Pages

Wednesday, June 8, 2011

Motema Pembe yamfukuza kazi kocha

Uongozi wa klabu ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo umetangaza kumuachisha kazi kocha wao Mohamed Nashridine Nabi huku wakiwa katika maandalizi na ya mchezo dhidi ya Simba ya Tanzania kwa ya kuwania nafasi ya kushiriki katika raundi ya makundi ya kombe la shirikisho la Africa.
Pembe
DC Motema Pembe

Timu hizo mbili zitakutana katika mchezo wa kwanza wiki ijayo na kurudiana baada ya wiki mbili.
Tangazo hilo limetolewa baada ya viongozi wa klabu hiyo kukutana na kocha.

Motema Pembe kwa sasa imekwenda mjini Goma kucheza mechi za kirafiki za kujiandaa kupambana na Simba. Timu hiyo kwa sasa inafundishwa na aliyekuwa kocha msaidizi Andy Fulila.
Uongozi wa DC Motema Pembe umesema umemuachisha kazi kocha huyo raia wa Ubelgiji, kwa sababu alishindwa kufanya kazi na wasaidizi wake, na pia kushindwa kufanya vyema katika ligi ya nyumbani.
Motema Pembe ilifungwa na Ndo Mbosco ya Lubumbashi na TP Elima ya Matadi, kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Kocha Nabi ameviambia vyombo vya habari hapa Kinshasa kuwa klabu haijamlipa mshahara wake katika kipindi ambacho walikuwa wakijadili suala lake. Amesema amesikitishwa na uongozi wa klabu hiyo, kwa kuwa alikuwa na mipango mizuri ya kuiongoza klabu hiyo hadi fainali ya Kombe la Shirikisho.
Mchezo wa kwanza kati ya DC Motema Pembe na Simba utachezwa jijini Dar Es Salaam, Tanzania.

No comments:

Post a Comment