Pages

Monday, October 31, 2011

MAJAMBAZI YAPORA TEMEKE

 Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo katika tukio hilo

 michirizi myeusi inayoonekana ni damu baada ya kupigwa

 Watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamevamia duka moja la uuzaji wa jumlawa dawa za binadamu maeneo ya Temeke hospita, baadhi ya walioshuhudia  tukio hilo wamesema baada ya watu hao kuingia dukani walitaka funguo ya garina pesa, na mmliki wa hilo duka hakutaka kubishana nao na aliwapa baada ya kupokea funguo waliamua kumpiga risasi mbili za kifua na kutokome

MTOTO KAKUA

Imekaaje hii

Mtoto India awa wa bilioni saba duniani

Nargis awa mtoto wa Bilioni Saba duniani

Mtoto aliyezaliwa nchini India ametangazwa na shirika linalotetea haki za watoto la Plan International kuwa mtu wa bilioni saba.
Mtoto Nargis alizaliwa saa kumi na moja kasoro dakika tano (saa za Afrika Mashariki) katika kijiji cha Mall katika jimbo la Uttar Pradesh nchini Libya.
Plan International linasema Nargis amechaguliwa kama ishara kwa sababu si rahisi kujua kihalisi kuzaliwa kwa mtoto wa bilioni saba.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa Jumatatu 31 Octoba, idadi ya watu duniani itafikia bilioni saba.
Mapema Jumatatu, Ufilipino ilitangaza mtoto wake wa bilioni saba, mtoto wa kike aliyezaliwa katika hospitali ya Manila.
Kila dakika watoto 51 wanazaliwa India, 11 kati yao ni kutoka jimbo lenye watu watu wengi la Uttar Pradesh.
Nargis alizaliwa na wazazi Vinita na Ajay Kumar Jumatatu katika hospitali ya serikali kijijini Mall karibu kilometa 50 kutoka mji mkuu wa jimbo hilo Lucknow, afisa mmoja wa Plan International ameiambia BBC.
Mtoto huyo Nargis wa mkulima maskini alichaguliwa kuwa wa bilioni saba kuelekeza malengo yake ya kupambana na utamaduni potofu dhidi ya watoto wa kike na idadi yao, shirika hilo limesema.
Mamia kwa maelfu ya mimba changa za watoto wa kike zinatolewa nchini Inida kila mwaka, licha ya haki ya kujua jinsia ya mtoto na matumizi ya teknolojia ya mionzi kujua jinsia kuzuiliwa kisheria.
Picha za mtoto Nargis zilionyeshwa katika hafla iliyohudhuriwa na karibu wanakijiji 250 katika hospitali hiyo, mwandishi wa BBC Ram Dutt Tripathi amearifu kutoka Mall.
Maafisa wa afya walitoa cheti cha kuzaliwa kwa baba wa mtoto katika maadhimisho hayo.
"Tunamuombea mtoto wetu ," Ajay Kumar alisema. "Huyu ni Lakshmi [mungu wa utajiri wa kihindu], ataleta bahati nzuri kwetu," alisema.

'Mtoto wa Bilioni 7 " azaliwa mara tatu Urusi

Hata hivyo katika Urussi ambayo ni miongoni mwa nchi chache ambazo idadi ya wakaazi wake inazidi kupungua--watoto watatu waliozaliwa Jumaatatu usiku wamepewa vyeti vya kuwatambulisha kuwa ni mtu wa billioni 7 duniani. .
Mmojawao alizaliwa Petropavlovsk-Kamchatsky, Mashariki ya Mbali, na wengine katika miji ya Kaliningrad na St Petersburg. Umoja wa Mataifa umefahamisha wazi kwamba vyeti hivi ni ishara tu na hazina uzito nje ya Urussi.
Hata hivyo kuzaliwa kwa watoto hao kumetangazwa kwa marefu na mapana nchini Urussi kupitia wavuti wa Rais.
Katika Kamchatsky inafahamika baada ya mwaka mmoja mama wa mtoto billioni 7 atatunukiwa fleti ya vyumba viwili .


Kinyume na kuzaliwa kwa mtoto billioni 6 mnamo mwaka 1999;safari hii Umoja wa Mataifa hautamtambua rasmi mtoto mmoja na mahali alikozaliwa. Umoja wa Mataifa unasema kuzaliwa kwa mtu wa billioni 7 si wakati wa kusherehekea,lakini ni wa kutafakari mustkbala wa dunia yetu.

