Pages

Friday, May 20, 2011

MAPENZI SHULENI

Vurugu kubwa ziliibuka jana baada ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mbagala kuvamia shule ya Nzasa na kuanza kuwashambulia baadhi ya wanafunzi kwa fimbo na mawe.

Tukio hilo limetokea jana saa 7 mchana ambapo chanzo kikubwa inadaiwa  kuwa, ni mahusiano ya kimapenzi ambapo kuna mwanafunzi wa kike mmoja alikuwa akiwachanganya wanafunzi hao wa Mbagala na Nzasa.

Akizungumza na gazeti Dar Leo kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Missime, amesema kuwa, hadi sasa jeshi lake linawashikilia wanafunzi wanne kuhusiana na vurugu hizo.  Akasema wanafunzi wa Mbagala mmoja wao alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na msichana ambaye pia alibaini kuwa ana mahusiano na mvulana mwingine anayesoma Nzasa ambapo aliamua kwenda na kundi lake kumfanyia vurugu.

Kutokana na vurugu hizo, wanafunzi sita walipata mshtuko na walikimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Kamanda Missime amesema waliokamatwa katika vurugu hizo ni Shana Reagan wa kidato cha nne 'D', Twahir Sultan kidato cha 3 katika sekondari ya Nzasa, Said Muhibu mkazi wa Zakhem alijiingiza kwenye vurugu hizo na Reuben Hosea, kidato cha 3 katika Sekondari ya Mbagala.

"Tumeamua kuwashikilia hawa watuhumiwa kwa kuwa wanaonekana kama ni wahuni na si wanafunzi kwani wamewezaje kujiingiza kugombea mwanamke wakati bado wapo shuleni? Hivyo tukijiridhisha tutawafikisha Mahakamani," amesema Kamanda Missime.

Mazungumzo baada ya habari...
Hawa yaelekea hawajawahi kusikia nyimbo zenye mafunzo kama huu wa Mbaraka Mwinshehe na kufuata mafunzo yake. Sijui wanasikiliza nyimbo zinazochochea kuwakiana tamaa ya mapenzi tu? Ndiyo shida yake.

No comments:

Post a Comment