Pages

Thursday, January 29, 2015

MAJAMBAZI YAPORA TABATA



Watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wamepora pesa kiasi cha  Tsh. 18 milioni maeneo ya tabata relini dereva alijeruhiwa na risasi ya begani

Tuesday, January 27, 2015

Watoto 4 wa familia moja wafa baada ya kula chakula chenye sumu.

Watoto wanne wa familia moja wakazi wa kijiji cha kibambila wilayani kakonko mkoani kigoma wamefariki dunia na mmoja amelazwa katika kituo cha afya kakonko baada ya kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu .
Mganga  mkuu wa wilaya ya kakonko Dk. Fadhil Seleman  amewataja watoto hao waliofikishwa kituo cha  afya kakonko kuwa ni  Neema Joseph, Jonas Joseph, Majaliwa Joseph, Yusuph Joseph wote wakiwa na umri wa kati ya miaka 11 na 18 walifikishwa hospitalini hapo  wakiwa na hali mbaya na walipoteza maisha wakati wanaendelea kupatiwa huduma na kwamba uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa watu hao wamekula sumu katika ugali.
Akizungumzia tukio hilo baba wa watoto hao Joseph Kajolo ambaye alinusurika katika tukio hilo amesema hajui chanzo cha tukio hilo huku baadhi ya wananchi wa kakonko waliokuwa wakieleza maskitiko yao nakusema  vitendo hivi vimekuwa vikijirudia mara kwa mara katika wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya kakonko Peter Toyima amesema polisi inamshikilia mtu mmoja kuhusiana na tukio hilo huku akiwataka wananchi kuacha vitendo vya kuwekeana sumu.
Chanzo.itv

Saturday, January 24, 2015

Prof.Muhongo ajiuzuru sakata la escrow


Tayari katangaza Kujiuzulu.

Aliyekua Waziri wa Nishati na madini Sospeter Muhongo Amejiuzulu Wadhifa wake wa Uwaziri Katika mkutano wake wa waandishi wa habari alio uitisha hii leo.
Asisitiza yeye ni msafi, mwenye ushahidi wa uchafu wake awasilishe kwenye vyombo vya dola
Mapema leo hii Waziri Muhongo alikuwa ameitisha mkutano na Waandishi wa habari
Kufuatia kuhusishwa na sakata la uchotwaji wa mabilioni ya fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow, Waziri wa Nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo ameamua kumuandikia barua Raisi ya kujiuzulu wadhifa wake.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Profesa Muhongo ameelezea furaha yake ya kupatikana kwa maendeleo ya haraka katika wizara yake kwa kipindi chake akisema kuwa nidhamu na uwajibikaji vilikuwa dira ya maendeleo wizarani hapo.
Profesa Muhongo amekwenda mbali zaidi na kueleza kuwa anaamini kujiuzuru kwake kutaisaidia Serikali na Bunge kutuliza malumbano ya Sakata hilo ambalo linazidi kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Amesema yeye si mwizi na hawezi kuuza utu wake kwa kupewa rushwa ili kuwakandamiza watanzania.
“Nimeamua kujiuzuru kwa dhati kabisa bila kushinikizwa na mtu yeyeote, inaonekana mimi ndiyo nitamaliza mjadala huu wa sakata la Escrow, tuna mambo mengi ya kitaifa yanayotakiwa kujadiliwa lakini watu wamekazana na Escrow, nimemuandikia Rais barua rasmi ya kujiuzuru wadhifa wangu, amesema Profesa Muhongo.
Amesema pamoja na kujiuzuru anatarajia mapema kuzungumza na watanzania ili kuwaeleza ukweli wa sakata la Escrow na kujiuzuru kwake ili kuvunja majungu yanayoendelea kuitesa Tanzania na watu wake.
Amesema yeye amelelewa katika malezi yenye maadili mema na kwamba tokea alipomaliza masomo yake aliaswa kutopokea ama kutotoa rushwa hivyo hawezi akapokea rushwa kwa ajili ya kuutukana utu wa mtanzania hicho ndicho kinachomgharimu.