Pages

Thursday, May 24, 2012

Miss Kigamboni waanza kujifua

MAZOEZI kwa ajili ya kushiriki shindano la kumsaka malkia wa kitongoji cha Kigamboni
mwaka huu 'Miss Kigamboni City 2012' yameshaanza mapema wiki hii imefahamika.

Shindano hilo limepangwa kufanyika Juni 15 kwenye ukumbi wa Navy Beach ulioko Dar es Salaam.


Akizungumza jana jijini, Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu, alisema kuwa maandalizi ya kinyang'anyiro hicho yanaendelea na warembo tayari wameshaanza mazoezi kwenye

ukumbi wa Break Point ulioko Posta jirani na Club Billicanas.

Alisema, bado milango iko wazi kwa warembo wenye sifa kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini wanakaribishwa kushiriki kuwania taji hilo.


Aliongeza kuwa kampuni yake imejipanga kuhakikisha shindano la mwaka huu linakuwa bora na kuwapata washiriki watakaokwenda kutwaa taji la Kanda ya Temeke na hatimaye taji la taifa la Redd's Miss Tanzania baadaye mwaka huu.


"Kila kitu ni maandalizi, tumejiandaa katika kufanya mchakato wa kupata warembo wenye sifa ili waweze kuiwakilisha vyema Kigamboni katika mashindano ya Kanda," alisema

Somoe.

Aliwataja warembo ambao wameshaanza mazoezi ni Caroline Peter, Theopisther Wenso, Sophia Martime, Amina Aboubakar, Aisha Rajab, Rosemary Peter, Mariam Mbulilo, Julieth Phili na Doreen Kweka.


Warembo hao wanafanya mazoezi chini ya Hawa Ismail ambaye alikuwa mshindi ya shindano la Kanda ya Temeke mwaka 2003.


"Bado tunakaribisha wadau wa sanaa ya urembo kutudhamini shindano hili, tunaamini uwepo wao ndio utafanikisha ubora na hadhi ya shindano letu mwaka huu kama tulivyodhamiria," aliongeza.

No comments:

Post a Comment