO SAHIHI, ATAJIKUTA KATIKA MASHAKA, KWA SABABU HANA (MTU MJINGA) UFAHAMU WA ELIMU YA KUTOSHA JUU YA UMUHIMU, FAIDA, HASARA VYA JAMBO
(NJIA, UENDESHAJI WA GARI, UJENZI, MAPENZI, HURUMA, MSAADA….N.K) HUSIKA.

KUMBUKA YA KWAMBA SIKU ZOTE MWIZI HAAMINI KWAMBA KUNAMTU MWENYE UWEZO WA KUMLINDIA MALI YAKE BILA KUMUIBIA,SIKU ZOTE MWIZI HUAMINI KWAMBA KILA MTU NI MWIZI.




AU MZINZI HAAMINI KWAMBA KUNA WATU WEMA WASIOKUWA NA TABIA YA UZINZI,

AU MTU MWENYE UKOSEFU WA IMANI JUU YA KUWEPO MUNGU, HUWEZI KUMSAIDIA KATIKA JINA LA MWENYEZI MUNGU NA AKAKUBALI MSAADA WAKO.

YOTE HAYO, YANATOKANA NA UPUNGUFU WA ELIMU JUU YA KUJUWA FAIDA YA UMUHIMU, FAIDA NA HASARA VYA JAMBO ULIFANYALO.

MTU MINGA HUWA NI MWEPESI WA KUKUBALI KILA NENO NA KILA TENDO LIPITALO MBELE YAKE, BILA KUFANYA UCHAMBUZI WA KINA, KATIKA MSINGI WA MCHAKATO WA MANENO NA MATENDO HUSIKA. JAMBO HILO HUWA NILENYE KUANGAMIZA NAFSI YA MTU MJINGA NA KUSABABISHA MAUMIVU MAKALI NDANI YA MOYO WA YULE RAFIKI MWEMA.

IKIWA JAMBO HILO, LITAJITOKEZA KATIKA MSINGI WA KUSHAURIANA, NAKILA UPANDE UKLABAKI NA MSIMAMO WAKE, KATIKA UKUTA WA MANENO NA MATENDO, KITAKACHOFUATA NI KUTENGANA KWA WEMA NA UJINGA.

KUTENGANA KWA WEMA NA UJINGA, NI KAMA MTENGANO WA KIZA NA MWANGA. IKIWA MWANGA UNAHITAJIKA KATIKA MAENDELEO YA JAMII, KITAKACHOTOKEA NI KUATHIRIKA KIDOGO KWA ULE MWANGA HUSIKA, NA BAADAE MWANGA UTARUDI KWENYE KUNDI LA WATU WEMA, NA UTAPATA MAFANIKIYO MAZURI KUTOKA KATIKA KUNDI HUSIKA( KUNDI LA WATU WENYE KUHURUMIANA KATIKA MANENO NA MATENDO).

KWA UPANDE WA UJINGA, UTASHINDWA KUJITAMBUWA NA KUTAMBUWA UMUHIMU, FAIDA NA HASARA VYA KUMPOTEZA RAFIKI MKARIMU, AMBAYE NI YULE MTU MWEMA. MATOKEO YAKE UJINGA WAKE UTAOTA MIZIZI NA BAADAE ATAJIKUTA AKITUMIWA NA MAADUI WA YULE MTU MWEMA, KUMSHAMBULIA, KUMJERUHI…..KATIKA NJIA YENYE MISINGI YA MANENO NA VITENDO.





ITAKAPOFIKIA HATUWA HIYO,NDIO UTAONA KWAMBA MTU MWEMA, HAWEZI KUISHI NA MTU MJINGA KUTOKANA NA KIZA KINENE KILICHO TANDA NDANI YA MOYO WAKE(MTU MJINGA).

UKOSEFU WA BUSARA, UTAUFANYA MOYO WA YULE MTU MJINGA KUWA SILAHA YENYE MASHAMBULIZI DHIDI YA MTU MWEMA, BILA KUJALI FAIDA YAKE KATIKA JAMII. CHUKI ITACHUKUWA NAFASI KUBWA KWA UPANDE WA MTU MJINGA, NA KWA UPANDE WA MTU MWEMA,ATAJITAHIDI KUTUMIA UFAHAMU (ELIMU) WAKE ILI AWEZE KUEPUKA CHUKI YA MJINGA DHIDI YAKE.

