Pages

Friday, June 10, 2011

Ngozi ya chura kuponya saratani

Wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Belfast wamejishindia tuzo kwa kazi waliyoifanya kuhusiana na ngozi ya chura ambayo wamegundua inaweza kutibu zaidi ya maradhi makuu 70.
Ngozi ya Chura
kupoza saratani
Watafiti hao walipokea tuzo yao kwenye sherehe iliyoandaliwa na Tuzo ya ubunifu kutoka taasisi ijulikanayo kama Medical Futures Innovation mjini London.
Wataalamu hao wakiongozwa na Profesa Chris Shaw wa taasisi ya Famacia ya Queens, wamegundua proteni mbili ambazo zinaweza kurekebisha kukuwa kwa mishipa ya damu.
Waligundua kuwa proteni kutoka aina ya chura ajulikanaye kwa jina la kitaalamu 'waxy monkey frog' hubana kukuwa kwa mishipa inayosambaza damu mwilini na inaweza kutumiwa kuua uvimbe unaotokana na saratani.
Profesa Shaw alisema kuwa mara nyingi uvimbe huo huweza kuchochewa kufikia kiwango fulani kabla ya kuhitaji damu zaidi ili kupevuka kuwa kivimbe ambacho husaidia kupitisha hewa ya oksijeni na lishe.
Kwa hiyo akaongezea kusema '' Ili kusitisha kukuwa kwa mishipa hii isikuwe hadi kuvimba kutafanya saratani isienee na hatimaye kuiondoa mwilini kabisa.
Hili lina uwezekano mkubwa wa kuifanya saratani yawe maradhi yasiyo uwa ila ya kuishi nayo.
Kundi hilo liligundua pia kuwa aina ya chura mkubwa ajulikanaye kama ''firebellied toad'' huzalisha proteni inayoweza kuchagiza mishipa kukuwa na inaweza kusaidia katika kutibu majeraha ya mgonjwa yapone kwa haraka zaidi.

No comments:

Post a Comment