Pages

Friday, June 10, 2011

WANAUME MARUFUKU KUUZA NGUOZA NDANI ZA KIKE SAUDIA ARABIA

Ili kuondoa kero za wanaume kwenye maduka ya viwalo vya ndani vya wanawake, mfalme Abdullah wa Saudi Arabia amepiga marufuku wanaume kufanya kazi kwenye maduka ya kuuza nguo za ndani za kike nchini humo. Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia aliamua kuchukua uamuzi huo ili kuondoa kero wanazopata wanawake wanapoenda kununua viwalo vya ndani ambapo wamekuwa wakisumbuliwa na wanaume.

Kero hizo huwa kubwa zaidi pale mwanamke anapokuwa hajui saizi ya kiwalo ambayo itamkaa vyema hivyo kulazimika kukubali wauzaji wanaume kuwapima ukubwa wa maumbile yao kama vile kiuno, urefu na kadhalika.

Akitoa uamuzi huo, Mfalme Abdullah alisema kuwa ni marufuku kuanzia sasa wanaume kufanya kazi kwenye maduka yoyote yanayouza nguo za kike na kazi zote kwenye maduka hayo zitakuwa zikifanywa na wanawake.

Uamuzi huo wa Mfalme Abdullah umeshangiliwa na wanawake ambapo inasemekana utasaidia kupunguza idadi ya wanawake wasio na kazi nchini humo.

Takribani asilimia 30 ya wanawake nchini Saudi Arabia hawana kazi na uamuzi huo wa mfalme Abdullah utasaidia kuwapa kazi wanawake wapatao 6,000.

Mwezi februari mwaka jana wanaharakati wa kutetea haki za wanawake nchini humo walianzisha kampeni ya kuwataka wanawake wasiingie kwenye maduka ya viwalo vya kike ambayo wauzaji wake ni wanaume.

Wanaharakati hao walisema kuwa ni kinyume cha mafundisho ya dini ya kiislamu kwa mwanamke kumpa vipimo vya maumbile yake mwanaume ambaye si mume wake wala ndugu yake. Wasomi wa dini ya kiislamu waliunga mkono harakati hizo za wanawake.

No comments:

Post a Comment