IKIWA KIZA NA MWANGA, MATOKEO YAKE MSHINDI NI MWANGA, NDIO MAANA TUNASEMA WEMA NA UJINGA NI KAMA MWISHO WAKE NI CHUKI, LA KINI MLANGO WA MWISHO WAKE NI NINGELIJUWA.

KINGA YA KUZUIA KUENEZA UKIMWI

Utafiti uliofanywa pamoja na majaribio katika kinga mpya umedhihirisha kuwa kinga hii mpya imefanikiwa kukinga tumbiri asiambukizwe virusi vinavyosababisha ukimwi na kutokana na hilo kutowa ishara kwamba kuna uwezekano mpya wa kukabili kinga ya maradhi ya ukimwi.
majaribio ya kinga ya ukimwi
mtaalamu ajaribu kinga ya ukimwi

Watafiti wa huko Marekani wanasema kuwa walifanya majaribio hayo kwa kuwapa kinga tumbiri 13 kati ya 24 waliotumiwa.
Baada ya mwaka mzima baada ya majaribio hayo iligundulika kuwa kati ya Tumbiri wote hao 12 kati yao walikuwa bado wana kinga dhidi ya virusi vya ukimwi mwilini.
Matokeo hayo yaliyochapishwa katika jarida la sayansi, Nature, huenda yakawa mchango muhimu katika utengenezaji wa kinga maalum dhidi ya maradhi hatari ya ukimwi na virusi vinavyosababisha ugonjwa huo.
Wataalamu hao waliwadunga tumbiri 24 wasiokuwa na maradhi yoyote kinga iliyokuwa na mfano wa virusi uliotengenezwa katika maabara, rhesus cytomegalovirus (CMV).
Kinga hii ilitengenezwa kwa ajili ya kuunda sumu ya kushambulia ugonjwa wa ukimwi unaowakumba tumbiri (SIV) sawa na HIV kwa Binadamu.
Baada ya kipindi cha mwaka mzima ilibainika kuwa kinga hiyo ilikuwa na uwezo kamili dhidi ya ukimwi wa Tumbiri kati ya tumbiri 13 tu, ikiwa nusu ya idadi hiyo iligundulika kuwa na kinga baada ya kipindi cha mwaka mzima.
Kinga hiyo ilitumiwa kwa kushinikiza uzalishaji wa aina ya seli fulani ya damu, seli zijulikanazo kitaalamu kama "effector memory T-cells", ambazo hubaki kuwa imara mwilini kwa kipindi kirefu hata baada ya virusi kuteketezwa na kutowa ulinzi wa mwili kwa kipindi kirefu.
Kiongozi wa mradi huo Profesa Louis J Picker, wa taasisi ya tiba ya kinasaba huko Oregon, anazilinganisha seli hizi na askari imara wa kulinda doria.

"ni mfano wa askari wanaorejea kambini na kutelekeza silaha zao, kwa imani kuwa wenzao wanaendeleza kazi bila wasiwasi," Profesa Louis Picker aliambia BBC.
Aliongezea kusema kuwa kuna ushahidi kwamba kinga hiyo iliteketeza dalili zote za ukimwi (SIV) katika tumbiri wote, sababu aliyoielezea kama inayowezekana kwa ukimwi wa binadamu.

Mashaka

Wataalamu walio nje na wanaoendelea na uchunguzi walifurahia matokeo haya, lakini wakaonya kuwa sharti usalama uzingatiwe kabla ya kufanya majaribio kama haya kwa binadamu.

Hata hivyo Profesa McMichael wa Chuo Kikuu cha Taifa nchini Australia alisema kuwa ni mfano huo wa SIV uliomo katika nyani na tumbiri uliosababisha HIV, kwa hiyo majaribio haya kwa nyani na tumbiri yanaonyesha dalili nzuri. Tatizo ni la usalama wa afya pamoja na utaratibu wa jinsi ya kuwapa chanjo ya aina hii binadamu, ingawa wengi wetu tuna virusi hivyo mwilini.
"CMV alisema mtaalamu huyo haiaminiki kwa asili mia moja, kwa sababu huzua magonjwa mbalimbali. Kabla ya kufanya majaribio kwa binadamu lazima utafute jinsi ya kuwatunza endapo yatatokea matatizo.

Wednesday, May 11, 2011

RAIS MUSEVENI KUAPISHWA LEO


Rais wa Uganda, Yoweri Museveni,anatarajiwa kuapishwa kwa muhula mwengine hii leo siku ya Alhamisi.Anaapishwa huku kukiwa na wingu la shutma kwa utawala wake kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya upinzani.

