Pages

Friday, August 17, 2012

WANAKIJIJI KIMBIJI WALALAMIKA JWTZ KUPORA ARDHI YAO

Waheshimiwa 
Mabibi na Mabwana,
Tunasikita kuwajulisha kuwa sisi wanakijiji wa KIMBIJI, wilayani Temeke,
Nje kidogo (KM 30) ya Dar-es-salam,kupitia  Kigamboni,mjimwema.

Mwaka jana 16-08-2011 majira ya saa 4.00 asubuhi,Wanajeshi wa JWTZ
walikuja kijijini na kuvamia mashamba na makazi yetu na kufanya uharibifu
mkubwa. Wanajeshi hao walikuwa wamepakiwa katika magari maroli 
mawili na Landlover moja ya kijeshi.

Walipofika kijijini Kimbiji walipiga risasi hewani kututishia amani sisi wanakijiji,
na kuvamia mashamba pamoja na makazi yalikuwapo katika mashamba yetu
na kubomoa pamoja na kuharibu mazao yetu.
Tukio hili lilipotiwa Polisi ya kigamboni na mji mwema lakini vituo hivyo vilikataa
kupokea taarifa zetu na kusema Polisi watalindwa na nani?

Wanakijiji ambao ni wakazi wa asili wa Kimbiji tunakabaki na vilio hakuna wa
kumlilia.

CHANZO NA KIINI CHA UVAMIVI:
Sisi wanakijiji wa kimbiji tunamiliki maeneo ya ardhi na mashamba yetu,
Kihalali na pia kuwa na hati za serikali ya kijiji,
Mashamba ambayo wanajeshi na maofisa yao wanayataka kwa nguvu
kwa kutumia NEMBO (Crown) ya JWTZ,wakidai heti eneo la kulengea
au kufanya mazoezi ya shabaa ! Kitu ambacho akiwezekani kabisa.
kufanya zoezi la kijeshi katika makazi ya wanakijiji, lakini sababu yao
hii ni ya Uwongo,ukweli ni kuwa wanataka kupora ARDHI kwa
kutumia Nembo ya JWTZ. kwa maana hii basi wamekuwa mara
nyingi wakija na kututishia maisha na Mali zetu.

HAKUNA KIKAO CHOCHOTE KATI YA SEREKALI YA KIJIJI NA JWTZ
KILICHOFANYIKA JUU YA ARDHI YA WANAKIJIJI

Uongozi wa Kijiji chetu umesutushwa sana na uharamia huu wa JWTZ,kwani
hakuna kikao chochote cha kilichowahi kufanyika kati ya serikali ya Kijiji
na JWTZ, Kisheria Ardhi na mashamba ni mali ya wanakijiji, na iwapo
yeyote yule liwe jeshi JWTZ au shirika lolote kama linahitaji ARDHI basi lazima
kwanza likae meza moja na wanakijiji na serikali ya kijiji.Lakini katika tatizo
hili wanajeshi walitaka kutumia NEMBO YA JWTZ ikiambatana na vitisho
vya milio ya bunduki.

CHA KUSIKITISHA NI KUWA WALINZI WA NCHI (JWTZ)
WANAWAVAMIA WANANCHI

Uharamia wa JWTZ katika kijiji chetu kimbiji ni kitendo kinachodhiirisha
wazi kuwa walinzi wa nchi JWTZ wanatumia ubabe kutaka kupora ARDHI
ya wanakijiji ambao ndio wamiliki halali.yaani wanajeshi  wa serikali 
wananyanyasa sisi wananchi tulioichagua serekali !

PLAN YA IDARA YA ARDHI MIPANGO MJI,KIMBIJI HAIPO.
Ufuatiliaji na utafiti wa kina katika idara ya Ardhi,inaonyesha wazi kuwa
Kijiji cha Kimbiji hakipo. yaani ardhi ya kimbiji ni mali ya wanakijiji wa
Kimbiji, na anayetaka lazima aombe kwa wamiliki ambao ndio wanakijiji.
sio vinginevyo au kutumia ubabe.

Labda tahasisi ya HakiArdhi mnaweza kuliingia kati swala hili,
katika kutetea haki za sisi wanakijiji wanyonge tunausumbulia na
wababe wa JWTZ wanaotaka kupora ARDHI ZETU bila
ya ridhaa yetu.
Penginepo mngependa kuwasiliana na uongozi wa kijiji namba ya simu :
Diwani 0713768082.
Mwenyekiti wa Kijiji: 0713846688
Mbunge wa Kigamboni: 0713623106

Nimatumaini yetu kuwa taasisi za kutetea haki za binadamu walala hoi  zitalishughulia tatizo letu na kukomesha tabia za JWTZ
za kutishia wanakijiji milio ya  risasi kwa kutaka kupora ardhi,vitendo hivi vya kijambazi.
Wananchi wenzenu
Wanakijiji KIMBIJI

No comments:

Post a Comment