Hata hivyo katika Urussi ambayo ni miongoni mwa nchi chache ambazo idadi ya wakaazi wake inazidi kupungua--watoto watatu waliozaliwa Jumaatatu usiku wamepewa vyeti vya kuwatambulisha kuwa ni mtu wa billioni 7 duniani. .
Mmojawao alizaliwa Petropavlovsk-Kamchatsky, Mashariki ya Mbali, na wengine katika miji ya Kaliningrad na St Petersburg. Umoja wa Mataifa umefahamisha wazi kwamba vyeti hivi ni ishara tu na hazina uzito nje ya Urussi.
Hata hivyo kuzaliwa kwa watoto hao kumetangazwa kwa marefu na mapana nchini Urussi kupitia wavuti wa Rais.
Katika Kamchatsky inafahamika baada ya mwaka mmoja mama wa mtoto billioni 7 atatunukiwa fleti ya vyumba viwili .


Kinyume na kuzaliwa kwa mtoto billioni 6 mnamo mwaka 1999;safari hii Umoja wa Mataifa hautamtambua rasmi mtoto mmoja na mahali alikozaliwa. Umoja wa Mataifa unasema kuzaliwa kwa mtu wa billioni 7 si wakati wa kusherehekea,lakini ni wa kutafakari mustkbala wa dunia yetu. 

BBC

Saturday, October 29, 2011

WARM UP






Mpira mpaka sasa unaendelea na matokeo bado 0-0
Mechi imekwisha na Yanga imeshinda 1-0 goli lililofungwa na Davies Mwape

UWANJA WA TAIFA MCHANA KUSUBIRI YANGA NA SIMBA

Umati wa watu waliofurika kuangalia  mechi hapa watu wakiingia uwanjani

 Nyomi Uwanja wa Taifa Leo
 Simba kidedea
Kila mtu na timu yake

Wednesday, October 26, 2011

Moto wateketeza kituo cha watoto yatima

MOTO mkubwa umeteketeza kituo cha kulea watoto yatima cha Orphan Center cha Majimatitu Chasimba na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime alisema, moto huo ulizuka juzi mchana na kuteketeza nyumba hiyo yenye vyumba vitano mali ya Hidaya Shukrani (40) ambaye pia ni mkazi wa Majimatitu.

Alisema kuwa moto huo uliteketeza mali zote zilizokuwamo ndani ya kituo hicho na haukusababisha madhara yoyote kwa binadamu.

Chanzo cha moto huo na thamani ya mali zilizoteketea bado haijafahamika na moto huo ulizimwa na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji cha Jiji kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo.

Wakati huo huo, moto mwingine umezuka maeneo ya Mwenge Kijijini na kuteketeza nyumba ya uwani ya Michael Temu (61), mkazi wa eneo hilo pamoja na mali zote zilizokuwamo ndani likiwemo gari namba TZJ 3800 aina ya Toyota Staut.

Chanzo cha moto huo ambao ulizuka juzi jioni hakijafahamika na upelelezi unaendelea ili kufahamu thamani halisi ya mali zilizoharibika.

Moto mwingine umezuka na kuteketeza duka la Rashid Ally lililopo maeneo ya Njiapanda ya Uwanja wa Ndege karibu na baa ya Rongai.

Chanzo cha moto huo inasadikiwa ni jiko la mkaa lililokuwa limewashwa na mwenye duka na haukusababisha madhara yoyote kwa binadamu.

Monday, October 24, 2011

Baba ashuhudia mwanae akikatwa mkono, akinyofolewa vidole

MSOMAJI hili ni tukio la kusikitisha, kuhuzunisha na pengine laweza kukutoa machozi kama ilivyonitokea, lakini nakuomba uwe mvumilivu ili kuviachia vyombo vya usalama na sheria vifanye kazi yake.

Matukio ya kikatili, kudhalilisha utu wa mwanadamu na ambayo yanahitaji kukomeshwa kwa gharama yoyote ile ya kukata sehemu za miili ya walemavu wa ngozi, yaani Albino, yalikoma kwa muda, pengine ni kutokana na harakati zilizoanzishwa na Rais Jakaya Kikwete za kuwasaka na kuwafikisha mbele ya mkono wa sheria.

Lakini yaonekana juhudi hizo, hazijazaa matunda. Tatizo hilo ambalo limesababisha wanadamu na Watanzania wenzetu kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa viungo wa kudumu, limerejea tena Kanda ya Ziwa.

Mmoja wa waliofikwa hayo ni kijana Adam Robert (14), ambaye alijitahidi kutetea maisha yake dhidi ya wauaji wenye tamaa ya ya pesa kwa nguvu ya ushirikina.

