Pages

Tuesday, July 5, 2011

Gaddafi atajiuzulu akihakikishiwa usalama wake


Kanali  Muammar Gaddafi  ameonyesha  ishara  kuwa  anaweza  kung'atuka  kutoka  madarakani.

Kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, anatoa ishara ya kuachia madaraka, lakini kwanza anataka kuhakikishiwa usalama wake na pia mwanawe, Saif al-Islam, aruhusiwe kugombea urais wa nchi hiyo iliyo kwenye vita.

 

Gazeti  moja  la  Urusi  limesema  leo  kuwa  kiongozi  wa  Libya Muammar  Gaddafi  yuko  tayari   kuacha  madaraka , lakini  anataka kupatiwa  uhakika  wa  usalama  wake  likiwanukuu  maafisa  wa  juu wa   Urusi.
Ripoti  hiyo  katika  gazeti  linalosomwa  na  watu  wengi nchini  Urusi  la  Kommersant,  ambalo  hata  hivyo  halikutaja vyanzo  vya  vyake  hivyo, inakuja  siku  moja   baada  ya  harakati za  utafutaji  wa  njia  za  kumaliza vita  nchini  Libya  zikichukua nafasi  kubwa   katika  mazungumzo  baina  ya  Urusi  na  katibu mkuu  wa  NATO Anders  Fogh  Rasmussen  pamoja  na  rais  wa Afrika  kusini Jacob  Zuma.
Kanali Muammar  Gaddafi  anatoa  ishara   kuwa  yuko  tayari kuachia  madaraka   lakini  kwanza  anataka  apate  uhakikisho   wa usalama  wake, gazeti  la  Kommersant  limenukuu  kile  ilichokiita duru  za  ngazi  ya  juu  katika  uongozi  wa  Urusi.
Duru  hizo zimeeleza  katika  ripoti  kuwa   mataifa  mengine, hususan  ikiwa  ni pamoja  na  Ufaransa , ziko  tayari  kutoa  uhakika  huo.
Ripoti  hiyo ya  gazeti  la  Kommersant , pia  imesema  kuwa  Gaddafi  anataka mtoto  wake  Saif al-Islam  aruhusiwe  kugombea   iwapo  yeye atajiondoa  kutoka  madarakani , sharti  ambalo  waasi   huenda wasilikubali.
Serikali  ya  Libya  imesema  jana  Jumatatu  kuwa ilikuwa  katika  mazungumzo  na  viongozi  wa  upinzani, lakini upande  huo  umeshikilia  msimamo  wake  juu   ya  hatima  ya Gaddafi.
Waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Afrika  kusini  Maite Nkoana-Mashabane  alipokutana na  waziri  wa  mambo  ya  kigeni wa  Ujerumani  Guido  Westerwelle  jana amesisitiza  kuwa suluhisho  la kisiasa  ni  muhimu  katika  mzozo  wa  Libya.Mtoto  wa  kanali  Gaddafi , Saif al-Islam ambaye  baba  yake  anataka  aruhusiwe  kugombea urais.Bildunterschrift:   Mtoto wa kanali Gaddafi , Saif al-Islam ambaye baba yake anataka aruhusiwe kugombea urais.
"Wote  tunakubaliana  kuwa  kile  kitakachoisaidia  Libya  ni  suluhisho  la  kisiasa  na  sio  kijeshi.Wakati  nikuzungumza  nanyi  hivi  sasa  rais  Zuma amepewa  mamlaka  na  umoja  wa  Afrika  kujiunga  na  rais Medvedev  katika  mkutano  mjini  Sochi  ambao pia  unaendelea  kuliangalia  suala  hili."
Kiongozi  wa  upinzani  nchini  Libya  anatarajiwa   wakati  huo  huo kufanya  mazungumzo  mjini  Ankara  Uturuki  leo, muda  mfupi  baada ya  nchi  hiyo  kulitambua  baraza  la   taifa  la  mpito  lililoundwa  na waasi  likipambana  na  utawala  wa  kanali  Muammar  Gaddafi, ameeleza  afisa  wa  ngazi  ya  juu  wa  Uturuki.Mwenyekiti  wa  baraza  la  taifa  la  mpito  nchini  Libya

Mahmud  Jibril  alipokutana  na  waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Ujerumani Guido Westerwelle.
Mwenyekiti wa baraza la taifa la mpito nchini Libya Mahmud Jibril alipokutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle
Mahmud Jibril , ambaye  anahusika  na  masuala  ya   mambo  ya kigeni   katika  baraza  hilo  la  taifa ,TCN, lililo  na  makao  yake katika  ngome  ya  waasi  mjini  Benghazi, anatarajiwa  kuwa  na mazungumzo  ya  pande  tatu  na  waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa Uturuki Ahmet Davotoglo  na  mwenzake  kutoka  umoja  wa  falme za  Kiarabu  UAE, Sheikh Abdullah bin Zayed al-Nahayan.
Mazungumzo  hayo  yana  lenga  katika  kutayarisha   mkutano   wa kile  kinachojulikana  kama  kundi  la  kimataifa  linaloshughulikia Libya, unaotarajiwa  kufanyika  Julai 15  hadi  16  mjini  Istanbul.
Wakati  huo  huo  waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Uingereza William Hague  jana  alimsisitizia  rais  wa  halmashauri  ya  umoja wa  Afrika  Jean Ping  kuwa  kundi  hilo  la  mataifa  linajukumu muhimu  katika  kutatua   mzozo  wa  Libya  wakati  walipokutana kwa  mazungumzo  mjini  London.
Uingereza  ni  moja  kati  ya  nchi zilizo  mstari  wa  mbele  katika  kampeni  ya  mashambulizi   ya NATO    dhidi  ya  kiongozi  wa  Libya  Muammar  Gaddafi, lakini operesheni  hizo  hazijaweza  kuvuta  uungwaji  mkono  mkubwa kutoka  mataifa   yanayoizunguka  nchi  hiyo  ya  Afrika  kaskazini.
Dw.

No comments:

Post a Comment