Pages

Friday, November 16, 2012

TEMEKE PAMOJA CLASSIC WEAR YAKUTANISHA WATOTO WA TEMEKE

 
 Waendeshaji wa blog ya TemekePamoja (KC mwenye flana ya kijani na Ramaraldo flana nyeusi uwanja wa ndege wa Mwalimu nyerere D`Salaam)

Huyu ni rafiki yangu toka kitambo sana kabla yeye ajawa KC Mwenye Kijani  na mimi sijawa Raldo .Kwapamoja tumekaa chini na kujipanga katika mikakati ya life ya bongo na nje ya bongo na kwa upande wa bongo tumeanza na duka la nguo kuangalia upepo unaendaje.Watu wetu tegemeeni vitu vingi vitakuja ndani ya temekepamoja si tu biashara ya nguo kuna biashara nyingi zitakazoletwa na temekepamoja.Kwanini tumeamua kuwa temekepamoja na si Darstockhom?Tumefikia makubaliano haya baada ya kuona tunahitaji temeke yetu tujivunie nayo na ndio maana sote kwa pamoja tukaafikiana kutumia Temekepamoja kama kampuni yetu na tumeanza na duka la nguo.Ningependa kuwajulisha wadau  wooote wa darstockholm.blogspot.com haipo kuanzia leo fungua www.temekepamoja.blogspot.com humu utapata picha na matukio ya sweden,bongo na nchi zingine zote kama kawaida kama unataarifa,tangazo,tukio na picha au habari yoyote tutumie kwenye temekepamoja,
     Mwanzo mgumu duka letu tulianza hatua za mwanzo kama hvi.Hapo tukiweka tires
     tukavunja ukuta na kuweka geti kama unavyoona mdau wetu.
     Mtazamo wa nje ukilifungua geti wakati ujenzi unaendelea.
   Hapa imeanza kupatikana taswira ya mlango wa duka na hatua za mwisho.
    Mtazamo kwa nje baada ya robo tatu ya ujenzi kukamilika.
    Kwa ndani mabadiliko yameshaonekana.
   Hapa sasa tayari temeke pamoja classic wear ikazaliwa rasmi.
    Mtazamo wa ndani baada ya kuweka nguo za kutoka china,thailand na turkey mchanganyiko.
    Ukiwa ndani mteja utavuta pumzi vizuri kwa kiyoyozi a.k.a kipupwe huku unachagua nguo.
    Hapa utapata jezi pia za team za uingereza kama Manchester,Arsenal,Chelsea,Liverpool na Manchester city.Tupo katika michakato pia na jezi za Newcastle ili Salum Dau  nae aje kutuunga mkono.
 Kwa wale wapenzi wa team za bongo kubwa kama Simba,Yanga na Azam tunazo jezi za rangi zote.Tunashukuru kwa hili swala la jezi za team za bongo tuliomba kibali kwa team husika na tumeruhusiwa kuuza rakini kwa kununua kutoka kwao wahusika na si uchochoroni karibuni.
Watu wangu wooote wa pande zoote mzigo upo wa kutosha
 Azam kama kawa tumepata kibali kutoka kwao kuuza jezi zao dukani kwetu kama wewe shabiki wa azam karibu temekepamoja classic wear.
 Kwa upande wa snikers,makobazi na kofia vyote vinapatikana hapo karibuni sana .
Kwa wale wa spray na nguo za ndani(boxer)zipo pia ukiingia utakutana nazo sample kwenye kabati hapo.
Soon mzigo mwingine utaingia k.Pia muda si mrefu wateja wetu watakaokuja kununua bidhaa temekepamoja classic wear watawekewa bidhaa zao kwenye mifuko yenye nembo ya temeke pamoja classic wear ndio tupo katika mchakato wa mwisho wakutengeneza nembo kweye mifuko.
Wooote mkaribishwa temekepamoja classic wear tunapatikana karibu kabisa na kona ya temeke sudan kama unakwenda temeke mwisho mtaa wa kwanza kushoto kwako,mtaa mkumba karibu kabisa na Hotel ya Royal Girrafe barabara kubwa ya madaladala.Kwa maelezo zaidi endelea kupitia hapa tutakujuza kila kiingiacho dukani..
Ewe mwenyezi mungu tujaalie kheri kwenye utafutaji wetu kwa baraka zako amen.