Pages

Thursday, July 7, 2011

Gazeti la 'udaku' Uingereza kufungwa

Gazeti la kila Jumapili la News of the World la Uingereza lilatoka kwa mara ya mwisho siku ya Jumapili, siku chache baada ya tuhuma nzito kuliandama gazeti hilo.
Mwenyekiti wa kampuni inayomiliki gazeti hilo la News International, James Murdock amesema toleo la Jumapili ndio litakuwa la mwisho.
Gazeti hilo la kila wiki linatuhumiwa kufanya udukuzi wa simu kwa waathirika wa uhalifu, watu mashuhuri na wanasiasa.
Siku ya Alhamisi, polisi wa Uingereza walisema watawatafuta watu wapatao 4,000 ambao wametajwa kufanyiwa udukuzi katika nyaraka ambazo zimepatikana.
Gazeti hilo ambalo linasomwa zaidi nchini Uingereza limekuwa likitoka kwa miaka 168.
News of the World ambalo huuza nakala takriban milioni 2.8 kila wiki, limepata umaarufu kwa kutoa habari motomoto za watu maarufu na kufichua kashfa mbalimbali.
Ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza imesema haihusiki kwa njia yoyote katika uamuzi wa kulifunga gazeti hilo.

Bw Murdoch amesema hakuna matangazo yoyote yatarushwa katika gazeti hilo wiki hii, badala yake nafasi za matangazo zitatolewa kama sadaka, na hata mapato ya gazeti hilo yatatolewa kama msaada.
Kampuni ya News International imegoma kusema lolote kuhusiana na uvumu kuwa huenda gazeti lake la Sun sasa litatoka kila siku hadi Jumapili.

No comments:

Post a Comment