Katika siku za hivi karibuni serikali imelaumiwa kwa namna walivyokabiliana na maandamano ya upinzani na kusababishwa kulazwa hospitali kwa mwanasiasa wa upinzani, Dk Kizza Besigye pia kumezua shutma kali.

Wakati atakapoapishwa kwa muhula mwengine,Yoweri Museveni atakuwa amejiongezea muda wa kukaa madarakani kwa takriban miaka thelathini.

Alipoingia madarakani mwaka 1986 alisema tatizo la viongozi wa Afrika ni kukaa kwenye utawala kwa muda mrefu sana.

Kwa miaka mingi amefanya juhudi kuijenga upya nchi ya Uganda baada ya nchi hio kuwa kwenye vita na utawala mbaya.

Bado anaungwa mkono na wengi lakini wadadisi wanaona kuendelea kutegemea jeshi kunaweka nchi hio katika mazingira magumu.
Kizza Besigye akikabiliana na polisi

Kizza Besigye akikabiliana na polisi

Upinzani umekabiliwa vibaya katika wiki za hivi karibuni. Kiongozi wa upinzani, Dokta Kizza Besigye,bado yuko nchini Kenya baada ya kupata matibabu kufwatia kushambulia kwake na polisi.

Mapema siku ya Jumatano,Besigye alisema kuwa alizuiwa kupanda ndege kutoka Nairobi kwenda Uganda, baada ya kupatiwa matibabu nchini Kenya.

Serikali ya Uganda imekanusha kumzuia kusafiri.

Haijulikani kama atajaribu kusafiri hii leo kwenda nyumbani wakati Rais Museveni anaapishwa - hatua ambayo italeta aibu kwa serikali.

Baadhi ya viongozi walioalikwa kwa sherehe za kuapishwa kwa Rais Museveni waliwasili Kampala siku ya Jumatano huku wengine wakitarajiwa hii leo siku ya Alhamisi.

USALAMA
















Msamaria akiwavusha barabara wanafunzi wa chekechekea na shule ya msingi, eneo la Tandika Vetenari mjini Dar es Salaam. Eneo hili linahitaji kuwekewa alama ya kivuko ili kuepusha ajali zisizo za lazima kwa watoto hao.

Wageni wana haki ya kuamini Kilimanjaro haipo Tanzania



DHANA ya kwamba Tanzania tumekuwa hatufaidi maliasili zetu kama vile utalii, madini , pamoja na mlima Kilimanjaro, na badala yake fursa hii inatumiwa na nchi za wenzetu, dhana hii inazidi kupata mashiko kutokana na kile nitachokiita kushindwa kujitambua.

Nasema hivyo nikimaanisha kwamba bado watalii wengi wanazidi kuaminishwa kwamba, nirahisi kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia Kenya kuliko Tanzania.

Lakini bado serikali kwa kupitia mamlaka za mawasiliano na utalii hawajaona umuhimu wa kudhibiti habari au taarifa potofu zinazoingia mara tu unapoingia Wilaya jirani na Mlima Kilimanjaro.

Mfano mzuri ukiingia Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro utakaribishwa na ujumbe mfupi (sms) toka Kenya katika baadhi ya mitandao ukiambiwa "umeingia Kenya" au "karibu Kenya” na kupata maelekezo ya huduma kwa nchi hiyo.

Zaidi ya hapo utalakiwa na vyombo vya habari vyenye matangazo makini na yakudhihirisha utaifa wao kutoka Kenya, Vyombo hivyo ni kama vile KBC idhaa ya taifa, Mwanedu FM, Citized radio, Milele FM na nyinginezo lukuki.

Wakati huo kwa Tanzania ni redio mbili tu zinazosikika vizuri, ambazo ni Killi FM na Sauti ya Injili ambazo zote ni za palepale mkoani Kilimanjaro.Hivyo basi kwanini watalii wasione mlima upo Kenya, au ni vema kupitia Kenya kuliko Tanzania?.

Wakati umefika Serikali kuangalia maeneo yenye faida kubwa inayopotea pasipo sababu na isiwe Kilimanjaro tu, ila maeneo yote yenye thamani kubwa katika uchumi wa Taifa.

