Pages

Wednesday, May 18, 2011

Mgao wa umeme

*Nchi gizani tena
*Mikoa 12 kukosa umeme


WANANCHI wa mikoa 12 wataendelea kupata machungu ya mgao wa umeme, baada ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kutangaza tena ratiba ya mgao huo.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo asubuhi kwenye vyombo habari
kutoka kitengo cha mawasiliano Makao Makuu TANESCO, na kusainiwa na Ofisa Uhusiano, Badra Masoud.

Imeeleza kuwa, mgawo huo utahusisha Mkoa wa Dodoma, Morogoro, Mara, Tabora, Pwani, Arusha, Kilimanjaro, Shinyanga, Iringa, Mbeya, Manyara na Dar es Salaam katika wilaya zote za Temeke, Ilala na Kinondoni.

Taarifa hiyo imesema kuwa, umeme huo utaanza kukatika saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni, ambapo katika maeneo mengine, utakatika kuanzia saa 12 jioni na kurejea saa 5, usiku.

Hata hivyo, taarifa hiyo imesema kuwa, maeneo mengine mgawo utakuwa ukianzia saa 10 jioni hadi saa 5 usiku, wakati maeneo mengine yatakuwa giza kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni.
 

No comments:

Post a Comment