Pages

Sunday, May 29, 2011

KIAMA CHA KWELI OCTOBA 21


Kiama hakikutokea jumamosi mei 21 kwakuwa Mungu aliwaonea huruma watu wake lakini oktoba 21 mwaka huu kiama kitatokea kweli na kuua watu wote ambapo watu wema watapaishwa mbinguni kuonana na Yesu. Baada ya kujichimbia hoteli akiwakimbia watu waliokuwa wakitafuta ukweli kwanini kiama hakikutokea mei 21 kama ilivyotangazwa, Mchungaji Harold Camping amejitokeza na kusema kuwa kiama cha kweli kitakuwa oktoba 21 na dunia yetu hii itaangamizwa miezi mitano baadae.

Mchungaji Camping mwenye umri wa miaka 89 alijitokeza toka machimboni na kutangaza kwenye radio yake ya Family Radio kuwa walikosea mahesabu ya biblia wakati wa kutabiri mwisho wa dunia.

Lakini Camping aliongeza kuwa kiama cha kweli kitatokea mnamo oktoba 21 mwaka huu.

Mchungaji huyo wa California alisema kuwa kutotokea kwa kiama mei 21 kumetokana sana na nguvu za kiroho na wala si nguvu za asili.

Camping aliongeza kuwa Mungu aliwaonea huruma watu kuwaangamiza kwa matetemeko makubwa ya ardhi lakini hiyo oktoba 21 hakutakuwa na huruma ya Mungu na kiama kitatokea kweli.

Akiongea kwa muda wa lisaa limoja na nusu, mchungaji Camping alisema "Hakutakuwa na sababu za kiroho ifikapo oktoba 21, dunia itaangamizwa na itatoweka ndani ya muda mchache".

No comments:

Post a Comment