Pages

Friday, February 25, 2011

EVER GREEN QUEENS YAIFUNGA TMK QUEENS

 Timu ya soka ya  wanawake ya EVERGREEN wakikaguliwa kabla ya mchezo kuanza.

 Timu ya TMK Queens wakithibitishwa na mwamuzi kabla ya mchezo

 wachezaji wa TMK QUEENS
 Kazi na mwana mchezaji wa Evegreen Queens Jema Kilago akimpa mtoto lishe kabla ya Mchezo

 Moja ya patashika katika lango la Tmk Queens


 Marry Mtua aka (Tegete) akimkaba  Kibuna wa Evergreen

 Baadhi ya Wapenzi wa soka waliiojitokeza katika mchezo huo

 Swaumu akijaribu kumtoka Siwa wa EverGreen


 Mchezaji Bora wa Mechi Fatuma pamoja na kocha wake

 wachezaji wa Ever green wakishangili baada ya mechi
Mwenyekiti wa soka la wanawake Stephania akihojiwa na chombo cha habari

Timu ya soka ya Evergreen ya Temeke imeweza kuwaadhibu wapinzani wao wa TMK Queens kwa magoli 3-0 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa karume.
hadi kipndi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilikuwa suluhu ya 0-0 na kipindi cha pili kilipoanza mshambuliaji hatari wa Ever green Rukia aliweza kuipatia timu yake bao la kuongoza na katika dakika ya 60 Rukia aliipatia tena timu yake ya evergreen goli la pili dakika ya 67  na goli la tatu la evergreen lilifungwa kwa shuti kali alilopiga Vumulia Maarifa  na kumshinda kipa wa Tmk Queens Salama  hadi mwisho wa mchezo EVERGREENS QUEENS 3 - TMK QUEENS 0

Thursday, February 24, 2011

KONGAMANO LA VIJANA LA KIISLAM

Islamic Center for Research imeandaa kongamano la vijana wa Kiislam litakalofanyika tarehe 27/02/2011 katika ukumbi wa Al-haramain kuanzia majira ya saa 3.00 asubuhi

Hivyo mnaombwa kuhudhuria katika kongamano hilo bila kukosa ili kujua mustakhabari wa vijana wa kiislam kwa sasa na kujaribu kuchangia mada mbalimbali.

Nyote mnakaribishwa bila kukosa

MKOPO WA BIASHARA


Je wewe ni mfanyibiashara ama unanuia kuanzisha biashara hivi karibuni? Ni lazima basi utakuwa umewaza jinsi utakavyo pata fedha za kukuwezsha kuanzisha au kuipanua biashara yako.

Kuna njia mbalimbali za kupata fedha hizi unaweza kuweka akiba kwa muda fulani hadi kitakapotimia kiasi unachohitaji, unaweza pia kukopesha fedha hizo kutoka kwa jamaa na marafiki. Kila mojawapo ya njia hizi ina changamoto yake ambayo utakumbana nayo.

Habari njema sasa ni kuwa kando na njia hizi unaweza kupata mkopo kutoka kwa benki ama vyama vya ushirika lakini haina maana kuwa mikopo ya benki haina changamoto.

Hivi sasa kuna matangazo mengi ya benki na vyama vya ushirika katika magazeti, redio na vyombo vingine vya habari kuhusu namna ya kupata mikopo, kilicho muhimu ni wewe kama unyetaka mkopo kuchunguza kwa kina na uangalifu kuona ni benki ipi ama ni chama kipi cha ushirika kina mkopo ambao utakufaa.

Ni wazi kuwa benki hizi zinatumia lugha ya mvuto, kwa mfano benki ya Barclays nchini Kenya inafanya kampeni iitwayo ‘rarua mkopo’ ambapo ukijisajili kuchukua mkopo unewezeshwa kulipa mkopo ulio nao sasa. Huko Tanzania benki ya CRDB inatoa mkopo wa ‘Bidii’ mahsusi kwa wenye biashara ndogo.
Usipokuwa mwangalifu huenda ukaingia katika mpango ambao hauwezi kukimu ama kutoshelezi mahitaji yako. Lakini swali muhimu zaidi ni je utawezaje kutathmini mpango wa mkopo ambao unapendekezwa na benki fulani?

