Pages

Wednesday, June 29, 2011

VILLAS BOAS AMPA NAFASI DI MATEO KUWA MSAIDIZI

Robert Di Mateo akitambulishwa na Villas Boas

Watakaoiwezesha ni: kutoka kushoto, Jose Mario Rocha, Roberto Di Matteo, Andre Villas-Boas, Steve Holland and Daniel Sousa wakiwa katika uwanja wa Stamford Bridge.

Andre Villa-Boaz amekiri kuwa yupo katika wakati mgumu katika kushinda mataji tofauti akiwa kama kocha mpya aliyetangazwa na chelsea.

Na Villa-Boaz alimteua Meneja wa zamani wa west brom Robert Di-Mateo kuwa Msaidizi wake, najua Roman anataka mafanikio na ya haraka alisema Villa Boaz

MDEE AKUMBUISHIA DECI

Mbunge wa Kawe Halima Mdee, CHADEMA, aliyeuliza leo Bungeni swali la msingi kuhusu Development Entrepreneurship for Community Initiative, DECI, na maswali ya nyongeza, amempa wakati mgumu Naibu Waziri wa Fedha, Gregory Teu, wakati alipotakiwa aeleze hatua zilizochukuliwa na Serikali kuhusu maofisa wa DECI walioshindwa kutekeleza wajibu wao hadi DECI ikafanya shughuli zake kinyume cha sheria.

Katika maswalic yla nyongeza, Mdee alisema, DECI ilifanya shughuli zake kwa miaka mitatu za kuchukua amana za wananchi bila kuwa na kibali cha kufanya hivyo, je, “Serikali inatoa kauli gani juu ya maafisa wake ambao walikuwa wanajua suala hilo lakini hawakuchukua hatua zozote?" na "kwa kuwa fedha zinazoshikiliwa ni za wanachama na waliofanya uhalifu huo ni watu watano, na kwa vile thamani ya fedha inashuka kwa nini wanachama ambao hawakuwahi kuvuna hata mara moja wasikabidhiwe fedha hizo?"

Ndipo Teu aliposema, “Fedha zinazodaiwa na wanachama ni nyingi wakati fedha zilizoko kwenye akaunti za wakurugenzi ni kidogo.”

Baada ya kujibu hivyo alienda kukaa, ndipo Spika akamkumbusha kuwa hajajibu sehemu nyingine ya swali kuwa maofisa wa Serikali ambao walizembea hadi DECI wakaendesha shughuli zao kinyume cha sheria wamechukuliwa hatua gani?

Teu akarudi kwenye eneo la kujibia mwaswali na kusema “Nafikiri walikuwa bado hawajaandikishwa,” kauli iliyosababisha Wabunge wengine kuangua kicheko.

Awali akijibu swali la msingi la Mdee, Teu alisema Serikali haijachukua fedha za DECI bali fedha hizo, Shilingi bilioni 14.81 zimezuiliwa katika akaunti zilizomilikiwa na wakurugenzi wa DECI katika benki mbalimbali nchini.

Katika swali lake, Mdee alitaka kufahamu hatma ya fedha za wananchi. Alisema fedha hizo ni asilimia 37.77 ya ambazo zinadaiwa na wanachama wa DECI ambazo ni Shilingi bilioni 39.3/=, na uamuzi wa kuzizuia uliotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikiwa ni hatua mojawapo ya uchunguzi dhidi ya Deci ambayo ilikuwa inaendesha mchezo wa upatu.

“Napenda kuliarifu Bunge lako kuwa kesi ya DECI iliyofunguliwa mwaka juzi katika mahakama ya Kisutu inaendelea kusikilizwa,” alisema Teu na kuongeza, “Hivyo hatma ya fedha hizo za wananchi itategemea hatma ya kesi hiyo kwani Deci ilikuwa na matawi 40 katika mikoa 18 ya Tanzania Bara”.

