Pages

Monday, May 23, 2011

RAHA NA KARAHA YA MAPENZI

Bi harusi akijaribu kuokolewa

Ni ukweli usiopingika kuwa mapenzi ni matamu sana pale panapokuwa na maelewano na maridhiano baina ya wapendanao lakini mapenzi hayo hayo huwa sawa na sumu kali inayoua pale mambo yanapokuwa kinyume, mfano halisi ni mwanamke huyu wa nchini China ambaye aliokolewa sekunde ya mwisho kabla ya kujiua kwa kujirusha toka ghorofa ya saba baada ya bwana harusi wake kumkimbia na kwenda kumuoa mwanamke mwingine siku moja kabla ya harusi yao. Maandalizi yote ya harusi yakiwa yamekamilika, siku moja kabla ya harusi kufungwa bwana harusi alimtosa bi harusi na kwenda kumuoa mwanamke mwingine siku hiyo hiyo.

Kwa uchungu wa kuyakosa mapenzi ya aliyekuwa bwana harusi wake, bi harusi akiwa amevalia shela la harusi alipanda kwenye dirisha la ghorofa ya saba akiwa na nia ya kujiua kwa kujirusha hadi chini.

Hapa tunamzungumzia mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Li mwenye umri wa miaka 22 ambaye alisababisha mtafaruku mkubwa alipojaribu kujirusha toka ghorofa ya saba akiwa amevalia shela lake la harusi.

Uamuzi huo wa Li ulitokana na machungu ya kukimbiwa na mumewe mtarajiwa ambaye siku moja kabla ya harusi alivunja uhusiano wao na kwenda kumuoa mwanamke mwingine siku hiyo hiyo.

Li kabla hajajirusha chini mwanaume mmoja aliyewahi kufika ghorofa ya saba alimng'angania Li na kumvuta ndani huku watu wengine wakimsaidia kumvuta ndani mrembo huyo aliyeonja chachu ya mapenzi ili kunusuru maisha yake.

Tukio hilo lililochukua dakika kadhaa liliwavuta watu wengi ambao walijazana chini wakisubiria kuona kitakachojiri.

Baada ya dakika chache za patashika hilo, polisi kwa kushirikiana na raia walifanikiwa kumvuta ndani ya jengo hilo na hivyo kunusuru maisha ya mrembo huyo.

No comments:

Post a Comment