Kwanza jiulize ujue unahitaji pesa kufanya nini haswa katika biashara lako. Unataka kununua mashine, kukarabati vifaa, kuongeza mali ghafi au kuongeza uzalishaji ? na kufanya hivi utahitaji pesa kiasi gani, na ni muda gani ambao kwa mtazamo wako umetosha kuulipa mkopo huo na pia kulingana na mapato yako unaweza kulipa kiasi gani katika kila awamu ?
Baada ya kuzingatia mambo hayo hatua ya pili ni kusoma kwa kina masharti ambayo yamewekwa na benki ambayo inatoa mkopo ambao unaona unakufaa. Kwa kawaida masharti hayo licha ya kutegemea benki yenyewe huwa kama vile uwe raia wa nchi fulani, stakabadhi za kudhibitisha kuwa biashara yako ni halali na hulipa ushuru.

Kando na hayo utahitajika kuthibitisha una uwezo wa kulipa mkopo huo na hapa tena kulingana na kiasi ambacho unanuia kukopa huenda ukatakiwa kuweka dhamana kama vile gari, nyumba ama mali nyingine.

Hatua hii ndiyo italeta utata kwani inadaiwa kuna benki ambazo huficha taarifa na takwimu zilizo muhimu kama vile ada wanazo toza kando na zile za kulipa mkopo huo. Ni wajibu wako kuhakikisha umeelewa kikamilifu mkopo ambao umekubali kuchukua kabla ya kutia sahihi.

Kumbuka kuwa hatimaye utahitajika kulipa mkopo huo, na hivyo basi ni muhimu kuwa na mpango murwa wa kuulipa mkopo huo na jambo lingine la kutilia maanani ni kuwa na dhamira ya kuchukua mkopo ni kuanza au kuipanua biashara usije ukaingia katika mtego wa kuzifuja pesa hizo holela.

Msaada toka kwa:
Ken Owino

Saturday, February 19, 2011

Kambota: Tanzania Yetu, Dar Yetu Na Jeshi Letu


……Mjenga nchi ni mwananchi……..

Nimekaa nimetafakari naona iko haja ya kuandika kuhusu tukio la kulipuka kwa mabomu kule kambi ya Gongo la Mboto jijini Dar es salaam.


Ikumbukwe kuwa tukio hili linajitokeza ndani ya miaka mitatu tangu tukio la namna hiyo au linalofanana na hilo litokee kule Mbagala kuu na pia hapa sitaki kufanya assumption ila nalazimika kusema kuwa YAWEZEKANA BAADHI YA NDUGU WA WAATHIRIKA WA MBAGALA PIA WAMEATHIRIKA GONGO LA MBOTO.

Nani asiyejua kuwa ukiacha viongozi wa dini hapa Tanzania ni jeshi ndicho chombao ambacho kinaaminika zaidi hapa nchini? Nani asiyejua kuwa jeshi letu limedumisha nidhamu yake kwa muda mrefu licha ya mapungufu ya hapa na pale ikiwa ni pamoja na baadhi ya wanajeshi wachache kuhusika kwenye matukio kama ujambazi au kupiga raia lakini bado yatosha kusema jeshi letu tunaliamini sana.

Ingawaje ni ukweli wa kikatiba kama sio sheria kuwa kuandika kuhusu mambo ya jeshi kwa mtu asiye mwanajeshi ni kosa ila nafikiri kulipuka kwa mabomu na watu kuathirika sio jambo la jeshi bali la wananchi yaani watanzania hasa wa Dar es salaam ambao bila shaka ni waathirika wakubwa wa maafa hayo hivyo na kila sababu na haki ya kuliandikia tukio hili.

Kwa kweli tunaamini kuwa kilichotokea ni bahati mbaya sawa lakini kwanini hatukujifunza Mbagala? Kama kweli tulijifunza kwanini tukio hili limejirudia? Haya ni maswali ya msingi ambayo yanapaswa yajibiwe kwa hoja sio kwa kupoozana kwa kulipana fidia pekee au kuombana pole.

