Pages

Saturday, August 24, 2013

ASHANTI YAKARIBISHWA KWA 5 NA YANGA

Timu ya Yanga S.C ikiwa inapasha misuli moto kabla ya mechi yake na Ashanti United ya Ilala, Dar es Salaam.

Timu ya Ashanti United ikiwa inapasha misuli moto kabla ya mechi yake na Yanga S.C ya Jangwani, Dar es Salaam.

Timu zote mbili Yanga S.C na Ashanti United zikiwa zinasalimia Mashabiki kabla ya kuanza mchezo wao.

Purukushani kwenye mechi baina ya Yanga S.C na Ashanti United watoto wa Ilala. Mechi hiyo Yanga ilishinda goli 5-1. Mwanzo mzuri kwa wana Jangwani.(Picha kwa Hisani ya temeke pamoja).

Wachezaji wa Yanga na Ashanti wakiwa wanasubiri kona ipigwe kwenye lango la Ashanti united, Yanga ilishinda goli 5-1.

Moja ya hatari kwenye mechi hiyo.

Mlinda malngo wa Ashanti United akijaribu kuondosha moja ya hatari zilizoelekezwa langoni kwake na washambuliaji wa Yanga.

Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli walilofunga dhidi ya watoto wa Ilala Ashanti United. Poleni Ashanti ndio soka hilo.

Mabeki wa Yanga wakujaribu kuondosha mpira golini kwao.

Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli walilofunga dhidi ya watoto wa Ilala Ashanti United. Poleni Ashanti ndio soka hilo.

Shabiki wa Ashanti United akijipa moyo kwenye mechi yao na Yanga S.c.

Mlinda Mlango wa Yanga Ally Mushafa "Barthez" akiondoa moja ya hatari zilizoelekezwa kwake na washambuliaji wa Ashanti United.

Mabeki wa Ashanti wakimzuia Haruna Niyonzima wa Yanga kuumiliki mpira. Picha kwa Hisani ya Temeke pamoja.

Kipa wa Ashanti akishangaa bao la Yanga kujipatia goli baina ya timu zao.