CHADEMA, CCM SASA NI KULIPUANA

Gasper Andrew, Singida na Boniface Meena, Nkasi
VITA ya maneno baina ya vyama vikubwa vya siasa nchini CCM na Chadema, imezidi kushika kasi kwa vyama hivyo kurushiana tuhuma katika mikutano ya hadhara inayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.CCM kinawaita Chadema wanafiki na Chadema kinaendelea kudai kuwa chama hicho tawala ndicho kinachoisababishia nchi umasikini.

Jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye alidai kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa ni mnafiki kwa kula matapishi yake anapodai kuwa chama tawala kinafuja mali ya umma huku naye (Dk Slaa) akiwa katika mwelekeo huohuo.

Alidai kuwa Dk Slaa ameingia mikataba ya kukishinikiza chama chake kimlipe Sh7.5 milioni kila mwezi wakati alipokuwa mbunge alikuwa akiilalamikia serikali kwamba inawabebesha wananchi mzigo mkubwa kwa kuwalipa wabunge kila mmoja Sh milioni sita. Nape alisema hayo jana alipokuwa akizungumza kwenye mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katikia Kituo Kikuu cha mabasi cha zamani mjini Singida.

Alisema anazo nyaraka halali za chama hicho zinazoonyesha kwamba baada ya Dk Slaa kuukosa urais, sasa amekigeukia chama chake na kuanza kukishinikiza kimlipe mshahara mkubwa kuliko aliokuwa akiupata alipokuwa mbunge.Nape alisema madai kwamba Dk Slaa haombi alipwe si ya kweli akidai kwamba ndiye anayeshiniza kulipwa kiasi hicho kwa vile ameachishwa ubunge na ameukosa urais.

"Anashangaza sana bungeni alikuwa akipanua mdomo hadi mwisho kupotosha jamii kuwa wabunge pamoja na posho, mishahara na marupurupu mengine, wanalipwa shilingi milioni sita kiasi ambacho alidai kuwa kinawaumiza wananchi. Kwa hiyo ndiyo tuseme Sh7.5 milioni ni kiwango ambacho hakitawaumiza wanachama wa Chadema na walipa kodi wengine," alihoji Nape huku akishangiliwa na wananchi waliohudhuria.

 Katibu huyo alisema kwa kitendo chake hicho cha kushinikiza alipwe kila mwezi mamilioni hayo, anapaswa kuwaomba radhi Watanzania kwa kuwadanganya alipokuwa bungeni kuwa Sh milioni sita ni mshahara mkubwa mno.
 Aidha, alisema kuwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe naye aliwahi kutoa msaada wa Fuso (malori aina ya Mitsubishi Fuso) tatu ili zikisaidie chama hicho katika shughuli mbalimbali za ustawi wake lakini sasa anakidai Sh500 milioni za ununuzi.

Madai ya Nape kuhusu mshahara wa Dk Slaa yaliwahi kutolewa maelezo na Chadema ambacho kilisema kilifikia uamuzi wa kumlipa, Dk Slaa mshahara na maslahi yanayolingana na anayopata mbunge kwa sababu ndicho kilichomshawishi aache kugombea ubunge katika Jimbo la Karatu mkoani Arusha, ambako alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda na kumtaka agombee nafasi ya urais ambayo mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alishinda.

Kilisema uamuzi huo ulifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na vikao vikuu vya chama hicho, kama vile Kamati Kuu, kuidhinisha malipo hayo.Kuhusu malori Chaadema kilisema kiliamua kufanya mkakakti wa kununua magari matatu ambayo Mbowe aliyanunua na kuyatoa kwa muda ili yakisaidie kwenye kampeni.

Mbowe: CCM wanajipa mamlaka ya uungu mtu
Wakati Nape akisema hayo Mbowe amesema viongozi wa Serikali ya CCM wamelewa madaraka na kujivika mamlaka ya uungu watu na kusahau kuwatumikia Watanzania: "viongozi wa nchi hii, wanajipa mamlaka ya umungu-mtu na wananchi wanawaogopa."
Mbowe, ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alisema hayo jana alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa mji mdogo wa Namanyere, Wilaya ya Nkasi, Rukwa, ikiwa ni sehemu ya operesheni ya Chadema ya kuishinikiza serikali kusikiliza kilio cha wananchi.

