Pages

Thursday, May 10, 2012

HAKUNA NIA YA KUONDOA UMASIKINI - A. MILLANGA

Ili jambo lolote lifanikiwe duniani linahitaji mambo matatu: nia, sababu na uwezo.

Katika utelezaji likupungua moja kati ya mambo haya huwa hakuna mafanikio. Lakini jambo kubwa zaidi katika haya ni NIA.

Katika misahafu ya Mwenyezi Mungu na mafunzo ya manabii tunausiwa kwamba kila amali ya mja huanza na nia. Hata wahenga wetu wanasema, “Penye nia pana njia.” Katika nia ndipo zilipo fikra na ubunifu, uwajibikaji na uadilifu, kujitolea na kuthamini utu.

Kwa mnasaba na Tanzania na tatizo kubwa la kuongezeka zaidi kwa umaskini - sababu za kuondoa umaskini zipo; uwezo wa kuondoa umaskini upo; lakini nia ya kisiasa na kiuongozi ya kuondoa umaskini haipo.  Kila mmoja wetu anafahamu fika kwamba kiini cha umaskini wetu si uvivu wa wananchi  kwamba hawataki kufanya kazi kama wengi wa “wataalamu” wenye dhamana wanavyosema.

Kiini ni watawala na watendaji waliojaa ubadhirifu na mabingwa wa ufisadi. Watawala hawa wanadhulumu na kunyonya haki za watu katika taifa letu kwa mori kubwa, motisha kubwa na msukumo kubwa. 


2 comments:

  1. Ninyi Temeke blog waungwana sana, asante kwa ku-link back, ni advantage kwa blogu yako na yangu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante nasi tunafurahi kuona mtu kama wewe unaipitia Blog yetu japo si ya muda mrefu tunashukuru kwa hilo na kama kuna makosa yoyote unayaona ndani ya hii blog tunaomba utuambie ili tusiyarudie yale makosa muda mwingine.

      Delete