Pages

Monday, May 23, 2011

WANAFUNZI wa shule ya Sekondari Kigogo ya jijini Dar es Salaam, wameadhimia kuandamana hadi Ikulu kumuona Rais Jakaya Kikwete kwa kupinga uwepo wa nyumba ya kulala wageni iliyokuwandani ya eneo la shule


hiyo Wanafunzi hao ambao mwishoni mwa juma walionekana kufanya fujo shuleni hapo kupinga uwepo wa nyumba hiyo bubu iliyopo katika maeneo ya shule hiyo iondolewe kwa kudai inawachanganya katika masomo yao ya kila siku.

Nyumba hiyo ya kulala wageni ipo pembezoni mwa madarasa ya shule hiyo ya kata ambapo wanafunzi hao wamedai kuchanganywa kutokana na miziki na pilikapilika za watu za kila siku zinazofanywa katika nyumba hiyo jambo ambalo linaenda kinyume na na sheria za haki elimu na kudai kuwapotezea usikivu wawapo darasani ikiwemo na kuwafunza maadili mabovu wawapo shuleni

Hata hivyo wanafunzi hao walishafika ngazi za chini kuripoti tukio hilo lakini imeonekana taratibu za kisheria zinakwenda taratibu na kuonekana watendaji kushindwa kuifungia nyumba hiyo.

Hivyo wanafunzi hao wameadhimia kufanya maandamano ya amani kwenda kwa Rais Kikwete kumweleza kero hiyo ili aweze kuwasaidia.

Wakilalama wanafunzi wamedai “makelele ya wateja wa gesti yanatusumbua wakati wa masomo, mana ni vurugu badala tumsikilize mwalimu wakati mwingine wateja wanagombana vyumbani na kutupigia makelele, mara nyingine mavazi yanayovaliwa na baadhi ya wateja si stahili yanatuletea maadili mabovu.

Kwa kuwa madirisha ya gesti yanatizamana na madirisha ya shule mara nyingine ni rahisi kuona yanayotendeka ndani ya vyumba kwa kuwa madirisha hayana pazia, walilalama wanafunzi hao kwa jazba

Vilevile walilalamikia tabia ya kuona wasichana wenye umri mdogo wakiwa wanaingia na watu wenye rika kubwa mithili ya baba zao ni hali ambayo wanadai kuwaumiza kisaikolojia.

Hata hivyo wanafunzi hao wameadhimia kufika kwenye kituo wanachoshughulikia haki za watoto ili kupata msaada zaidi wa suala hilo

Nyumba hiyo ya kulala wageni ’Gesti bubu’ iliyopo ndani ya eneo la shule hiyo imedaiwa na mmoja wa wahusika kuwa hulipiwa kodi kihalali na imesajiliwa kwa mujibu wa sheria zote za Serikali ya Tanzania kwa jina la The Queen Guest House.

No comments:

Post a Comment