Alitoa mfano akisema, iwapo wananchi wa Wilaya ya Nkasi watajengewa barabara, wajue kuwa hiyo ni haki yao na pia wana haki ya kuiuliza serikali sababu za kuchelewa kujengewa kwa miaka 50 ya uhuru.
Alisema katika mkoa kama wa Kilimanjaro, wamekuwa wakijengewa barabara za lami kwa kadri inavyohitajika, tofauti na Mikoa kama ya Rukwa, Iringa, Mbeya na Ruvuma ambayo imeachwa nyuma kimaendeleo, licha ya kuzalisha chakula kinachohifadhiwa katika Hifadhi ya Chakula ya Taifa.

Kutokana na hali hiyo, alisema iwapo wananchi wa Mkoa wa Rukwa hawatapiga kelele kudai maendeleo, kamwe hawezi kushuka Malaika Gabriel kuwapigia kelele."Kwa hiyo ndugu zangu, si kila kitu ni cha kupongeza, muwatume wabunge wenu wakapige kelele," alisema Mbowe.Alisema tangu Chadema ianze kupiga kelele Rukwa, imefanikiwa kutoa Mbunge mmoja tu, Said Arfi na barabara zikianza kutengenezwa.

Mbowe alisema serikali imeshindwa kusimamia reli ya kati kiasi ambacho wananchi wanaotaka kusafiri kulazimika kutumia gharama kubwa kupata usafiri wa ndege.Alisema kuwa baadhi ya wabunge kutumia muda mwingi bungeni kuishukuru serikali katika mambo ambayo ni wajibu wake kuwatekelezea wananchi.Alisema wabunge hao wamekuwa wakifanya hivyo, huku wakijua wazi kuwa ni kinyume na jukumu la mbunge, ambalo ni kuisimamia serikali kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi.
"Kitendo cha kuishukuru serikali, ndicho kinatuchelewesha kupata maendeleo. Wananchi wanaiomba serikali, wabunge wanaishukuru..." alisema.Alisema vitendo hivyo vimechangia kwa kiasi kikubwa kuwafanya viongozi wa serikali nchini kujiona kuwa ni miungu kwa sababu wanatukuzwa.

Waliopewa siku 90 CCM wataaibika karibuni
Katika hatua nyingine, Nape alisema kuwa viongozi walioombwa na chama wajipime wenyewe na kuchukua uamuzi wa kuachia nyadhifa zao mapema kutokana na kutuhumiwa na wananchi juu ya tabia zao za kifisadi, kwamba sasa siku zao za kuja kuaibishwa, zinahesabika.

"Watu sasa wameanza kusema kuwa Nape hana nguvu tena za kupambana na ufisadi nchini, nawaambia kuwa si kweli. Sijalala wala sijaishiwa nguvu za kutokomeza ufisadi. Hawa wanaotuhumiwa kwa ufisadi wanakipa chama machungu na kuanza kukikosesha imani kwa wananchi, wanapaswa kujiondoa wenyewe na wasisubiri kuja kuapishwa kwa kufukuzwa kwa nguvu," alisema.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chilingati aliwataka viongozi na wanachama wa chama hicho ngazi ya wilaya na mikoa kusaidia kukirudisha kwenye misingi yake ya awali ili wananchi waendelee kukiamini.
Chiligati ambaye pia ni Mbunge wa Manyoni Mashariki, alitoa wito huo juzi alipozungumza na wananchi wa Kata ya Ikungi, Singida.
Alisema vikao vya Halmashauri Kuu vilivyofanyika hivi karibuni mjini Dodoma, vilibaini kuwa CCM imefika mahali pabaya kwa kuanza kuacha misingi yake na kusababisha baadhi ya wanachama wake na wananchi kwa ujumla, kuanza kukosa imani nacho.

Tuesday, May 10, 2011

AJABU NDANI YA KANISA, PADRE AMNASA VIBAO BI KIZEE

Ni habari ya kusikitisha na kustaajabisha ilyotokea ndani ya Kanisa katika Parokia ya Vugu mkoani Kigoma, mwishoni mwa wiki iliyowaacha waumini na butwaa, baada ya Padri kumpiga makofi Bibi Kizee katikati ya ibada ya misa ya pili, akimtuhumu kuondoka na Sakramenti aliyoipokea madhabahuni.

Padri aliyefahamika kwa jina moja la Sabas, alifikia hatua hiyo wakati wa ibada ya Sakramenti, ambapo bibi huyo aliungana na waumini wengine kwenda kushiriki, lakini alipopewa kipande cha mkate, aliondoka nacho na kwenda kukila akiwa ameketi. Inaripotiwa kuwa kitendo hicho kilisababisha Padre Sabasi kusimamisha huduma hiyo ghafla, na kumfuata bibi huyo na kuanza kumpiga makofi.

