Pages

Friday, May 13, 2011

KINGA YA KUZUIA KUENEZA UKIMWI

Utafiti uliofanywa pamoja na majaribio katika kinga mpya umedhihirisha kuwa kinga hii mpya imefanikiwa kukinga tumbiri asiambukizwe virusi vinavyosababisha ukimwi na kutokana na hilo kutowa ishara kwamba kuna uwezekano mpya wa kukabili kinga ya maradhi ya ukimwi.
majaribio ya kinga ya ukimwi
mtaalamu ajaribu kinga ya ukimwi

Watafiti wa huko Marekani wanasema kuwa walifanya majaribio hayo kwa kuwapa kinga tumbiri 13 kati ya 24 waliotumiwa.
Baada ya mwaka mzima baada ya majaribio hayo iligundulika kuwa kati ya Tumbiri wote hao 12 kati yao walikuwa bado wana kinga dhidi ya virusi vya ukimwi mwilini.
Matokeo hayo yaliyochapishwa katika jarida la sayansi, Nature, huenda yakawa mchango muhimu katika utengenezaji wa kinga maalum dhidi ya maradhi hatari ya ukimwi na virusi vinavyosababisha ugonjwa huo.
Wataalamu hao waliwadunga tumbiri 24 wasiokuwa na maradhi yoyote kinga iliyokuwa na mfano wa virusi uliotengenezwa katika maabara, rhesus cytomegalovirus (CMV).
Kinga hii ilitengenezwa kwa ajili ya kuunda sumu ya kushambulia ugonjwa wa ukimwi unaowakumba tumbiri (SIV) sawa na HIV kwa Binadamu.
Baada ya kipindi cha mwaka mzima ilibainika kuwa kinga hiyo ilikuwa na uwezo kamili dhidi ya ukimwi wa Tumbiri kati ya tumbiri 13 tu, ikiwa nusu ya idadi hiyo iligundulika kuwa na kinga baada ya kipindi cha mwaka mzima.
Kinga hiyo ilitumiwa kwa kushinikiza uzalishaji wa aina ya seli fulani ya damu, seli zijulikanazo kitaalamu kama "effector memory T-cells", ambazo hubaki kuwa imara mwilini kwa kipindi kirefu hata baada ya virusi kuteketezwa na kutowa ulinzi wa mwili kwa kipindi kirefu.
Kiongozi wa mradi huo Profesa Louis J Picker, wa taasisi ya tiba ya kinasaba huko Oregon, anazilinganisha seli hizi na askari imara wa kulinda doria.

"ni mfano wa askari wanaorejea kambini na kutelekeza silaha zao, kwa imani kuwa wenzao wanaendeleza kazi bila wasiwasi," Profesa Louis Picker aliambia BBC.
Aliongezea kusema kuwa kuna ushahidi kwamba kinga hiyo iliteketeza dalili zote za ukimwi (SIV) katika tumbiri wote, sababu aliyoielezea kama inayowezekana kwa ukimwi wa binadamu.

Mashaka

Wataalamu walio nje na wanaoendelea na uchunguzi walifurahia matokeo haya, lakini wakaonya kuwa sharti usalama uzingatiwe kabla ya kufanya majaribio kama haya kwa binadamu.

Hata hivyo Profesa McMichael wa Chuo Kikuu cha Taifa nchini Australia alisema kuwa ni mfano huo wa SIV uliomo katika nyani na tumbiri uliosababisha HIV, kwa hiyo majaribio haya kwa nyani na tumbiri yanaonyesha dalili nzuri. Tatizo ni la usalama wa afya pamoja na utaratibu wa jinsi ya kuwapa chanjo ya aina hii binadamu, ingawa wengi wetu tuna virusi hivyo mwilini.
"CMV alisema mtaalamu huyo haiaminiki kwa asili mia moja, kwa sababu huzua magonjwa mbalimbali. Kabla ya kufanya majaribio kwa binadamu lazima utafute jinsi ya kuwatunza endapo yatatokea matatizo.

No comments:

Post a Comment