Sawa kulipana fidia ni muhimu kweli hata kupeana pole ni swala la ubinadamu lakini hoja sio hii la msingi hapa jeshi letu lirudishe imani ya wananchi ambayo imeanza kupotea kwa jeshi hilo.

Kuna maneno yamezagaa kuwa mara jeshi letu halina wataalamu, mara uzembe tu, mara kutofanyika kwa ukaguzi wa mara kwa mara lakini haya sio mambo mazuri kuzungumzwa kuhusiana na jeshi letu. Mimi nadhani na naamini hata mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na mnadhimu mkuu wa jeshi Luteni Jenerali Abdurahman Shimbo na hata wanajeshi naamini hata wao hawapendi kauli hizi hata kidogo , leo wangependa kuona watu wakisema ….aah! jeshi letu lina wataalamu waliobobea bwana…, hakuna uzembe jeshini…., jeshi letu ni la wachapakazi……au jeshi letu safi sana bwana…



Lakini haya hayaji hivihivi hata kidogo, yanajengwa , kama watu sasa walivyojengwa bila kujua sasa wanaiogopa Dar es salaam, wanaogopa jeshi badala ya kulipenda na kuliheshimu kisa jeshi letu limeshindwa kuzuia mabomu yasilipuke tena baada ya kuahidi hivyo kule Mbagala kuu. Hili si jambo la kubeza kabisa watanzania wanalia, wana hofu na wametishika sana. Mabomu, mabomu mabomu! Kila kwenye mdomo wa watanzania! Sio jambo jema ni lazima twende mbele zaidi ya kulipana fidia.



JWTZ wadhamirie kwa dhati hili lisitokee tena, kama ukaguzi wa kambi ulikuwa unafanyika kila mwaka basi sasa uwe kila mwezi, kama ulikuwa kila mwezi sasa uwe kila week, kama kila week sasa uwe kila siku , kama kila siku sasa uwe kila saa NA KAMA UKAGUZI KWENYE MAKAMBI YETU YA JESHI ULIKUWA UNAFANYIKA KILA SAA SASA UFANYIKE KILA DAKIKA AU SEKUNDE.



Watanzania tumefadhaika sana, tumesikitika sana zaidi tumeanza kuliangalia jeshi letu kwa jicho la kuhoji hili si jambo jema hata kidogo ikumbukwe tu kuwa Tanzania ni Yetu, Dar ni Yetu na Hata Jeshi Pia ni Letu.





Nova Kambota mwanaharakati,

Mzumbe University,

Morogoro, Tanzania

0717-709618 au 0766-730256,

novakambota@gmail.com

novadream.blog.com

18 Februaary 2011.

Wednesday, February 16, 2011

ADHA YA MABOMU -GONGO LA MBOTO HADI TEMEKE

 Hapa ni eneo la Temeke Wailes na hawa wametokea eneo la Majowe wakielekea uwanja wa Taifa

 viatu havikuweza kukumbukwa

 Mtangazaji wa EATV akipata mahojiano toka kwa wananchi waliopatwa na mlipuko huo

 Huyu dada aliachiwa mtoto na wakapotezana na mama wa mtoto huyo na hawajuani



 Maandamano yakiendelea kila mtu akitaka kunusuru nafsi yake

hapa kila mtu hajui pakuelekea waliambi
 Eneo la machinjoni polisi Chang`ombe wakielekea kituo cha Chan`gombe



                                          Hivi ndivyo walivyotoka Nyumbani Mama na Mwana

 Tumechoka Sista kila siku sisi tu kwanini hayalipuki Upanga pale kambi ya Jeshi au, Mlalakuwa, yanalipuka kwetu sisi tu  wa hali ya chini kijana huyu akiongea maneno haya na mtangazaji wa EATV akionyesha kachoka
 Wakifunguliwa geti kuu la Uwanja wa Uhuru kwenda kujihifadhi kwa usiku huo
 Meneja wa Uwanja akihakikisha kila kitu kinaenda sawa na watu wakiwa katika hali ya usalama.

