Pages

Monday, December 16, 2013

Mjengwa: Kwa nini hotuba ya Rais Kikwete ya kumuaga Mandela kijijini Qunu ilikuwa bora?

Ndugu zangu,

NOTHING can come from NOTHING. Wamesema hili Wanafalsafa wa Uyunani ya Kale .

Nimemwona na kumsikiliza Rais wetu Jakaya Kikwete akizungumza kwenye siku muhimu ya kumuaga kwa mara ya mwisho Mzee wetu Nelson Mandela.

Muda wote wa hotuba yake, JK alibaki kwenye mstari kwa namna ile ile ya kuweka bayana kwa ulimwengu, kuwa ' msione
vinaelea'.

Hakika alichofanya JK leo ndicho haswa alipaswa kukifanya, na amekifanya kwa kutumia weledi wake kwenye diplomasia na kuchanganya uzoefu wake kwenye uongozi wa kisiasa na dola kwa ujumla.

Ni kuitumia fursa ile ambapo macho na masikio ya dunia yalielekezwa Quni, kwa yeye rais kuiambia dunia, na si kuisubiri CNN au vyombo vya habari vya Kimagharibi kuifanya kazi hiyo, juu ya mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa bara la Afrika ikiwamo mchango wa Tanzania kumfanya Mandela na viongozi wengine wa Kiafrika kuonekana kama walivyoonekana kwenye macho ya dunia.

Hakika, JK anastahili pongezi kwa kazi njema aliyoifanya leo ya kuiweka tena Tanzania katika ramani ya dunia, si tu kama nchi ile ya mbuga za wanyama na Mlima Kilimanjaro, bali ' Taifa Kubwa' lililochangia kushiriki mikakati ya ukombozi ikiwemo kutoa misaada ya silaha, mafunzo na hata makazi kwa wapigania ukombozi wa Afrika.

JK aliipitia historia ya mchango wa Tanzania ambayo wengi waliokuwa wakimsikiliza, ama waliisahau au hawakuijua kabisa.

Lakini, tujiulize pia kama Watanzania, katika aliyoyasema JK kule Quni, ni Watanzania wangapi wanayajua? Inahusu umuhimu wa kuipitia historia yetu ili, kama Watanzana, tuweze kumiliki ' K3'- Kujitambua, Kujiamini na kuthubutu. Imefika mahali tunaionea aibu hata historia yetu.

Na nyongeza katika yale aliyoyasema JK leo ni kumbukumbu ya kihistoria ambayo haitajwi pia, kuwa Baba wa Taifa , Mwalimu Nyerere, ndiye aliyempa hifadhi Tanzania, Rais wa Pili wa Afrika Kusini huru. Ni Thabo Mbeki. Baada ya kutoroka Afrika Kusini. Baadae Thabo Mbeki akaenda kusoma Uingereza.

Jambo hilo linathibitishwa katika kitabu alichoandika msomi mahiri wa Afrika Kusini, William Gumede. Anasema;

" In 1962, Thabo slipped out of the country to which he would not return for twenty -eight years, travelling through Botswana to Rhodesia, where he was arrested and held in a Bulawayo prison for several weeks. The white Rhodesian authorities intended to deport him back to South Africa and waiting for security police, but British Labour MP, Barbara Castle intervened after being lobbied by the ANC, and Mbeki was granted asylum in Tanzania by President Julius Nyerere." ( William Gumede, Thabo Mbeki and The Search For Soul of The ANC, pg 36)

Naam, ni wakati sasa wa viongozi wengine, bila kujali itikadi zao, wanapokuwa kwenye majukwaa ya kimataifa, kuzitafuta fursa za kuonyesha yale ambayo huko nyuma tumekuwa na uwezo nayo, na bado, kama nchi, tunaweza kuaminika katika kutoa mchango wa uzoefu wetu kwenye masuala mbali mbali ya Kimataifa.

Source: http://www.wavuti.com.

Tuesday, November 26, 2013

FFU WAUTEKA MJI WA BREMEN UJERUMAN

 Kamanda Ras Makunja katika gwaride Bremen

 Wapenzi na mashabiki wa Ngoma Afrika Band ndani ya Ubersee Museum Bremen
 FFU wakishambulia jukwaa
 Mo benda mpiga Rhythm gitaa
 Glory Mndeke Mwimbaji rapa wa Ngoma Afrika Band
 Mpiga bass msaidizi wa FFU kijana Gaiilo
 Hili ndilo jengo la Ubersee-Museum Bremen lililotingishwa na FFU
 Kamanda Ras Makunja akiwa katika gari maalum akiwasalim wakazi wa Bremen
fan wa ngoma africa band akisainiwa autograph katika CD na Kamanda Ras Makunja

FFU wa Ngoma Africa Band wameliteka tena jiji la Bremen !

Wamevuna umati wa washabiki wa kimataifa


Bremen,Ujerumani,

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU ughaibuni,usiku tarehe 23 Novemba 2013 walifanikiwa kwa mara nyingine tena
kuliteka jiji la Bremen,kule ujerumani. Kiongozi wa bendi hiyo kamanda Ras Makunja wa FFU alikiongoza jukwaani kikosi kazi chake katika jumba la Übersee-Museum akiwa na matumaini kuwa wanaenda kumbuiza washabiki high class wenye adhi ya kibwanyenye lakini mziki ulipoanza mdundo uliwachanganya washabiki na kuwadatisha akili ! kila mmoja alijimwaga uwanjani !
Ngoma Africa Band walijikuta wapo katika kibarua kama kawaida yao cha kushambulia kwa virungu vya muziki na kufanikiwa kuutapanua uwigo wake
kwa kuwanasa washabiki wengi wa kimataifa.
Bendi hiyo maarufu iliyojiimarisha na kujenga himaya ya kimataifa kwa kutumia
muziki wake,meshatajwa mara nyingi kuwa bendi bora ya kiafrika barani ulaya,
bendi ya Ngoma Africa inafanananishwa sawa na kikosi maalumu cha kuzuwia ghasia FFU, pia ina majina mengi ya utani na kiusanii kama vile viumbe wa ajabu  "Anunnaki Elien" n.k ambayo imepewa na washabiki au wapenzi wake,kiongozi wake pia ana majina kama vile kamanda Ras Makunja wa FFU,mtawala wa Anunnaki Empire.
Ngoma Africa band wanasikika at www.ngoma-africa.com

Tuesday, November 19, 2013

WAILES YAWA GEREJI BUBU

         Njinjo barabara zimekuwa sehemu ya kupakila mmizigo na matengenezo ya magari


                       Hali ya sasa maeneo ya temeke wailes mtaa, wa ngarambe, mkumba, ngeta na Njinjo ilivyo kwa sasa.

Sunday, November 3, 2013

HAKIKA YA MTOTO AKRAM SAID BUNGARA

                         Mr & mrs bungara wakiwa katika picha ya pamoja na mtoto wao Akram          
Said akimkabidhi Akram kwa bibi yake

Familia ya said bungara inapenda kutoa shukrani kwa wote waliohudhuria katika tafrija hiyo iliyofanyika nyumbani kwa babu yake mtaa wa mjimwema 'B' Temeke




                                       

Friday, November 1, 2013

UTANUZI WA BARABARA YA KILWA ROAD

    Utanuzi wa barabara ya kilwa road ukiendelea, huku baadhi ya majengo yakibomolewa kupisha
                                                                    utanuzi huo
                               


                                     Maeneo ambayo kwa sasa yashaanza kubomolewa ni barabara ya bandari, gerezani
                                   mpaka kamata