Pages

Saturday, August 17, 2013

Tiketi ya mchezo wa Yanga na Azam yaleta utata kwenye Mechi ya Ngao ya Jamii.

Tiketi inayohusu mchezo huo inasema mchezo utaanza saa 9:00 jioni wakati Ubao wa matokeo ukisema na kuandika mechi inaanza saa 10:00 jioni. Utata huu utaisha lini??

Wahusika TFF mko wapi kwenye hili? Inakuaje watu wanafanya mambo bila kufuata utaratibu? Ina maana muda wa kuanza mchezo huo ulikuwa haujulikani? Tunaelekea wapi kama vitu hivi vidogo vidogo vinatushinda.!!.

Tiketi inaonyesha Mchezo wa Yanga Sc Vs Azam Fc inaanza saa 9:00 jioni.

Tiketi inaonyesha Mchezo wa Yanga Sc Vs Azam Fc inaanza saa 10:00 jioni. Picha ya hapo juu mechi inaanza saa 9:00 tuelewe lipi sasa?... Poleni mlioathirika na tatizo hilo. TFF kuweni makini na mipangilio yenu......