Alisema, usikilizwaji wa mashahidi wa Dar es Salaam umekamilika na hatua za kuwapata mashahidi kutoka mikoa mingine zimeanza. Alisema, DECI ilikuwa na wanachama 649,859 na sehemu ya wanachama hao watahitajika kutoa ushahidi mahakamani.

Anayetuhumiwa kutapeli mil. 218/- za magari anatafutwa

POLISI Mkoa wa Temeke, inamtafuta Mtanzania anayeishi nchini Japan, Hassan Omary (30) kwa tuhuma za utapeli wa zaidi ya Sh. milioni 218 na kutoroka mara baada ya kuachiwa kwa dhamana.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, David Misime aliliambia gazeti hili jana kuwa, Omary anayejishughulisha na biashara nchini Japan, anatuhumiwa kuwatapeli Watanzania baada ya kuwaahidi kuwa angewaletea magari.

Kwa mujibu wa Misime, awali Omary alikamatwa Juni 23, mwaka huu Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam wakati akijiandaa kurudi Japan.

Kamanda Misime amesema, Omary alipelekwa katika kituo kidogo cha Polisi uwanjani hapo na baadaye alihamishiwa kituo cha Polisi Chang’ombe wilayani Temeke.

“Usiku huo alishikiliwa hapa na kuhojiwa kuhusu tuhuma hizo na aliachiwa kwa dhamana kwa masharti ya kutakiwa kurudi siku inayofuata kuendelea na mahojiano na utaratibu mwingine wa kisheria,” amesema Misime.

Kamanda Misime amesema, cha kushangaza siku iliyofuata, mshitakiwa huyo hakufika kituoni hapo na baadaye walipata taarifa kuwa ametoroka nchini.

Hata hivyo Kamanda huyo amesema, suala la kutoroka nchini halina ukweli wowote na ana uhakika kuwa mtuhumiwa huyo bado yupo nchini.

“Tunaendelea kumtafuta na hata kama kweli atakuwa ametoroka, tutatumia njia zingine kumpata ikiwemo askari wa Interpol (Shirika la Kimataifa la Polisi), ili aje kujibu tuhuma za utapeli zinazomkabili na za kutoroka dhamana yake,” ameongeza Misime.

Omary anatuhumiwa kutapeli kiasi hicho cha fedha kwa walalamikaji wawili waliotambulika kwa jina moja moja la Titus na Philemon kwa kuwadanganya kwamba angewaletea magari na matrekta.

Kamanda Misime amesema, mshitakiwa atakapokamatwa, wataangalia afunguliwe kesi ya aina gani; ya madai au jinai na kuongeza kuwa tayari wameweka mitego sehemu mbalimbali ili kumkamata.
habari leo

SIMBA YAIFUNGA OCEAN VIEW 1-0




SIMBA imezinduka na kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Zanzibar Ocean View katika mechi ya michuano ya Kombe la Kagame iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Amir Maftah aliipatia Simba bao hilo la ushindi katika dakika ya 22 kwa shuti kali la umbali wa mita 28 na mpira kujaa wavuni moja kwa moja.

Bao hilo la Maftah lilikuwa ni kama kusawazisha makosa yake baada ya kukosa bao la
penati katika dakika ya nane ya mchezo huo.

Penati ilitolewa na mwamuzi Sylvester Kirwa wa Kenya baada ya Mussa Hassan Mgosi kuangushwa eneo la hatari na mlinzi mmoja wa Ocean View.

Ushindi huo kwa Simba ni ahueni kwao na mashabiki wao baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mechi ya kwanza dhidi ya Vital ‘O’.

Katika mechi hiyo ya jana, Simba ilitawala zaidi kipindi cha kwanza, ambapo Athumani Iddi
‘Chuji’ anayeichezea Simba kwa mara ya kwanza tangu ajiunge nayo akitokea Yanga kutokana na kuzomewa na mashabiki wa Yanga.

Chuji alibadilishwa dakika ya 58 na nafasi yake kuchukuliwa na Mohamed Banka. Kipindi cha pili Simba ilianza mchezo kwa kasi na kukosa mabao kadhaa.