Hatujui pa kwenda bora tukae hapa hapa ni pembeni mwa barabara ya Mandela eneo la Petrol Station




Monday, February 14, 2011

KINACHOWAVUTA WANAUME KUPENDA



MWANAMUME anapojikuta anampenda mwanamke humpenda kwa dhati na hali hiyo huwafanya wanaume wengi kujikuta wanapenda kupenda.

Mara nyingi wanaume wamekuwa wakitambuliwa kama jamii ya watu wasiokuwa na hisia zaidi ya kujijali wenyewe linapokuja suala la mapenzi.

Ukweli ni kwamba, tumbo la mwanamume hushituka kama mashine pale anapokuwa katika hatua ya kuwa na uhusiano wa kudumu na mwanamke.

Lakini, bado swali linabaki palepale ni kitu gani kinachoweza kumfanya mwanamume ampende mwanamke kwa moyo wake wote na kutulia naye?

Zaidi ya asilimia 60 ya wanaume huchukulia urafiki kama ni kitu muhimu katika uhusiano, lakini je ni aina gani ya mwanamke ambaye humvutia zaidi mwanamume?

Japokuwa hakuna ubishi kwamba suala la mvuto kwa mwanamume halitabiriki, lakini kuna baadhi ya vitu ambavyo wanaume wengi hupendelea mwanamke anayempenda awe navyo.

Wanaume wengi huvutiwa na mwanamke ambaye ana hisia na kitu kingine zaidi yake, pamoja na kwamba wengi hupenda mwanamke anayewasifia na wenye uangalifu mkubwa, lakini huvutiwa zaidi na wanawake ambao huthamini kazi zao au ndugu zao.

Hali hiyo huwafanya wanaume watambue aina ya mwanamke waliyenaye uzuri wake, malengo yake binafsi, na uhuru wake na kuamua kama huyo ndiye mwanamke wanayetaka kuishi naye maisha yao yote.

Pia wanaume hupenda mwanamke ambaye hatumii muda wake mwingi kumganda, pamoja na kwamba kuna ukweli kuwa wapenzi hupenda kutumia muda wao mwingi pamoja lakini si mara zote hufurahia hali hiyo.

Wanaume hupenda kutumia muda wao wa ziada kwa kukutana na marafiki, kucheza michezo kama vile soka, kamari au kunywa, kutokana na hili kufurahia na kuvutiwa zaidi na mwanamke ambaye anawaelewa na hawabani mara kwa mara.

Wanaume pia huvutiwa na wanawake ambao ni watundu katika nyanja zote, yaani mwanamke ambaye hachoshi, kuanzia tabia yake, ufedhuli au jeuri yake, kujiamini kwake, haiba yake na ucheshi wake ambao unaonesha kuwa anaweza kuwa shujaa kidogo na jasiri wakati huo huo.

Ukweli ni kwamba wanaume wanapenda mwanamke ambaye atawapatia changamoto, ambaye wanaweza kushindana katika mambo mengi ya kimapenzi na kimaendeleo, lakini pia mwanamke ambaye anaweza kuwaongoza wakati mwingine.

Aidha wanaume pia hupenda wanawake ambao watawajali na kuwa nao karibu zaidi kiupendo kuliko hata ule upendo wa mama zao.

Wanawake mkumbuke kuwa, kila uhusiano unaguswa na suala la kupokea na kutoa, na wanaume moja kwa moja watamkimbilia mwanamke ambaye atawaonya pale wanapofanya mambo ya kijinga, atakayewafanya wanaonekane watanashati machoni mwa watu wengine pia atakayewasaidia kutoa maamuzi bila kuwapo kwa tatizo.

Hata hivyo mara nyingi wanaume hupenda kujiona kuwa wanafahamu wanachokifanya na kwamba hawahitaji msaada wowote, lakini wanawake ambao hujitolea kuwalinda na kuwasimamia huwa na nafasi kubwa katika mioyo ya wanaume wengi.

