Pages

Sunday, April 29, 2012

NINI KINACHOFUATIA HAPA

MAUAJI YA USA RIVER

 Nimeshindwa kusema lolote kuhusu hii picha naomba radhi kwa wote ambao picha hii inaweza kuwakwaza naomba tusameheane mengi keshasema Mjengwa ntakuwa nayarudia tu

Ndugu zangu, 

Kuna kisa cha mtego wa panya uliosababisha madhara hata kwa wasio panya.
Panya kwenye nyumba aliubaini mtego wa panya uliowekwa uvunguni  mwa kitanda na mwenye nyumba.

Panya yule akamwendea jogoo  wa mwenye nyumba. Akamwambia; " Ewe jogoo, kuna mtego umewekwa  uvunguni mwa kitanda. Tusaidiane namna ya kuutegua kabla haujatudhuru wote".

Jogoo akajibu; " Ondoka zako, mie mtego wa panya unanihusu nini wakati sina kawaida ya kufika uvunguni mwa kitanda!"

Panya yule akaenda hadi kwa mbuzi wa mwenye nyumba. Akamwambia; " Ewe mbuzi mwema, unajua kuna mtego wa panya uvunguni mwa kitanda cha mwenye nyumba. Tusaidiane mawazo ya kuutegua kabla haujatudhuru sote".

Mbuzi akajibu; " Hivi tangu lini ukaniona nikiingia chumbani kwa mwenye nyumba? Mtego huo wa panya haunihusu mie mbuzi".

Panya akaenda hadi kwa ng'ombe wa mwenye nyumba. Akamwambia; " Ewe ng'ombe wa bwana, kuna mtego wa panya umewekwa uvunguni mwa kitanda. Tusaidiane mawazo namna ya kuutegua kabla haujatuletea madhara"

Ngombe akajibu akionyesha mshangao; 
" Sijapata kusikia jambo la ajabu kama hilo. Yaani, mie ng'ombe nidhurike na mtego wa panya ulio uvunguni mwa kitanda! Hilo halinihusu."

Basi, ikatokea siku moja, nyoka akaingia chumbani kwa mwenye nyumba. Katika kutambaa kwake uvunguni mwa kitanda,  mkia wa nyoka ukanasa mtegoni. Kishindo kilisikika. 

Mwenye nyumba alikwenda kwa furaha akiamini hatimaye panya aliyekuwa akimsumbua sasa amenaswa. Hapana, ni nyoka aliyenaswa mkia. Na ni mwenye hasira pia. Akamng'ata mguu mwenye nyumba. Sumu kali akamwachia. Mwenye nyumba akafa.

Jirani wakafika msibani. Siku ya kwanza watu walikuwa wachache. Wakahitaji kitoweo . Akakamatwa jogoo wa mwenye nyumba  achinjwe.

Siku ya pili watu wakaongezeka. Kilihitajika kitoweo pia. Akakamatwa mbuzi wa mwenye nyumba ili achinjwe.

Na siku ya maziko watu wakawa wengi  zaidi. Akakamatwa  ng'ombe wa mwenye nyumba ili achinjwe.

Ni jogoo, mbuzi na ng'ombe wa mwenye nyumba walioamini kuwa madhara ya mtego ule wa panya  yasingewahusu wao. Walikosea. Panya alikuwa sahihi, na wala mtego haukumdhuru panya!


Naam, Watanzania tunazidi kupokea habari mbaya za matukio ya mauaji ya kutisha. Vuguvugu la mapambano ya kisiasa linasemwa kuwa ni moja ya sababu za matukio ya mauaji na hata watu kujeruhiwa kwa mapanga. 

Na vuguvugu la mapambano ya kisiasa halipawi kuandamama na vitendo vya mauaji au kujeruhiana kwa mapanga, bali, liwe ni vuguvugu la mapambano ya hoja.

Kule Nyamagana tumeshuhudia wabunge wamepigwa mapanga. Na jana  kiongozi wa Chadema pale Usa River amechinjwa kama  kuku.

Inasikitisha sana kuona vitendo hivi vya kinyama vinazidi kuongezeka.  Inasikitisha pia kuwa polisi wanashindwa kwa haraka kuwatia nguvuni wahusika wa mauaji na kuwafikisha mahakamani.  Labda idara za upelelezi wa kipolisi zinahitaji kuimarishwa zaidi.

Na huu ni wakati, kwa Watanzania, bila kujali tofauti zetu za  kiitikadi, kidini au rangi, tukemee kwa sauti moja vitendo hivi viovu.  Kamwe tusikubali ikawa ni vitu vya kawaida.

Ni wakati  sasa kwa wananchi wakiongozwa na viongozi waandamizi wa vyama vya siasa. Viongozi wa kidini na  wanaharakati wa haki za kibinadamu, kusimama kwa pamoja, na kwa kauli na vitendo,  kulaaani  maovu haya na mengineyo yenye hata kupelekea roho za wanadamu wenzetu kutoweka.