Katika dakika ya 45, Haruna Moshi Boban alichelewa kuunganisha krosi ya Mgosi na kukosa bao la wazi.

Ocean View pamoja na kushindwa kuhimili mikikimikiki ya Simba, walipata nafasi chache za kufunga, dakika ya 20, mabeki wa Simba walijichanganya lakini Walulya Derrick alirekebisha makosa na kuokoa.

Matokeo hayo yameifanya Simba ifikishe pointi nne nyuma ya Ocean View inayoongoza
kundi kwa kuwa na pointi sita.

Simba sasa inahitaji ushindi katika mechi zilizosalia ili ifike hatua ya robo fainali.
Akizungumzia mechi hiyo, Kocha wa Ocean View, Abdulfatah Abbas alimlalamikia mwamuzi
kuwa aliipendelea Simba.

Michuano hiyo inaendelea tena leo ambapo mabingwa soka Tanzania Bara, Yanga watashuka
dimbani kumenyana na Elman ya Somalia.

Yanga inahitaji ushindi katika mechi hiyo ili kufufua matumaini ya kucheza robo fainali baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na El Merreikh ya Sudan katika mechi ya kwanza.

Tuesday, June 28, 2011

BEI YA PETROL YASHUSHWA

WAMILIKI wa vyombo vya usafiri vya moto kuanzia keshokutwa watajisikia afueni baada ya utekelezaji wa mabadiliko ya bei ya nishati ya mafuta kuanza.

Hatua hiyo inatokana na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na Majini (Ewura) jana kutangaza kushuka kwa bei ya mafuta jamii ya petroli na dizeli.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu, kuanzia siku hiyo, bei ya dizeli itapungua kwa Sh 215 kwa lita huku ya petroli ikisubiri nayo kushuka kwa kiwango ambacho hakikutangazwa jana.

Lakini wakati hali ni hiyo kwa mafuta hayo,ya taa yatapanda kwa Sh 385, ambapo Masebu aliongeza kuwa, ifikapo Agosti Mosi bei ya mafuta hayo inatarajiwa kushuka zaidi ili kutoa nafuu kwa mtumiaji.

Masebu, alisema hayo Dar es Salaam jana katika mkutano wa wadau wa mafuta na kutaka bei hizo mpya zifuatwe na kuheshimiwa.

Alisema, pia bei ya petroli itapungua na kiwango chake kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa baada ya kukamilika ukokotoaji wa tozo zilizopunguzwa, huku akionya kuchukua hatua za kisheria kwa watakaokiuka agizo hilo la kushusha bei.

“Lengo la mkutano wa leo (jana) ni kuwaeleza wadau wa mafuta kuhusu mambo yaliyotokea Dodoma, ambayo yamesababisha sisi Ewura kama wadhibiti, kuwatangazia kuwa kutokana na punguzo la kodi katika mafuta na nyongeza katika mafuta ya taa, bei mpya ya bidhaa hizo itaanza rasmi Julai mosi,” alisema Masebu.

Alisema, kwa sasa kinachosubiriwa ni kusainiwa kwa Sheria ya Fedha yenye makubaliano hayo yaliyopitishwa na Bunge.

Kutokana na mabadiliko hayo, Masebu alisema, tofauti ya bei ya dizeli na mafuta ya taa itakuwa Sh. 15 kwa lita, kwa maana ya mafuta ya taa kuuzwa kwa bei ya chini ya dizeli kwa kiwango hicho ili kuzuia uchakachuaji.

Bei ya zamani ya bidhaa hizo mbili kwa mujibu wa Masebu, mafuta ya taa yaliuzwa kwa bei nafuu pungufu ya Sh. 400 ikilinganishwa na ya dizeli na kusababisha baadhi ya mafuta yaliyokuwa yakiuzwa nchini kuchakachuliwa.

