Pages

Friday, June 24, 2011

TALAKA KWA KUTOJIBIWA SIMU

KIJANA aliyefahamika kwa jina la Riziki amejikuta akimpa talaka mke wake baada ya kukerwa na kutopata majibu kutoka kwa mke wake wakati alipokuwa akimpigia simu 

Hata hivyo Riziki alifikishwa Mahakamani baada ya kumjeruhi mke wake huyo na kumsababishia maumivu.

Imedaiwa katika mahakama ya mwanzo Temeke kuwa mshitakiwa huyo alifunguliwa mashitaka hayo na mke wake baada ya kumjeruhi kwa kumpa kichapo cha nguvu mke wake huyo kutokana na hasira za kutojibiwa kwa simu yake.

Imedaiwa kuwa, mshitakiwa huyo June 12 mwaka huu, akiwa nyumbani kwake Tandika alimpa kichapo mke wake aliyetambulika kwa jina la Fatma Hamisi [29] baada ya kumuudhi kwa kutopokea simu wakati alipokuwa akimpigia.

Mshitakiwa huyo alikana shtaka hilo na kuwa nje kwa dhamana na kesi hiyo itasikilizwa mahakamani tena baada ya wiki tatu .

Awali imedaiwa kuwa, Fatma alipigiwa simu na mume wake huyo na hakuweza kupokea kwa kile kilichodaiwa ni ugumu wa mazingira aliokuwa nao wakati simu hiyo ikipigwa ambapo alidai alikuwa kwenye kikao cha familia eneo la Mbagala.

Hivyo kutokana na kukerwa na tabia hiyo Fatma aliporudi nyumbani majira ya usiku Riziki alianza kumporomoshea matusi na hakuridhika alimpa kichapo kwa kudhani mke wake alikuwa na mwanaume mwingine wa nje ya ndoa

Hivyo kutokana na kipigo hicho alichopata kutoka kwa mume huyo na tuhuma aliyopewa na mume wake ,Fatma alikwenda kuripoti tukio hilo nyumbani kwao hali iliyopelekea Riziki kufikishwa polisi.

Hata hivyo mume huyo inadaiwa kuwa alikuwa na wivu wa kupindukia na hata alipothibitishiwa na baadhi ya ndugu kuwa walikuwa wote na Fatma mume huyo alimpa talaka moja mke wake kutokana na hasira.

No comments:

Post a Comment