Pages

Wednesday, October 19, 2011

Pedro Pires: Mshindi wa tuzo ya Mo

Historia ya Pedro Pires inakwenda sambamba na historia ya Cape Verde yenyewe. Alizaliwa mwezi April mwaka 1934, katika kisiwa cha Fogo, wakati wa utawala wa Wareno na alishiriki vilivyo katika harakati za mapinduzi.
Aliongoza nchi wakati wa utawala wa chama kimoja na kufuata itikadi za Ki- Marx.
Pedro
Pedro Pires katika majadiliano kuhusu Ivory Coast

Baadaye aliongoza nchi katika utawala wa vyama vingi na kuanzisha uchumi wa biashara huria.
Bw Pires kwa mara ya kwanza alikumbana na vuguvugu la kupinga ukoloni, wakati alipoondoka Cape Verde na kwenda kusoma mjini Lisbon, Ureno wakati akiwa na miaka 16.
Huko alikutana na viongozi wa vuguvugu linalopinga utawala wa Ureno barani Afrika. Mwezi Juni mwaka 1961, kama sehemu ya vuguvugu la vijana wa Afrika, aliamua kuondoka Ureno na kujiunga na chama kudai uhuru cha Guinea na Cape Verde PAIGC kilichokuwa kikiongozwa na Amilcar Cabral.
Baadaye alifanya shughuli zake nchini Senegal na Ufaransa akikusanya raia wa Cape Verde kwa ajili ya mapigano ya kutumia silaha dhidi ya Ureno.
Alikuwa waziri mkuu baada ya nchi kupata uhuru mwaka 1975 hadi mwaka 1995.
Bw Pires aliongoza mchakato wa kuingia katika mfumo wa vyama vingi nchini Cape Verde, hali iliyosababisha chama chake cha PAICV kupoteza uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi katika ubunge na urais.
Miaka kumi baadaye, aligombea urais na kupata ushindi mwembamba baada ya duru ya pili. Chama cha upinzani cha MPD kilipinga uhalali wa ushindi wake na kususia sherehe za kuapishwa kwake.
Aliwania tena muhula wa pili mwaka 2006 na safari hii kushinda katika duru ya kwanza.
Wakati akiwa madarakani, Cape Verde imeshuhudia mabadiliko katika sekta za afya na elimu. Nchi hiyo ikawa ya pili barani Afrika kufanikisha kiwango cha kipato cha kati kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Katika nyanja za kimataifa, serikali ya bw Pires ilihusika kwa kiwango kikubwa katika mchakato wa majadiliano yaliyosababisha kupatiaka na uhuru wa Namibia na pia kuondoka kwa wanajeshi wa Cuba na Afrika Kusini nchini Angola.
Bw Pires aliondoka madarakani mwaka 2011, baada ya mihula miwili, akitupilia mbali wito wa kubadili katiba na kusalia madarakani.
Na ulikuwa upande wa upinzani uliopata ushindi baada ya uchaguzi uliofanyika baada ya kuondoka.
Hatua ya kubadilishana serikali ilifanyika kwa nia ya amani.
Pedro Verona Rodrigues ana mke na watoto wawili wa kike.

No comments:

Post a Comment