Pages

Tuesday, July 12, 2011

Mambo yaiva Redd’s Miss Temeke



WAREMBO wanaowania taji la Redd’s Miss Temeke, leo watatembelea makao makuu ya wadhamini wakuu wa kanda tatu za Dar es Salaam, Kampuni ya Bia Nchini (TBL) ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao ya kumsaka mrithi wa Geneveive Mpangala.

Redd’s Miss Temeke ambayo inatarajiwa kufanyika Jumamosi wiki hii kwenye ukumbi wa TCC Chang’ombe, ina warembo 16 kutoka vitongoji vya Kurasini na Chang'ombe, ambao watapanda jukwaani katika shindano hilo la kwanza katika kanda za Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kampuni ya BMP Promotions inayoandaa shindano hilo, Benny Kisaka alisema ziara hiyo ya leo itakayoanza mchana hadi jioni, warembo hao wataona na kupata maelekezo jinsi ya vinywaji mbalimbali vinavyotengenezwa kiwandani hapo ikiwamo na kinywaji cha Redd's ambacho kimedhamini shindano lao na baadaye jioni watajumuika na uongozi wa kampuni hiyo katika hafla fupi.

Geneveive ambaye pia ni Miss Tanzania mwaka huo, alikuwa mshindi wa Redd’s Miss Temeke mwaka jana alipopata tiketi ya kushiriki Miss Tanzania sanjari na washindi wengine wawili, Anna Daudi na Britney Urassa.

Wanyange wa mwaka huu ni pamoja na Cynthia Kimasha, Elizabeth Boniface, Eunice Mbuya, Husna Twalib, Irene Jackson, Joyce Maweda, Lucia John, Mwajuma Juma, Naifat Ally, Naomi Ngonya, Prisca Stephen, Sasha Seti, Sara Said, Sara Paul na Victoria Mtega.

Mbali ya Geneveive, warembo wengine waliopata kutwaa taji la Miss Tanzania kupitia Temeke ni pamoja na Happiness Magesse (2001) na Sylvia Bahame mwaka 2003.

Pia warembo Jokate Mwegelo aliwahi kutwaa taji la Ubalozi wa Redds huku mwaka 2009, Sia Ndaskoy alishinda taji la Ubalozi wa Utalii.

Mashindano ya Miss Temeke yalianza mwaka 1996, ambapo mshindi alikuwa Asela Magaka.

Warembo wengine waliopata kutwaa taji la Miss Temeke ni pamoja na Miriam Odemba (1997), Khamisa Ahmed (1998) na Ediltrda Kalikawe(1999).

Wengine ni Irene Kiwia (2000), Regina Mosha (2002), Cecylia Assey (2004), Seba Agrey (2005), Queen David (2007), Angela Lubala (2008), Sia Ndaskoy(2009) na Genevive Mpangala anayeshikilia taji hilo.

No comments:

Post a Comment