Alisema, pia upo mchakato wa kukokotoa tozo zingine kwa ajili ya kuzipunguza, ili kuifanya bei ya mafuta hayo jamii ya petroli kuwa nafuu zaidi na Agosti mosi, punguzo kubwa linatarajiwa kuanza rasmi kutumika.

Akizungumzia mfumo wa kuweka vinasaba katika mafuta, Masebu alisema, umepitishwa rasmi kutekelezwa nchini ili kudhibiti wafanyabiashara wadanganyifu wanaosingizia kusafirisha mafuta nje ya nchi na baadaye kuyauza nchini ili kukwepa kodi.

“Tumeamua kuwataarifu kuwa mfumo huu wa ‘fuel marking’ tunaendelea nao na tangu uanze, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeongeza mapato yake kutokana na magari mengi kukamatwa, yakifanya udanganyifu na kupigwa faini,” alisema.

Pia mfumo huo umesaidia TRA kupata mapato yaliyokuwa yakivujishwa kwa kukwepa kodi.

Kuhusu mfumo wa uingizaji mafuta kwa pamoja, Masebu alisema, Serikali imekamilisha michakato yote ikiwa ni pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kusaini kanuni za mfumo huo na kuzichapisha katika Gazeti la Serikali toleo namba GN 164 la Juni 3.

Kanuni hizo kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, zimetoa wajibu mkubwa kwa wadau wa mafuta zikiwamo taasisi na kampuni za mafuta, ambazo zimetakiwa kuunda Kamati ya Uratibu na Bodi ya Wakurugenzi, katika miezi mitatu ijayo, ili mfumo huo uanze kutekelezwa.

Alisema, vyombo hivyo viwili pamoja na Ewura kuwa msimamizi na mdhibiti, vitasimamia masuala ya zabuni.

“Mfumo huu tunatarajia utasaidia kupunguza gharama kubwa za mafuta, kwa kuwa utashindanisha kampuni za mafuta na hivyo bei itapungua, suala hili sasa si hadithi, bali ndiyo ukweli wenyewe,” alisema.

Wakati akiwasilisha Bajeti ya mwaka wa fedha 2011/2012 Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, alisema, katika jitihada za Serikali za kupunguzia mzigo wa gharama za maisha wananchi, imeamua kupunguza baadhi ya kodi za mafuta ili bei ya bidhaa hiyo ipungue.

Akiwasilisha muswada wa Sheria ya Fedha kwa mwaka 2011, Naibu Waziri wa Fedha, Pereira Silima, alisema Serikali imeongeza ushuru wa bidhaa kwa mafuta ya taa kutoka Sh. 52 hadi Sh 400.30 pamoja na mambo mengine, lengo ni kudhibiti uchakachuaji wa mafuta nchini.

Upunguzaji huo wa bei za mafuta, pia una lengo la kudhibiti mfumuko wa bei, ambao umekuwa ukisababishwa na bidhaa hizo kutokana na umuhimu wake katika bidhaa na huduma za kijamii.

MAONYESHO YA SABASABA YAANZA

Maonyesho ya 35 ya Kimataifa ya Biashara (Tan Trade) sabasaba yameanza leo jijini Dar es Salaam na zaidi ya nch 16 zimeshiriki kushiriki maonyesho hayo.Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Ramadhani Khalfan, amesema maoonyesho hayo yamekuja na tofauti kubwa ambapo amesema viingilio havitabadilika tofauti na miaka ya nyuma

Pia amesema mabadiliko mengidne ni kuweza kuchapisha tiketi za viingilio nje ya nchi ili kudhibiti uharifu wa mapato katika maonyesho hayo

Amesema nchi 17, mashirika binafsi kutoka nchi 28, kampuni zipatazo 300 za nje ya nchi na kampuni zipatazo 1,500 za ndani ya nchi zimethibitisha kushiriki maonyesho hayo

Mabadiliko mengine aliyoainisha ni kupigwa marufuku maonyesho ya muziki ndani ya viwanja hivyo ili kutoa fursa kwa wananchi kupata maelezo mazuri katika mabanda bila kuathiriwa na kelele ya muziki kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Kilele cha maonyesho hayo yanatarajiwa kuwa Julai 7 mwaka huu