Robert ni mlemavu wa ngozi (albino), mkazi wa kijiji cha Nyaruguguna Kata ya Nyijundu wilayani Geita katika mkoa mpya wa Geita.

Kwa sasa, kijana huyo amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita, akipatiwa matibabu, baada ya kukatwa mkono wa kushoto na kisha kunyofolewa vidole vitatu vya mkono wa kulia.

Tukio hili limetokea usiku wa kuamkia Jumamosi ya Oktoba 15 mwaka huu, nyumbani kwao na mlemavu huyo. Siku hiyo alivamiwa na mtu mmoja ambaye bado hajatambulika wala kutiwa mbaroni na polisi, ingawa upelelezi mkali unaendelea wilayani Geita juu ya tukio hilo.

Siku hiyo ya tukio majira ya saa 7 na dakika kadhaa usiku, napigiwa simu na moja ya vyanzo vyangu vya habari wilayani Geita na kujulishwan juu ya kuwepo kwa tukio hilo.

Chanzo hicho kilinisisitizia kwamba hali ya majeruhi ni mbaya sana, ambapo gari la polisi limeamua kuachana na msako wa mtu anayetuhumiwa kujihusisha na kitendo hicho ili kumkimbiza hospitalini kujaribu kuokoa maisha ya mlemavu huyo.

‘’Wewe rafiki yangu unalala sasa hivi wakati huku kuna tukio kubwa limetokea? Nyanyuka uende hospitalini kuna mlemavu wa ngozi au albino amejeruhiwa vibaya kwa kukatwa mkono na kunyofolewa vidole vitatu, hali yake ni mbaya, tuko njiani tunamleta hospitali hapo Geita…..’’ kilisema chanzo hicho cha habari kupitia simu ya mkononi kikinipa taarifa za tukio hilo.

Nikanyanyuka kutoka kitandani. Nilipoangalia saa yangu nilibaini kuwa ni saa 7 :30 usiku, nikajiuliza umbali alipo mtu huyo ni kilomita zaidi ya 90, hivyo mpaka atakapofika hospitalini itakuwa saa 10 alfajiri, nikasema hapana ni bora nilale ili asubuhi niwahi hospitalini.

Kesho yake niliamka mapema na kwenda hospitalini majira ya saa 1:30, nilipofika katika hospitali hiyo, nikaenda moja kwa moja wodi ya wanaume namba 8, kwa sababu usiku wake nilikuwa nimeelezwa kwamba majeruhi ni mwanamume, hivyo nilijua kwamba kwa vyovyote atakuwa katika wodi hiyo.

Nilipoingia tu, macho yangu yaligota kwa mlemavu huyo, ambaye amelazwa kitanda namba 5 katika wodi hiyo. Nilimtambua mapema ikizingatiwa kwamba siku hiyo hakukuwa na wagonjwa wengi waliolazwa katika wodi hiyo.

Nilipofika kwa mtoto huyo, nilimkuta mtu mmoja ambaye baada ya kujitambulisha kwake, aliniambiwa kwamba yeye ni baba wa mlemavu huyo. Wakati huo mtoto huyo alikuwa akihema juu juu huku akiwa na dripu ya kumuongezea damu mkononi mwake. Hakika hali ile ilinisikitisha sana na kujikuta nikitokwa na machozi .

Siyo mara yangu ya kwanza kushuhudia tukio kama hilo la kujeruhiwa kwa albino. Nimewahi kushudia matukio makubwa, ikiwemo kushuhudia mwili wa albino aliyeuawa vibaya baada ya kukatwa miguu yote miwili. Huyo wauaji walimkata miguu yote miwili kwenye mapaja na kubakiza usawa wa makalio tu!.

Baada ya hapo, nikaanza kumhoji baba wa mlemavu huyu ambaye alijitambulisha kwangu kwa jina la Robert Tangawizi (36). Alinisimulia kwa kina juu ya tukio hilo. Hata hivyo, muda wote alionekana kama mtu mwenye wasiwasi na alikuwa akitetemeka. Wakati mwingine alikuwa akitetemeka mno hadi kushindwa kuongea.

Akisimulia zaidi mkasa huo, baba huyo anasema siku ya tukio alifika nyumbani majira ya saa moja kasoro na alimkuta mwanae nyumbani akitengeneza kuni kwa ajili ya moto wa kuota, maarufu kwa jina la Kikome. Wakasalimiana kisha yeye akaenda ndani na kuhifadhi jembe lake, ambalo alikuwa ametoka nalo shambani.