Pamoja na hayo, ikumbukwe kuwa suala la upendo na mapenzi hutegemea zaidi moyo wa mtu, pamoja na sifa hizo bado uchaguzi na uamuzi wa kupenda upo mikononi mwa mhusika.
sheby biboze.wabongousa.blogspot.com

UMEME JANGA LA TAIFA

MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Nishari na Madini, January Makamba, amesema yeye na wajumbe wenzake wa kamati hiyo wamejizatiti kuchukua hatua za haraka za kuishauri na ikibidi kuishinikiza serikali kuchukua hatua za haraka na sahihi za kukabiliana na tatizo kubwa la mgawo wa umeme linalolikabili taifa.

January aliyasema hayo jana jioni wakati alipozungumza kwa simu na Tanzania Daima muda mfupi baada ya kuwaongoza wajumbe wa kamati yake kutembelea bwawa la Mtera ambalo ni moja ya vyanzo muhimu vya uzalishaji wa umeme.

“Wakati tukitambua kwamba kazi ya utekelezaji ni ya serikali, baada ya kutembelea Mtera tumemweleza Waziri (wa Nishati na Madini) bayana kwamba tutaishauri serikali na wakati mwingine tutalazimika kuishinikiza kuchukua hatua sahihi na za haraka za kulimaliza tatizo la umeme ambalo lina athari kubwa kwa maendeleo ya taifa,” alisema January.

Katika kuonyesha namna hali ilivyo mbaya alisema hivi sasa Mtera imebakiza kina cha maji cha mita 1.32 tu kabla ya mitambo kuzimwa kutokana na kina cha maji kupungua.

Alisema hali hiyo ndiyo ambayo inalifanya bwawa hilo ambalo lina uwezo wa kuzalisha megawati 80 za umeme litoe megawati 52 tu kwa sasa wakati taifa likisubiri kudra za Mungu kuifanya mvua inyeshe ili kina cha maji kiongezeke.

Akieleza kile walichokiona Mtera, January alisema wamejifunza kwamba ni jambo la hatari kuendelea kuweka matumaini ya kudumu katika umeme unaozalishwa kwa nguvu ya maji wakati hali ikijulikana bayana kwamba mvua ni za msimu na zisizo za uhakika.

January ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli (CCM), alisema ni jambo lisiloingia akilini kwa taifa kuendelea kuweka matumaini makubwa kwa umeme unaozalishwa na maji yayotokana na kudra za Mwenyezi Mungu za kuleta mvua.

“Leo hii tumekuwa tukiwahimiza wakulima kutumia njia mbadala za kilimo badala ya kuendelea kutegemea mvua iwapo wanataka kupiga hatua. Iweje sisi wenyewe tunaosema hivyo ndiyo tuwe wale wale tunaotaka umeme wetu uwe wa uhakika kwa kutegemea mvua?” alihoji January.

Alisema baada ya kuzungumza na wataalam wa TANESCO wakati wakiwa Mtera, wanajipanga kusafiri hadi Dar es Salaam baada ya vikao vya Bunge kwisha na kukutana nao kujadili kwa kina namna ya kumaliza tatizo la mgawo wa umeme.
Kwa hiyo watu wa Temeke msilalamike hili suala ni la kitaifa zaidi tuombe dua mvua zianze kunyesha huko Mtera.

Wednesday, February 2, 2011

TAMASHA LA MASKAUTI -TEMEKE


Chama cha Maskauti wilaya ya Temeke inawatangazia Tamasha la Maskauti litakakalofanyika kwenye viwanja vya maonyesho ya Sabasaba vilivyopo wilayani Temeke kuanzia tarehe 18/02/2011 hadi tarehe 20/02/2012.

Madhumuni makubwa ya Tamasha hilo ni:-
  1. Kuazimisha siku ya skauti duniani kwa kumbukumbu mwanzilishi wa skauti Sir. Robert Baden Powell.
  2. Kukuza vipaji vya skauti/wanafunzi kwa kufanya mashindano ya michezo mbalimbali ya kunoa akili na ya kuchangamsha mwili.
  3. Kumwandaa kijana kuwa na tabia nzuri inayofaa kwa jamii.
  4. Kuwakaribisha skauti wapya
Ili kijana wetu aweze kushiriki katika tamasha hili la kuelimisha na kukuza vipaji 
wasiliana kwa namba zifuatazo :
  • 0657 202983
  • 0759 364187