Waumini waliohudhuria ibada hiyo wameeleza kuwa ni mara ya kwanza kitendo hicho kutokea mkoani humo.

"Huyu ni mtu mzima, hivyo hakuweza kuvumilia kusimama na kukila kipande cha mkate na kuamua kukaa chini, Padri alitakiwa kumuonya kama alikuwa amekosea na siyo kumpiga, " alisema muumini mmoja mara baada ya kumalizika kwa misa hiyo.

Padri Sabas alipohojiwa kuhusu kitendo hicho alidai kuwa alifikia uamuzi huo kutokana na muunini huyo kwenda kinyume na utaratibu wa kanisa hilo na kuongeza kuwa,  alimwona muumini huyo akikiweka kipande hicho kwenye ziwa (titi) kwa imani za kishirikina.

Waandishi wa gazeti la DarLeo (credit) hawakuweza kuzungumza na muunini huyo ili kujua undani wa tuhuma hizo kwa vile Bi Kizee huyo aliondoka mara baada ya ibada hiyo kumalizika.

Monday, May 2, 2011

Tafakuri Yangu ya Leo; Popote Ulimwenguni Ambapo Masikini Waliowengi Hawakusikilizwa Basi Imesikika Milio Ya Risasi Na Mabomu!

   “A Hungry Man Is Always An Angry Man”….Bob Marley(1945-1983)

  Haya ni maneno ya kifalsafa yaliyowahi kutamkwa na gwiji wa muziki wa Reaggae hayati Robert Nestar Marley maarufu kama Bob Marley nayaita maneno ya kifalsafa kwasababu yalilenga kwenye Ulimwengu halisi aishio mwanadamu , kwa maana ya Kiswahili kauli hii yaweza kusemwa kuwa “mtu mwenye njaa mara zote huwa na hasira”
   Hili halina ubishi hata kidogo ingawaje ukweli ni kuwa mara nyingi kauli za kifalsafa huwa hazina maana moja hivyo najua wapo baadhi ya watu watanipinga kwenye hili nakuibua tafsiri zao nasema hewala na natanguliza shukrani zangu kwao kwa maana binadamu tumeumbwa tofauti hivyo wanatimiza haki yao ya msingi ya kufikiri lakini kwangu mimi naungana na maana iliyotolewa na legend huyu wa reaggae.
    Jana asubuhi nimemsikia Bw Gracian Mukoba ambaye ni mwenyekiti wa chama cha walimu Tanzania akizungumza kupitia kituo kimoja cha redio jijini Dar es salaam Bw Mukoba alinukuliwa akisema “hata hela ya chakula bado haijatosha kwa walimu, mwalimu anatoka nyumbani hajanywa chai kisha mtoto wake karudishwa nyumbani anadaiwa ada na duka la jirani mwalimu anadaiwa kwasababu alikopa ili mwisho wa mwezi alipe hata hivyo mshahara wake bado mdogo sana kukidhi haya yote, halafu mwalimu huyu anenda darasani kufundisha, hivi tutegemee ni nini kutoka kwa mwalimu huyu?”
    Naam! Hizi ni zama za kuambiana ukweli , hivi mara ngapi walimu wamelilia nyongeza za mishahara? Nani anawasikiliza? Kwanini hawasikilizwi? Viongozi wahusika na serikali naomba wajibu maswali yafuatayo ambayo yanawahusu watanzania masikini walio wengi kwenye nchi hii;
1.      Hivi serikali inafaidika nini wananchi wake wanapoishi kwenye lindi la ufukara na umasikini wa kutisha?
2.      Hivi watoto wetu kwenye shule za kata wataendelea kufeli mitihani mpaka lini?
3.      Hivi serikali inaona sawa jinsi wazungu wanavyoendelea kupora maliasili zetu kama madini huku mtanzania anazidi kudidimia kwenye umasikini wa kutisha?
4.      Hivi viongozi wetu wanafaidika nini na kuharibika kwa maadili miongoni mwa vijana? Wengi wakiwa wasikilizaji wa bongo flava hawapendi kujifunza mambo wala utamaduni wao, serikali kwanini haina program maalumu ya malezi ya vijana?
5.      Hivi serikali ya rais Kikwete kwanini bado haijatimiza yale yote iliyoahidi walau robo yake tu? hivi Mheshimiwa rais Kikwete anajisikia furaha gani wananchi wake wanapoulizia mambo aliyowaahidi?
6.      Hivi serikali inafaidika nini matabaka yanapoongezeka kila uchao? Tabaka la walionacho na wasio nacho yana faida gani kwa serikali? Kwanini masikini ndiyo wengi?
7.      Viongozi wa serikali wanafaidika nini na mgao wa umeme? Kwanini mpaka leo tatizo la umeme linaendelea? Au Mheshimiwa rais Kikwete alivyoahidi kujenga barabara za juu(fly-overs) halafu mpaka leo msongamano wa magari unaendelea jijini Dar rais alimaanisha nini kuahidi jambo hili?
8.      Serikali inafaidika nini na malumbano yanayotengenezwa kwa makusudi? Mfano hii rasimu mbovu ya mapendekezo ya katiba mpya ambayo watu hawaitaki kwanini serikali inang’ang’ania? Kwa faida ya nani? Au kwanini swala la muungano kujadiliwa linazuiwa kwa faida ya nani? Na litazuiwa mpaka lini? wananchi wanautaka muungano ila wanataka kuujadili serikali inapopiga chenga ina maanisha nini?
9.      Hivi uwekezaji usio nufaisha wananchi utaendelea mpaka lini? mpaka lini mapigano ya kugombea ardhi kama ya Mbarali yataendelea? Na haya yanamfaidisha nani?
10.  Lini serikali itajifunza kusikiliza wananchi wake? Lini serikali itawalinda wanahabari wa nchi hii ambao wanayumbishwa kwa rushwa na ubabe kila uchao kiasi kwamba wanashindwa kusema ukweli, je wao wasiposema kwa niaba ya wananchi nani atasema? Au lini basi viongozi wa dini wa nchi hii hawatakaripiwa bila aibu na wanasiasa uchwara pale viongozi hao wa dini wanapokosoa ubabaishaji wa serikali?

