Pages

Tuesday, August 6, 2013

HISIA ZA MTOTO WA TEMEKE

Imepita kama miaka miwili hivi toka nione picha iliyobeba taswira ya sura yake humu mtandaoni japo ilikuwa nzuri kuitazama kwa mda mrefu bahati mbaya kwa upande wangu ikawa kinyume na apo niliitazama kwa dakika chache kisha nikafanya kuilike nikaachana nayo wala akilini akiwepo tena kama nimelike ile picha yake na kama ilikuwepo labda nilog in nikiona mtu kalike nami nakumbuka kuwa nilishaipa haki yake ya dole gumba kuwa naikubali. Kwa kuwa humu mtandaoni nilikuwa na mambo mengi sana wala sikuwa na mda wa kumfAtilia kwa sana siku moja niliona alama ya sms upande wa inbox nilipuuzia kwa kuwa nilishazoea sana sms za marafiki nakukubali unakaa pande gani nikawa nazipotezea tu wala sikuwa na hamu na inbox cha ajabu siku hiyo nilikuwa na hamu sana ya kushinda inbox naingia tu ndipo nikakuta sms zake nyingi za salamu, za kuniuliza npo wapi, nikajibu nazoweza kujibu zingine nikawa namjibu navyujua mimi bila kufahanu kuwa namuumiza kwa majibu yangu mabaya mm kwangu niliona kawaida sana japo yeye aikumfanya kukata tamaa ya kuchat na mimi tukawa tunachat sana mpaka nikamzoea kupita nilivyojizoea mwenyewe ikawa nisipomuona fb basi nakosa raha kabisa mawazo mengi upita kichwani kwangu kila jambo namwazia yeye liwe zuri au baya naye kama alijua vile kunipima ninja wa kimarekani kwa mzuzu wa ndevu ili nijue kuwa ni gaidi mkali wa akili na mawazo yangu kwa kuwa mazoea yalizidi sana mwisho wa siku akaniambia story flani za maisha yake ya kimapenzi nilimwulumia sana nikajitaidi kuwa mpole nikamfaliji kwa kila neno zuri nalolijua mimi mpaka akanielewa sana pia akashukuru mm kuwa fungua mpya ya maisha yake katika ushauri ikawa kila jambo analilotaka kulifanya lazima aniambie nimpe ushauri nam sikusita nilipoweza nilitia neno niliposhindwa nikawa namwambia omba Mungu yatakwisha siku zikapita ukaribu wetu ukawa unazidi kusogea zaidi tukapeana namba za simu ili kuzidi kudumisha mawasiliano yetu nami nikatumia mwanya huo kuwa namjulia hali kila sekunde nikiwa sina kazi ya kufanya majibu yake alionyosha kufurahi sana kwa kila nachomwambia akawa anasema "asante Dee kwa kujali" nikamwambia kawaida wangu tu wangu wala usiwaze sana siku zikapita miezi ikasogoea ndipo akaniambia jambo moja anaomba tufanye fb nikamuuliza jambo gani akajibu tuweke relation mimi na yeye nikamwambia nipe mda akangoja mda bahati mbaya haukufika kwa upande wangu kwa kuwa sikupenda kuwa na mwanamke fb nilitaka kuwa huru kwa kila jambo nikajaribu kumwambia siwezi akaumia sana akaniambia "Dee unaniumiza moyo wangu kama unanipenda tuweke reletion" nami sikupenda kumuumiza ila nikaomba aniambie sababu za kutaka kuweka relation na mm tena fb ndipo akajibu "mimi kiukweli nakupenda Dee nimechunguza kimyakimya humu fb nimegundua huna demu coz mademu wengi wanakuogopa wanakuchukuila wewe ni mkolofi mtata sana kumbe haupo hivyo kingine mda mwingi unachat na mm unanifaliji mda wote kama ungekuwa nae nadhan mimi nisingepeta nafasi ya kufalijiwa na kuwa karibu na wewe jua nakupenda usiniumize" baada ya kuona maneno yake niliwaza nikamwambia mpaka tukutane ndipo nitakubali kuweka reletion nae Mungu saidia akaelewa mawasiliano yakawa mazuri zaidi kwa kuwa mm sikuwa na wazo la kuwa nae ndipo nikaaza vituko humu fb alivumilia sana mwisho wa siku akaniambia anajitoa fb amechoka na kudhalilishwa na mm moyoni nilifurah sana nikajua sasa nakuwa huru vizuri huku nikichat nae najifanya majonzi mengi mpaka anionee huruma abaki fb huruma yangu haikusaidia kitu mwisho wa siku akaijitoa na urafiki wetu ukaishia apo. Imepita kama miaka miwili sasa leo npo zangu bar flani hv na mchizi wangu na baadhi ya rafiki zake kuna kasherehe flan kanafanyika sasa ikafika zamu ya kujuana majina utambulisho ukaanza vizuri mpaka kufikia kwangu mchizi wangu aliponitambulisha kuwa huyu rafiki yangu wa fb anaitwa Dee Dion kwa sasa muite Mchungaji ndipo nikashangaa binti aliyekuwa kakaa pembeni yangu akinivuta shati na kuniuliza "Dee unanikumbuka mm?" Nikamtazma lakini sikuweza kumkumbuka ndipo akanisimulia mambo mengi kuwa yeye ndio yule niliyekuwa nikimfaliji fb na akaniomba tuwe wapenzi, kusikia hivyo nikastuka kidogo nikajifanya kama sijasikia vizuri kisha nikaanza kumtazama kwa macho ya wizi uongo dhambi ni mzuri kupita uzuri wenyewe nikaanza kujuta sasa kuwa ubushi mwingine hauna maana kumbe tukaongea mengi sana mwisho akaniambia bado ananipenda kama nikiwa ok nimwambie napia nikiwa simwamini tukapime ngoma tujue akazidi kuniambia yuko ok kuish na mimi kwa mazingira yoyote cha msingi nimpende nimuoe pili yeye kamaliza chuo kikuu anaminsupermarket yake kinondon kama npo ok kesho niende nikapaone. Namtazama huku nawaza mm sasa nina mtu nampenda na huyu anasema ananipenda au nibadili dini nioe wawili wa kwanza nioe nayempenda wa pili nimuoe yeye anayenipenda npo njia panda

Mtoto wa Tmk
Dee Dion