Pages

Wednesday, October 26, 2011

Moto wateketeza kituo cha watoto yatima

MOTO mkubwa umeteketeza kituo cha kulea watoto yatima cha Orphan Center cha Majimatitu Chasimba na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime alisema, moto huo ulizuka juzi mchana na kuteketeza nyumba hiyo yenye vyumba vitano mali ya Hidaya Shukrani (40) ambaye pia ni mkazi wa Majimatitu.

Alisema kuwa moto huo uliteketeza mali zote zilizokuwamo ndani ya kituo hicho na haukusababisha madhara yoyote kwa binadamu.

Chanzo cha moto huo na thamani ya mali zilizoteketea bado haijafahamika na moto huo ulizimwa na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji cha Jiji kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo.

Wakati huo huo, moto mwingine umezuka maeneo ya Mwenge Kijijini na kuteketeza nyumba ya uwani ya Michael Temu (61), mkazi wa eneo hilo pamoja na mali zote zilizokuwamo ndani likiwemo gari namba TZJ 3800 aina ya Toyota Staut.

Chanzo cha moto huo ambao ulizuka juzi jioni hakijafahamika na upelelezi unaendelea ili kufahamu thamani halisi ya mali zilizoharibika.

Moto mwingine umezuka na kuteketeza duka la Rashid Ally lililopo maeneo ya Njiapanda ya Uwanja wa Ndege karibu na baa ya Rongai.

Chanzo cha moto huo inasadikiwa ni jiko la mkaa lililokuwa limewashwa na mwenye duka na haukusababisha madhara yoyote kwa binadamu.

No comments:

Post a Comment