BARABARA YA VUMBI TOSHA SERENGETI

Mipango iliyojaa utata ya kujenga barabara ya lami katikati ya mbuga ya wanyama ya Serengeti na sasa baada ya ubishi na kuonywa kuwa mpango huo utaathiri mazingira na nyenzo za wanyama pori.
Ajabu ya dunia Serengeti
Thamani ya mazingira ni kubwa
Serikali ya Tanzania ilipanga barabara mbili yaani ya kutoka na inayoelekea kupitia mbuga hiyo kutoka ukingo wa Ziwa Victoria na pwani.
Lakini utafiti uliofanywa umeonyesha kuwa mpango huo utaathiri vikali hali ya wanyama kama vile nyumbu na punda milia, ambao misafara yao ya kuhama, jambo ambalo linaangaliwa kama maajabu ya maumbile Duniani.
Serikali sasa imethibitisha kuwa barabara hiyo haitoguswa na itabaki kuwa ya vumbi.
Katika barua kwa Kituo kinachoshughulikia Hifadhi ya Mazingira Duniani mjini Paris, Idara ya mali asili na Utalii nchini Tanzania imesema kuwa sehemu ya barabara hiyo yenye umbali wa kilomita 50 itaendelea kusimamiwa kwa ajili tu ya utalii na utawala.
Serikali kwa sasa inatathmini njia nyingine ingawa itakuwa ndefu kuweza kuwafikishia wananchi wake huduma kupitia kusini mwa mbuga hiyo ya wanyama.
Barabara hiyo itaepuka maeneo yenye thamani ya kuhifadhi mazingira na athari zinazoweza kufuata.
Nyumbu wa Serengeti
Serengeti
Mwaka jana, kundi la wataalamu walionya kua barabara iliyopendekezwa kupitia mbuga ya wanyama inaweza kupunguza idadi ya Nyumbu wanaokadiriwa kuwa milioni 1.3 kufikia 300,000.
Athari kwa wanyama pori, wataalamu hao walionya kuwa Uchumi utaathirika mno kutokana na kupungua kwa wanyama hao.
Wataalamu hao waliitaja mbuga ya wanyama ya Serengeti kama mfano wa kipekee wa hifadhi ya wanyama wanaohamahama.
Safari ya kuhama hama kwa wanyama hao kila mwaka hushiriki takriban wanyama milioni 1.5, wakiwemo nyumbu na punda milia.
Wakati wanyama hao wakisafiri, huacha vinyesi ardhini, ambavyo husaidia kurutubisha mimea, huku nyayo zao zikizuwia ukuaji wa kupindukia wa nyasi.
Mabadiliko ya aina yoyote katika hali kama hiyo, wataalamu hao wamesema kwenye ripoti yao kwa serikali ya Tanzania, yatasababisha kupungua kwa wanyama wanaotegemea nyumbu na punda milia kama chakula chao kama simba,chui na duma.
Simba watatoweka
Simba
Hawa ni baadhi ya wanyama wanaovutia mno watalii.
Halikdhalika wataalamu hao wameonya kuwa barabara hiyo ingeweza kusababisha kubadilika kwa mimea na vilevile kusafirisha aina mbalimbali za magonjwa yasiyokuemo ndani ya mbuga.
BBC

SENEGAL WAANDAMANA KUPINGA MGAO WA UMEME

Maandamano yamezuka katika mji mkuu wa Senegal, Dakar na katika jiji la kusini la Mbour kutokana na ukosefu wa umeme. Jijini Dakar, majengo kadhaa ya serikali yalichomwa moto, zikiwemo ofisi za shirika la umeme la serikali - Senelec.
Dakar
Maandamano Dakar
Majeshi ya usalama katika mji wa Mbour yalipiga mabomu ya machozi kutawanya maelfu ya waandamanaji.
Tatizo la ukataji umeme, ambao umedumu kwa saa 48 katika maeneo kadhaa, limekuja wiki moja tu baada ya kutokea maandamano dhidi ya rais.
"Mamia ya vijana walivamia ofisi za Senelec na kuzichoma moto," amesema mkazi mmmoja wa Dakar, Ismail Diop akikaririwa na Reuters.
Chupa zilizovunjwa, mabaki ya majengo na matairi yaliyochomwa moto vimetapakaa mitaani, amesema mkazi huyo.