Baadaye alitoka nje na kukuta mwanae akiwa amekwishawasha moto, akaenda kuketi naye huku wakiota moto. Muda mfupi baadaye alimuona mtu amesimama umbali wa mita 20 hivi shambani. Alimuita na kutaka kujua shida yake.

Mtu huyo alipofika, alimwambia kwamba anatafuta ng’ombe wake, aliodai kuwa walikuwa wamepotea tangu asubuhi. Alimkaribisha na kumpatia kiti. Alipoketi walianza kuota moto huku wakiendelea na mazungumzo yao juu ya upotevu wa ng’ombe wake.
Ghafla mtoto wake huyo (majeruhi) akamwambia kwamba mtu siyo mzuri, kwani tangu mchana alikuwa anamfuatafuata alipokuwa malishoni akiwa na ng’ombe, ambako alikuwa akimdanganya kuwa angempatia kofia.

Baada ya kusikia mwanae akimueleza hivyo juu ya mtu ambaye wameketi naye, aliamua kumvuta pembeni na kumtaka amueleze vizuri, ambapo huko alisisitiza kuwa mtu huyo alikuwa akimdanganyia kofia kwamba akaichukue, lakini yeye alikataa. Baadaye, alimtaka warejee kwenye kikome na wakafanya hivyo.
“Tukarejea na tukaketi, lakini kabla sijaanza kumuuliza zaidi mtu huyo, chakula kikaletwa mbele yetu, tukanawa na kuanza kula. Ghafla mvua ikaanza kunyesha hivyo ikabidi nichukue ugali na mwanangu huyu akachukua mboga ili twende kula ndani. Nikatangulia kuelekea ndani, lakini nilipoingia tu ndani, nikasikia kishindo na kelele za huyu mwanangu akilia, nikatoka nje nikasimama mlangoni. Nilipoangalia niliona mtu huyo aking’ang’ana kuukata mkono wa kulia wa mwanangu. Nilishikwa na butwaa na kushindwa la kufanya pamoja na kwamba kitendo hicho kilichukua zaidi ya dakika 10. Baada ya mtuhumiwa huyo kumaliza kutenda unyama huo, aliondoka na kutokomea gizani na ndipo nilipoamua kuanza kuwaita majirani ili waje kusaidia”, anasema.
Habari leo

MLOPELO AFUNGUKA

Kwa jina anaitwa Khalid ni msanii wa maigizo alishawahi kuigiza kipindi cha nyuma akiwa na kundi la kaole,Jamaa ni mkazi wa temeke wailes,mimi kumbukumbu zangu toka nipo mdogo nimemkuta kama alivyo hivi.Siku za karibuni alitoa malalamiko yake katika media kwamba amepeleka nyimbo yake clouds fm na imewekwa kapuni haipigwi. 
Asante Darstockholm & Zamaradi (Take One)

Thursday, October 20, 2011

washerehekea kufa kwa Gaddaf

Majeshi ya Libya 'yamkamata Gaddafi'

Makamanda kutoka baraza la mpito la Libya wamesema wamemkamata aliyekuwa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.
Taarifa hizo zimetolewa baada ya majeshi ya baraza hilo la mpito kudai kudhibiti Sirte, mji alipozaliwa Kanali Gaddafi.
Hakuna uthibitisho huru wa kukamtwa kwake.
Kanali Gaddafi alichukua madaraka nchini Libya mwaka 1969.
Alitolewa madarakani katika machafuko yaliyoanza mwezi Februari.
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC unataka akamatwe.
"Amekamatwa. Amejeruhiwa miguu yake yote miwili," afisa wa baraza la mpito la taifa (NTC) Abdel Majid ameliambia shirika la habari la Reuters.
"Amechukuliwa na gari la kubebea wagonjwa."
Shirika la habari la AFP limemnukuu afisa mwengine wa NTC, Mohamed Leith, akisema Kanali Gaddafi amekamatwa mjini Sirte na "amejeruhiwa vibaya" lakini bado anapumua.

TEVEZ AGEUKA TAKATAKA MANCHESTER


washabiki wa Man Utd na City wakishirikiana kutupa jezi  za Tevez katika Mji wa Manchester.

Carlos Tevez is fast becoming public enemy No 1 in Manchester and he may want to avoid the Old Trafford area this Sunday.
The Argentine striker, who quit Manchester United for rivals City in 2009, will miss this weekend's top-of-the-table derby clash after his alleged refusal to come off the bench against Bayern Munich last month has seen him cast aside by manager Roberto Mancini.
City fans have since turned on their former captain with Manchester now seemingly united in their loathing of the ex-West Ham star.