Hakika, kama mtego ule wa panya, tutafanya makosa makubwa kama kuna watakaodhani,  kuwa haya ya watu kuchinjwa na kujeruhiwa na mapanga yatawakuta watu wa kundi fulani tu. Tukiacha yaendelee, basi, yeyote yule, bila kujali dini, rangi,  itikadi au hata wadhifa wake, anaweza kuwa mhanga wa maovu haya. Kama taifa,  kwa pamoja tuwalaani wauaji hawa.

Na hilo ni Neno Fupi la Usiku Huu.

Maggid Mjengwa,
Iringa.

BORA JUA

Yombo

SIMBA YA ULAYA


 Nyomi iliyofulika kuja kuangalia mechi


Mchezaji wa timu ya Simba Mganda Emmanuel Okwi akikokota mpira kuelekea goli la timu ya Al Ahly Shandy, huku mchezaji wa timu ya Isaac Seun Malik wa timu ya Al- Shandy ya Sudan akijaribu kumzuia katika mchezo wa kombe la Shirikisho unaofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Simba, imefanikiwa kuitandika Al Shandy ya Sudan magoli 3-0 katika kipindi cha lala salama na kutoka kifua mbele katika mchezo huo wa kwanza kabla ya ule wa Sudan wiki mbili zijazo.
Magoli ya Simba yamefungwa na wachezaji Haruna Moshi dk 66, Patrick Mafisango dk 77,  na Emmanuel Okwi88, hata hivyo mchezji Patrick Mafisango alikosa penati baada ya mchezaji Emmanuel Okwi kuchezewa vibaya na beki wa timu ya Al Ahly Shandy katika kipindi cha kwanza.

Saturday, April 28, 2012

DAR ALL STARS vs AND1

 AND1 TEAM
DAR ALL STARS
 
Hii ni noma kuna vitu vinatokea mara moja tu kwa mwaka ndio kama hii  uwanja wa ndani wa Taifa Maskani ya wanaume Tmk 
You are invited to attend the most entertaining basketball game you have ever seen between AND1 basketball team from USA Vs Dar All Stars from Tanzania, @National Indoor court on Sunday 29th April,2012.

The entertainment will start from 12noon with various contests e.g. Dunks, 3 points shoot out, jump shots etc  and lots of give aways, the main show will start at 4PM.

Only Tshs. 2,000/= at the gate.

The whole tour is sponsored by Cocacola through SPRITE brand.

You are most welcome.

Phares Magesa,
Vice President
Tanzania Basketball Federation-TBF
------------------------------

---------------

MDAU AREJEA SWEDEN

 Mdau wangu Iddy Harambe leo alfajiri amerejea kwenye michakato yake Sweden hapa akiwa uwanja wa ndege wa Dar es Salaam
 Wakati wa kuondoka siku zote mabegi hayawi makubwa

Kushoto: Idd Harambe, Suma Harambe na Shemeji

Wednesday, April 25, 2012

MISS CHANG`OMBE WAANZA KUPEWA SOMO

Mratibu wa mashindano hayo, Thom Chilala (kushoto), akitoa somo kwa baadhi ya warembo
watakaoshiriki Miss Chang'ombe.

Warembo wanmaotarajia kuwania umalkia wa mashindano ya Miss Chang'ombe, wakiwa katika mazoezi ya awali jana kwenye viwanja vya Hoteli ya Lamada, Dar es Salaam. Mazoezi ya kukata na shoka yataanza rasmi Mei 1, mwaka huu na mashindano itakuwa Juni 9, mwaka huu..

 Mwalimu wa warembo hao,Vumilia Willbrod akiwaelekeza jinsi ya kusimama walipokuwa wakipiga picha ya pamoja wakati wa mazoezi hayo.

 Mwalimu Msaidizi wa mashindano hayo, Teddy Chilala (kulia)akitoa maelekezo kwa warembo kuhusu mavazi yanayotakiwa kuvaliwa wakati wa mazoezi
 
Msaada: machelablog

BANDARI DSM MABINGWA MASHINDANO YA UMMA

 Kapteni wa Mchezo wa Bao akikabidhi kombe kwa mgeni rasmi
 Kapteni wa Mpira wa wavu Irene akikabidhi kombe lao walilochukua
 Peter Nkwera kapteni wa Mpira wa Miguu akipeleka kombe walilochukua

 Kenny Mwaisabula akipeleka Kombe la Ushindi wa jumla
 Baadhi ya wachezaji walioshiriki katika mashindano hayo
Mgeni rasmi akitoa shukrani zake kwa wachezaji wote walioshiriki katika mashindano hayo.

Monday, April 23, 2012

ASKARI WAVAMIA TAWI LA CUF MBAGALA

Kundi la Askari wamevamia katika Tawi la CUF Mbagala kwa kiburugwa mtaa wa  kwa nyoka, chanzo cha uvamizi huo ni mtazamo wa kisiasa uliopo katika maeneo hayo, polisi walilazimika kutumia risasi za moto katika tukio hili

JK, Msiba Wa Jirani Na Yanayotokea Dodoma- Tafsiri Yangu

 
 (Pichani Naibu Waziri Athuman Mfutakamba akipitia magazeti Iringa, enzi hizo akiwa DC wa Kilolo)
 
Ndugu zangu,
Katika dunia hii mwanadamu huwezi kumchagua jirani yako. Jirani yako ni jirani yako. Msiba wa jirani ni msiba wako pia, unakuhusu.