Naam! Nauliza hivi kwasababu naona viongozi wamelala usingizi wa pono, wao hawashtuki kwanini watanzania masikini wanamlilia Nyerere kila uchao? Hawajui kuwa hii si dalili njema hata kidogo, kwa maana nyingine wananchi wamekata tamaa kwasababu hawasikilizwi ndiyo maana kilasiku wanamkumbuka Nyerere.
   Lakini katika mkanganyiko huu kuna ukweli wa kihistoria kuwa popote ulimwenguni masikini walio wengi wasiposikilizwa basi hapo milio ya mabomu na risasi husikika, ndiyo hata Tunisia wanyonge hawakusikilizwa sihitaji kusema nini kilitokea? Pia Misri wanyonge walipuuzwa na sisi wote ni mashahidi ya kilichotokea kule, hofu yangu mimi si huu ukweli wa kihistoria HAPANA hofu yangu kubwa ni tabia ya historia kujirudia, hii ndiyo hofu yangu kubwa na hii ni kanuni haiwezi kupingwa na kwa bahati mbaya si kanuni yangu mimi Nova Kambota bali ya kihistoria!  Naam! Iwe usiku au mchana siku ya wafanyakazi au wakulima serikali ijihoji itaendelea kupuuza wananchi mpaka lini? lakini isiishie hapo bali pia ijiulize kwa kiasi gani imejipanga kukabiliana na ukweli huu wa kihistoria?

Kitendawili si deni ukishindwa nipe mji,
Kwa wanataaluma kutofautiana kimawazo si kosa bali ni dalili ya jamii iliyo hai,
Nova Kambota Mwanaharakati,
Nipigie; 0717-709618(Tanzania) au +255717-709618(Nje ya Tanzania)
Kwa maoni na ushauri niandikie;
Kwa habari zaidi za kitafiti na uchambuzi tembelea Blog yangu;
Tanzania, East Africa,
Jumatatu, Mei 2,  2011.

Sunday, May 1, 2011

UWANJA WA UHURU WABOMOLEWA

Uwanja wa Uhuru (Shamba la bibi ) eneo la green stand kam inavyoonekana imebomolewa kupisha ujenzi

Hali halisi ilivyo kwa sasa


Uwanja wa Taifa ukiwa unaeendelea kubomolewa kuongeza idadi ya majukwaa na kukiweka katika hali nzuri zaidi na kuwa kiwanja cha kisasa zaidi