Wednesday, October 19, 2011

Pedro Pires: Mshindi wa tuzo ya Mo

Historia ya Pedro Pires inakwenda sambamba na historia ya Cape Verde yenyewe. Alizaliwa mwezi April mwaka 1934, katika kisiwa cha Fogo, wakati wa utawala wa Wareno na alishiriki vilivyo katika harakati za mapinduzi.
Aliongoza nchi wakati wa utawala wa chama kimoja na kufuata itikadi za Ki- Marx.
Pedro
Pedro Pires katika majadiliano kuhusu Ivory Coast

Baadaye aliongoza nchi katika utawala wa vyama vingi na kuanzisha uchumi wa biashara huria.
Bw Pires kwa mara ya kwanza alikumbana na vuguvugu la kupinga ukoloni, wakati alipoondoka Cape Verde na kwenda kusoma mjini Lisbon, Ureno wakati akiwa na miaka 16.
Huko alikutana na viongozi wa vuguvugu linalopinga utawala wa Ureno barani Afrika. Mwezi Juni mwaka 1961, kama sehemu ya vuguvugu la vijana wa Afrika, aliamua kuondoka Ureno na kujiunga na chama kudai uhuru cha Guinea na Cape Verde PAIGC kilichokuwa kikiongozwa na Amilcar Cabral.
Baadaye alifanya shughuli zake nchini Senegal na Ufaransa akikusanya raia wa Cape Verde kwa ajili ya mapigano ya kutumia silaha dhidi ya Ureno.
Alikuwa waziri mkuu baada ya nchi kupata uhuru mwaka 1975 hadi mwaka 1995.
Bw Pires aliongoza mchakato wa kuingia katika mfumo wa vyama vingi nchini Cape Verde, hali iliyosababisha chama chake cha PAICV kupoteza uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi katika ubunge na urais.
Miaka kumi baadaye, aligombea urais na kupata ushindi mwembamba baada ya duru ya pili. Chama cha upinzani cha MPD kilipinga uhalali wa ushindi wake na kususia sherehe za kuapishwa kwake.
Aliwania tena muhula wa pili mwaka 2006 na safari hii kushinda katika duru ya kwanza.
Wakati akiwa madarakani, Cape Verde imeshuhudia mabadiliko katika sekta za afya na elimu. Nchi hiyo ikawa ya pili barani Afrika kufanikisha kiwango cha kipato cha kati kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Katika nyanja za kimataifa, serikali ya bw Pires ilihusika kwa kiwango kikubwa katika mchakato wa majadiliano yaliyosababisha kupatiaka na uhuru wa Namibia na pia kuondoka kwa wanajeshi wa Cuba na Afrika Kusini nchini Angola.
Bw Pires aliondoka madarakani mwaka 2011, baada ya mihula miwili, akitupilia mbali wito wa kubadili katiba na kusalia madarakani.
Na ulikuwa upande wa upinzani uliopata ushindi baada ya uchaguzi uliofanyika baada ya kuondoka.
Hatua ya kubadilishana serikali ilifanyika kwa nia ya amani.
Pedro Verona Rodrigues ana mke na watoto wawili wa kike.

Thursday, October 13, 2011

ENZI ZA MWALIMU

HATUA MOJA MBELE

Mdau Juma Marijani kushoto akiwa na mmoja wa Mwanazuoni mwenzake baada ya kumaliza degree applied ya Accounting katika chuo cha Anglia Ruskin University cha Uingereza
Juma Marijani wa Kwanza kushoto akiwa na wanachuo baada ya kupata vyeti vyao

Tuesday, October 11, 2011

TANDIKA RELINI

Kitu cha ugali kikitoka pembeni dogo akijisaidia, choo paspot saiz

Yombo Relini-Bondeni

Asili ya Hip Hop imeanzia huku

MAITI YA MWANACHAMA CHADEMA YAKUTWA PORINI

MAITI ya mkazi wa Dar es Salaam, Mbwana Masudi Mbwana anayedaiwa kuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imepatikana katika pori la Magereza katika Barabara ya Mwanzugi wilayani Igunga, mkoani Tabora ikiwa imeharibika.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Anthony Lutta, kwa sasa Polisi wanasubiri ripoti ya uchunguzi wa daktari itakayobainisha sababu ya kifo cha mtu huyo.