Miaka mingi

Mjini Mbour, karibu kilomita 80 kusini mashariki mwa Dakar, ofisi za shirika la umeme pia zilishambuliwa. watu walioshuhudia walisema ofisi za Senelec zilivunjwa na magari yaliyoegeshwa nje kushambuliwa pia.
Senelec imeshindwa kutoa huduma ya umeme ya kuridhisha kwa miaka mingi.
Wiki iliyopita, kulikuwa na maandamano mjini Dakar, yaliyotokana na pendekezo la rais Abdoulaye Wade kutaka kubadilisha katiba.
Maandamano hayo yalikuwa ya kiwango ambacho hakijawahi kuonekana katika kipindi cha miaka 11 ya utawala wa Bw Wade.

Gharama za maisha

Rais huyo alitaka kupunguza kiwango cha asilimia kinachohitajia kushinda urais kutoka asilimia 50 hadi 25 ili kuepuka duru ya pili katika uchaguzi.
Wakosoaji wamesema marekebisho hayo ya katiba yamelenga kuhakikisha Rais Wade, ambaye ana umri wa miaka 85, anachaguliwa tena mwakani.
Bw Wade alingia madarakani katika uchaguzi wa kidemokrasia, lakini sasa anakabiliwa na ongezeko la hasira kutoka kwa wananchi kutokana na matatizo ya umeme ya kila siku na kupanda kwa gharama za maisha.

Monday, June 27, 2011

NDONDO: FOMBA YAIFUNGA TITANIC

Mchezo ukiendelea kati ya Fomba Fc na Titanic
Vinafanyika vitu sehemu nyingine huwezi kuvipata kiukweli kabisa Uswazi very talented nimeweka msisitizo kidogo, watoto wa uswahilini ndio mambo yote
Kikosi cha Fomba Fc
Mashabiki wa Fomba wakisherehea ushindi baada ya kuifunga Titanic 1-0
Fomba Fc Pamoja

Kombe lililoanzishwa Maeneo ya Temeke kata 14 na limejaribu kuchukua kata mbalimbali kutoka wilayani humo,  mashindano yanafanyika katika viwanja vya Temeke Boyz vilivyopo Shule ya Msingi Temeke na Muungano hamasa imekuwa kubwa mno kwa wakazi wa maeneo hayo na nje ya maeneo hayo dhumuni ni kujaribu kuendeleza Mchezo wa soka kwa wilaya ya Temeke, na katika mchezo uliochezwa leo Fomba Fc imewafunga Titanic 1-0 goli lilifungwa na Haji Harambe

CHANDIMU

Ni mpira wa Miguu ambao kuna umri wa utoto lazima ucheze usipocheza utoto wako haujakamilika  hii haina kanuni kila mtoto anaonyesha uwezo wake wa kucheza soka hii nimeikuta Kati ya mtaa Rusende na  Miteja zamani garden
Hata ikipatikana mita 10 mpira huwa unachezeka

Mpira ukiendelea kuchezwa

MITAA YETU

Barabara ya Mtaa Sungwi kati ya Hospital ya Temeke na ofisi za Wilaya kuu CCM

Barabara ya Temeke kuelekea Polisi Chang`ombe

Barabara ya Temeke Kuelekea Temeke Hospital
Mahakama ya Mwanzo Temeke

Barabara Ya Evereth

Maeneo ya Polisi chan`ombe

Mtaa wa Miteja uliopo Temeke kata ya 14

Mtaa wa Ndalala Kuelekea Kituo cha mabasi Polisi chang`ombe

Mtaa wa Ndalala kuelekea Msikiti mkubwa wa Tungi

Msikiti wa Tungi unavyoonekana kwa mbali maeneo ya temeke kata ya 14

Ungependa kujua Baadhi ya Mitaa ya Temeke ilivyo na mazingira yake yalivyo unaweza unaweza kututumia sehemu ambayo unataka uijue ikoje kwa E-mail ifuatayo:-temekepamoja@gmail.com  

