Pages

Monday, May 28, 2012

TATIZO LA UMEME KIGAMBONI NA MBAGALA

Hivi karibuni nimekuwa nikipokea malalamiko mengi ya kukatika mara kwa mara kwa umeme katika maeneo ya Kigamboni na Mbagala.

Matatizo haya yanatokana na sababu kuu mbili: Moja, miundombinu ya umeme kuzidiwa na mahitaji na pili, uchakavu wa miundombinu.

Kwa hivi sasa, watumiaji wa umeme wa Kigamboni, Mbagala na Mkuranga wanapata mahitaji toka kwenye kituo kidogo kilichopo Ilala. Umeme unaotoka kwenye kituo hautoshelezi mahitaji ya maeneo yote yaliyotajwa hapo juu. Hali hii imepelekea baadhi ya maeneo kuwa na umeme ndogo na baadhi ya maeneo kukatika hususan nyakati za usiku.

HATUA ZINAZOCHUKULIWA KUTATUA TATIZO HILI
Hatua za muda mrefu:: Tanesco inatarajia kujenga Sub-station kubwa maeneo ya Mbagala ambayo itahudumua maeneo ya Kigamboni na Mbagala. Kazi hii inatarajia kuanza karibuni baada ya kukamilisha zoezi la fidia kwa wananchi waliobaki.

Hatua za muda mfupi: Tanesco inaendelea na ukarabati wa mfumo uliopo ili uweze kuihimili mahitaji ya sasa. Katika wiki hii, Tanesco ilikata umeme tarehe 22, 24 na leo 27 kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni ilikufanya kazi hii. Kwa mujibu wa Tanesco kazi hii inatarajia kukamilika wiki mbili zijazo.

Naomba tuvute subira wakati Tanesco wanalifanyia kazi tatizo la umeme kukatika mara kwa mara.

Ahsanteni.

Dkt. Faustine Ndugulile
Mbunge Kigamboni

DrFaustine.com

No comments:

Post a Comment