Pages

Sunday, June 5, 2011

AUZA FIGO KUNUNUA iPHONE

 
Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 17 wa nchini China ameiuza figo yake ili aweze kununua simu moja ya iPhone na iPad. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na magazeti ya China, kijana huyo anayeitwa Xiao Zheng alifanyiwa operesheni ya kuliondoa figo lake moja kwenye jimbo la Hunan mwezi aprili mwaka huu.

Pesa alizolipwa kwa kuuza figo lake kijana huyo alinunua simu ya iPhone na kompyuta ndogo ya iPad.

Xiao aliuza figo lake kwa yuan 20,000 ambazo ni sawa na Tsh. milioni 4.5.

"Wakati mtoto wangu aliporudi nyumbani akiwa na kompyuta ya iPad na simu ya iPhone, nilimuuliza amepata wapi pesa za kununulia vitu hivyo, haukupita muda mrefu alitoboa siri kuwa ameliuza figo lake moja, nilihisi kama dunia inatuangukia", alisema mama yake Xiao.

Mama yake Xiao aliripoti polisi lakini hadi sasa hawajafanikiwa kumkamata mfanyabiashara aliyenunua figo yake.

No comments:

Post a Comment