EXCEL BAND WAANZA MAONYESHO

Baadhi ya Wanamuziki wanaoounda kundi la Excel One Band

Mbile Muhango Kiongozi wa Band ya Excel One Band

Kundi la Muziki la Bendi ya dance Excel One Band wamenza rasmi kufanya maonyesho mbalimbali katika kumbi tofauti hapa Dar es Salaam, akizungumza kiongozi wa Kundi hilo Mbile Muhango, amesema kundi lake kwa sasa linafanya maonyesho katika Ukumbi wa Swizz Pub uliopo Tabata na Polisi Ufundi (Balax) uliopo barabara ya Kilwa Temeke
Mbile Muhango kipindi cha nyuma shughuli zake za Muziki alikuwa anafanyia nje ya nchi baadhi ya nchi ambazo alizokuwa anafanyia ni Muscat, Australia, Denmark pamoja na visiwa vya malta na pia wanapiga nyimbo za asili za makabila tofauti ndani na nje ya nchi

Sunday, June 26, 2011

KUPIGA VITA MADAWA YA KULEVYA -VIWANJA VYA MWEMBE YANGA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Tatu Mapando, ambaye ni mmoja kati ya vijana waliotoa ushuhuda mbele ya Makamu wa Rais kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya, baada ya kuacha kutumia madawa hayo. Tatu aliwahi kuwa mnenguaji wa muziki wa dansi katika bendi za Fm, Academia, Diamond Sound, Betta Musica na bendi kadhaa za jijini kabla ya kuanza kutumia madawa. 

Vijana waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya, Rajab Huseein na Tatu Mapando, wakitoa ushuhuda kuhusu utumiaji wa madawa ya kulevya baada ya kuacha kutumia madawa hayo.

Baadhi ya vijana waliowahi kutumia madawa ya kulevya wakipita na mabango mbele ya jukwaa la mgeni ramsi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, yenye ujumbe wakitaka kusaidia dawa na Serikali dawa za kuzuia kutumia madawa, wakati wa Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya madawa ya kulevya yaliyokuwa katika moja ya mabanda hayo kwa ajili ya maonyesho.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkemia Mkuu wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Bertha Mamuya (katikati) wakati alipotembelea na kukagua mabanda katika Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam leo, wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam leo.

USAFI MPAKA TUSIMAMIWE


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akiangalia Uchafu Mtaa wa Toroli Chang'ombe Manispaa ya Temeke Mjini Dar es Salaam wakati aliposhiriki katika zoezi la usafi wa Mazingira Linalofanyika kila siku ya Kwanza ya Mwenzi ambalo ni agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania  Dk Mohammed Gharib Bilali.
Picha na Ali Meja

Friday, June 24, 2011

TALAKA KWA KUTOJIBIWA SIMU

KIJANA aliyefahamika kwa jina la Riziki amejikuta akimpa talaka mke wake baada ya kukerwa na kutopata majibu kutoka kwa mke wake wakati alipokuwa akimpigia simu 

Hata hivyo Riziki alifikishwa Mahakamani baada ya kumjeruhi mke wake huyo na kumsababishia maumivu.

Imedaiwa katika mahakama ya mwanzo Temeke kuwa mshitakiwa huyo alifunguliwa mashitaka hayo na mke wake baada ya kumjeruhi kwa kumpa kichapo cha nguvu mke wake huyo kutokana na hasira za kutojibiwa kwa simu yake.

