Pages

Monday, July 1, 2013

HISIA ZA MTOTO WA TEMEKE NA TAIFA LAKE

Kichwa kimeanza choka, ebu niwaze
Taifa...

1. Taifa ambalo binti zake wakimwona Mzungu wanadhani ana ela.

2. Taifa ambalo ukiongea kiingereza unaonekana umesoma.

3. Taifa ambalo bank haikutafuti we ndo unaihonga ikukopeshe.

  4. Taifa ambalo ukifeli unakuwa mtangazaji wa kipindi maalumu kabisa.

5. Taifa mbalo simu kali ni dili hata kama vocha waweka za jero jero.

6. Taifa ambalo unazaliwa umeme
shida, unafika miaka 30 hata huna bajeti ya Jenereta/Solar, unailaumu tu TAAnexo!

7. Taifa ambalo warembo washajiona wao ni waomba kusaidiwa daima.

8. Taifa ambalo kila mtu anataka ajue bei ya kitu ulichonunua!

 9. Taifa ambalo usipoiba unaonekana fala!

10. Taifa ambalo kila mtu analalamika hana ela, mpe dili sasa, anaanza longolongo

11. Taifa ambalo sanne lina foleni ya watu wanaenda makazini

12. Taifa ambalo ukisema upo ofisini saa tatu usiku unashangawa ila upo club sanane usiku unasifiwa

13. Taifa ambalo kusema jana nlikuwa bata sana ile mbayaaaa ni dili na waonekana mjanja

14. Taifa ambalo bila kuigana siku haijapita

15. Taifa ambalo kila anayehojiwa anasema "Naiomba Serikali iliangalie suala hili"

16. Taifa ambalo ukiwa na gari hutongozi unatoa tu lift kitu shaa

17. Taifa ambalo kulipa bili yako pekeako ukaruka za wengine ni vita

18. Taifa ambalo ikinyesha dakika 5 tu foleni masaa

 19. Taifa ambalo viongozi wanajua "hawa watazoea tu" washazoea umeme, washazoea "haijajulikana", watazoea na hii

20. Taifa ambalo kijiMC kidonyo tu kinaweza kufariki Taifa zima likageukia Msiba

21. Taifa ambalo kuteswa ni kunyofolewa Meno na Kucha

22. Taifa ambalo, dah, nmechoka, endeleeni nyie.
 
Mtoto wa Tmk
Dee Dion