Chadema wametoa taarifa kwa vyombo vya habari wakitaka Polisi ifanye uchunguzi wa kifo cha mwanachama wao huyo ambaye wanadai alipotea, kwa kuwa taarifa za awali za uchunguzi zinaonesha kuwa mwili wa marehemu una majeraha, macho yametobolewa na kichwa kimepasuliwa kutokana na kipigo.


“Ni kweli Polisi tulipokea Oktoba 2, mwaka huu siku ya uchaguzi Igunga, taarifa kutoka kwa Chadema juu ya kupotea kwa mwanachama wao ila mpaka sasa uchunguzi kuhusu suala hilo unaendelea,” amesema Kamanda Lutta.


Amesema, askari walioenda kuichukua maiti hiyo katika eneo ilikopatikana, waliikuta ikiwa katika hali mbaya hivyo suala la macho kutoboka au kichwa kupasuliwa hawakuliona. “Na ndio maana kwa sasa tunasubiri kwanza ripoti ya daktari,” alifafanua Kamanda huyo.


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe katika taarifa yake leo kwa vyombo vya habari, alisema chama hicho kinalaani ilichokiita mauaji na uharamia aliofanyiwa mwanachama wao huyo aliyewasili Igunga Septemba 30, mwaka huu kushiriki katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge akiwa wakala wa chama hicho.


“Hata hivyo, tangu awasili hakuonekana tena hadi Oktoba 9, mwaka huu maiti yake ilipopatikana katika pori hilo la Magereza,” alisema Mbowe na kuvitaka vyombo vya dola kuchunguza haraka na kuwakamata wote waliohusika na tukio hilo na kuwataka wananchi wenye taarifa yoyote kuiwasilisha kwenye vyombo vya usalama ili sheria ichukue mkondo wake.


Amesema, kwa kuwa mwili wa marehemu umeharibika vibaya, chama hicho kimeshauriana na ndugu wa marehemu na kukubaliana azikwe leo Igunga kwa heshima zote za chama na baadaye maombi na sala kwa marehemu vitafanyika Dar es Salaam.

Habari leo. 

ENOCK WA- TMK MAJITA

 Muanzilishi wa kundi la TmK Majita Enock wa kati akiwa na wafanyakazi wenzake katika ofisi za  Multichoice Dar es Salaam kwa sasa kundi hilo linajiandaa kutoa album abayo itakuwa na nyimbo 8
 Hapa Enock kabla hajawa kibonge wazee wa misumari

Enock akiwa na rafiki zake wa kundi la Tmk Majita hii ilikuwa mwaka 2005 kaeni kwa mkao mpya wakazi wa Temeke na Tanzania kwa ujumla kabla ya kuitambulisha single yao mpya inayo kuja  hivi karibuni

Saturday, October 8, 2011

TOGWA

Kinywaji chetu cha asili, ila kinazidi kutoweka kinywaji hiki nilikutana nacho maeneo ya Yombo Relini

WAKAZI WA MTONI WALALAMIKA MALIPO YAO

 Baadhi ya viongozi wa Mtoni Mtongani ambao mpaka sasa wanalalamika kwa Serikali kwa kutolipwa fidia zao ambazo walipisha upanuzi wa barabara ya Kilwa tangu mwaka 2002 mpaka hii leo hawajapata haki zao, ambapo M/kiti Jamal Mkumba mwenye shati la mistari na Mzee Juma Makarani Katibu mwenye shati jeupe wakiwasikiliza wakazi wa eneo lao la Mtoni.
 Wananchi waliohudhuria kikao hicho ambacho kilifanyika katika shule ya Msingi Bokorani maarufu kwa Mama Marry Mtoni Mtongani
Mzee Hamis Mwinyimvua akitoa malalamiko yake kwa baadhi ya viongozi hao baada ya kuona suala lao halipewi kipaumbele na Serikali ilishatangaza kuwa pesa yao ishatoka.

BAGAMOYO ASUBUHI

 Hotel inayotumika baadhi ya wakazi wa Bagamoyo

 Tukipata kifungua kinywa.

 Petrol haina haja ya kwenda ya Petrol Station mtaani tu inapatikana

 Baadhi ya Mitaa ya Bagamoyo inavyoonekana



 Baadhi ya Wanafunzi wa shule za sekondari wakipata maelekezo katika eneo la bagamoyo

 Njia ya kuelekea Soko la Samaki



 Jahazi zikisubiri abiria wa kwenda Zanzibar


 Madungu yashaanza kujitokeza