Maana, kuna wanaohoji JK kuacha mambo ya nyumbani na kwenda kushiriki maziko ya Bingu wa Mutharika. Silioni kosa katika hilo. Na hata kama JK angeamua kutokwenda mazikoni Blantyre, bado, asingekwepa lawama. Maana, kuna ambao wangemlaumu JK kwa kutozingatia mila na desturi zetu Waafrika; kushiriki kwenye kumzika jirani yako. 

Tukumbuke, kuwa Wamalawi si tu ni jirani zetu, ni ndugu zetu pia. Kuna Wanyasa wengi wa Malawi katika nchi hii waliochanganyika na makabila yetu. Na tunaambiwa, kuwa siku ya mkesha wa Uhuru wa Malawi, Watanzania wengi kando ya Ziwa Nyasa  nao walikesha wakishangilia. Uhuru wa Mnyasa ni Uhuru wetu.
Msiba wa Mnyasa, ni msiba wetu.

Mengineyo...

Nchi yetu inapita sasa kwenye kipindi kigumu sana. Tusishushe chini kiwango cha mjadala. Kubaki kumjadili JK na safari kwenda kutuwakilisha mazikoni ni kushusha kwa makusudi kiwango cha mjadala. Kwa makusudi tutakuwa  tumeacha kujadili hoja za msingi ikiwamo hii ya  kashfa za ufisadi wa kutupwa uliodhihiri bungeni na unaotutaka tuweke shinikizo kwa wahusika kuachia ngazi na hata kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Maana, anayeliibia taifa ni mhalifu tena zaidi ya mwizi wa kuku. Huyu ni jambazi. Kumwacha aendelee kukalia ofisi ya umma  ni sawa na kumsusia mlevi bia, au kumpa fisi kazi ya kulinda bucha.

Tuliko sasa ni kubaya. Tunakokwenda kutakuwa ni kubaya sana kama hatutachukua hatua sasa. Nimeona asubuhi ya leo kwenye runinga ( Channel Ten)  utetezi wa ajabu kutoka kwa Waziri wa Uchukuzi Bw. Omar Nundu.   

Nundu anadai hawezi kujiuzuru kwa kutoa hoja ambazo kimsingi zinamtaka aachie ngazi haraka iwezekanavyo ili abaki na heshima kwa jamii kama bado anayo.

Anatwambia Watanzania kuwa amekuwa 'akizungukwa' na Naibu wake Athuman Mfutakamba.  Ndio, Waziri Nundu anapojitetea kwa Watanzania  kwa kusema haelewani na Naibu wake  na kuwa kampuni ya Kichina ilimpeleka Naibu wake China, Mauritania na  Equatorial Guinea bila kibali chake inatosha kuonyesha kiwango cha juu cha ukosefu  wa nidhamu, uwajibikaji na uadilifu katika baraza la mawaziri .  Sioni ni kwa namna gani maelezo ya Nundu yanaweza kumlinda mbali ya kuonyesha ulazima wa  kuwajibishwa kwake haraka iwezekanavyo.

Ndio huwezi kuonyesha kuwa ulijua kilichokuwa kikifanyika, ukabaki kimya mpaka unatwambia hii leo, halafu utake ridhaa ya umma ikuamini kuendelea kukupa dhamana ya kushika nafasi hiyo hiyo.

Na wahenga walisema; kwenye msako wa nyani ngedere hawezi kusalimika.
Ndio, tutafanya makosa kudhani kuwa ’madudu’ haya yaliyoibuliwa kwenye ripoti ya CAG yanahusu Wizara tano au sita tu.  Hii ni fursa pekee kwa Watanzania kupitia wabunge wao kuendesha ’ msako mkubwa’ wa wote wenye kulitafuna taifa letu tunalolipenda.

Ni wakati pia wa kuhakikisha  Katiba Mpya tunayokwenda kuitolea mapendekezo yetu itusaidie kuziba  mianya ya wezi wa mali ya umma kuendelea kuliibia taifa bila ya hofu ya kufikishwa mahakamani na hata kutiwa magerezani.

Ndio, hatuwezi kuenenda kama tunavyoenenda sasa; maana,  unapoona Wananchi wanalalamika, Wabunge wanalalamika, Mawaziri  wanalalamika, na Rais analalamika, basi, hilo ni taifa la ajabu sana. Taifa la Walalamikaji.

Na maradhi ya  ' kulalamika' ni  ya kimfumo. Ni mfumo mbovu tu ndio unaoweza kuzaa Taifa la Walalamikaji. Turekebishe mfumo wetu kwa kupitia Katiba. Inawezekana.

Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765