Imedaiwa kuwa, mshitakiwa huyo June 12 mwaka huu, akiwa nyumbani kwake Tandika alimpa kichapo mke wake aliyetambulika kwa jina la Fatma Hamisi [29] baada ya kumuudhi kwa kutopokea simu wakati alipokuwa akimpigia.

Mshitakiwa huyo alikana shtaka hilo na kuwa nje kwa dhamana na kesi hiyo itasikilizwa mahakamani tena baada ya wiki tatu .

Awali imedaiwa kuwa, Fatma alipigiwa simu na mume wake huyo na hakuweza kupokea kwa kile kilichodaiwa ni ugumu wa mazingira aliokuwa nao wakati simu hiyo ikipigwa ambapo alidai alikuwa kwenye kikao cha familia eneo la Mbagala.

Hivyo kutokana na kukerwa na tabia hiyo Fatma aliporudi nyumbani majira ya usiku Riziki alianza kumporomoshea matusi na hakuridhika alimpa kichapo kwa kudhani mke wake alikuwa na mwanaume mwingine wa nje ya ndoa

Hivyo kutokana na kipigo hicho alichopata kutoka kwa mume huyo na tuhuma aliyopewa na mume wake ,Fatma alikwenda kuripoti tukio hilo nyumbani kwao hali iliyopelekea Riziki kufikishwa polisi.

Hata hivyo mume huyo inadaiwa kuwa alikuwa na wivu wa kupindukia na hata alipothibitishiwa na baadhi ya ndugu kuwa walikuwa wote na Fatma mume huyo alimpa talaka moja mke wake kutokana na hasira.

MKUBWA NA WANAWE BAND NDANI YA TAMASHA LA ZIFF

Mkurugenzi wa Bendi ya Mkubwa na wanawe akiitambulisha rasmi bendi hiyo 


Aslah Mwimbaji wa Bendi ya Mkubwa na Wanawe

Lotti na Zozo Widdah wakitoa burudani

Dulla Yeyo akifanya mambo katika jukwaa la Ziff

Kundi la Mkubwa na wanawe katika show ya Zanzibar International Film Festival (Ziff) ambalo kundi hilo kwa sasa linapiga muziki wa bendi (Live bend) Maskani yake yapo Temeke Mikoroshi maeneo ya Sandari hili ni zao lingine la Temeke Family wamekuja kwa mfumo mwingine, Kundi hilo kwa sasa linaongozwa na Yusuph Chambuso pamoja Said Fella

MITAA YA TEMEKE

Hali ya Mazingira halisi yalivyo katika Baadhi ya maeneo ya Temeke huu ni Mtaa wa Mkumba ambao upo Temeke Miburani-Wailes hali ndio iko hivyo
Huu ni Mtaa Sungwi, karibu na kituo cha Mwembeyanga


Hivi ndivyo ilivyo hakuna utaratibu maalum wa sehemu za kuegesha magari kila mtu anaegesha gari anapojisikia hii ni baadhi ya Mitaa ya wailes ilivyo kwa kipindi hiki licha ya serikali za mitaa kupewa taarifas lakini hakuna utaratibu wowote waliochukua kuhusu suala hili

Monday, June 20, 2011

UNDER ZONE BINGWA FIESTA DANCE 2011

1,000,000/= ya kwetu

Sam Moris Bingwa alionyesha uwezo wa hali juu ni dancer katika kundi la Under Zone

Under Zone Crew
Matayarisho kabla ya kupanda stejini

Viongozi wa Under zone katika picha ya pamoja

kwa mara nyingine tena watoto toka temeke,ambao maskani yao Mtoni kwa Mama Marry  wameweza kuwa mabingwa wa Dance la Fiesta 2011 baada ya kuvibwaga vikundi vitano ambavyo vilifika katika Final. wanapenda kuwashukuru wakazi wote wa Temeke kwa ushirikiano wao waliouonyesha na mashabiki wote wa Underzone na tunahitaji msukumo wenu ili tuweze kufanya vizuri zaidi ya hapa ujumbe  wasijali Ubingwa upo DSM ndani ya TmK