Pages

Sunday, June 2, 2013

SERIKALI IFUTE SHERIA KUHUSU MRADI WA MJI MPYA WA KIGAMBONI

Mradi wa Mji mpya wa Kigamboni, Wizara ya Ardhi lazima ifuate Sheria siyo kutumia ubabe katika kuchukua ardhi ya wananchi bila ridhaa yao.

Haiwezakani kuwaondoa Wazawa, ardhi wapewe Wageni!

Wizara ya Ardhi imejikuta kuwa mvunjivu wa sheria za nchi,na kutumia nguvu, na kuwatisha wananchi wa wilaya Temeke  kwa kutaka kuwanyang'anya Ardhi katika kutekeleza mradi wa mji mpya Kigamboni (KDA).

Malalamiko na vilio vya wananchi wa maeneo yanayokadiliwa kuanzia ekali 6,000 hadi 50,000 wilaya ya Temeke,vilio vya wananchi hao ambao wanatishiwa kuondelewa katika makazi au ardhi zao ,vimekuwa vilio vya samaki machozi yanakwenda na maji.

Sura mpya ya kutisha inayowaletea mashaka wakazi  Kigamboni na maeneo mengine ambayo Waziri wa Ardhi Prof. Anna Tibaijuka ametangaza kuwa yatachukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa mji mpya Kigamboni, wananchi

wamekuwa wakijiuliza hivi serikali inaivunja sheria ya nchi kwa kupitia wizara ya Ardhi? na kuwatosa wananchi wake katika wingu la giza!

Utata unakuja pale waziri Anna Tibaijuka anapozitaja kata za Pemba Mnazi, Kisarwe II, Kimbiji, wilaya Temeke,kuwa kata hizo zitachukuliwa ili kuongezea utanuzi wa mradi mji mpya Kigamboni, wakati maeneo ya awali yaliotajwa jatika mradi,kata Kimbiji,pemba mnazi,kisarawe II haziku wepo. Wananchi wa maeneo hayo wanajiuliza maswali mengi ambayo majibu yake hakuna, Hivi Serikali itachukua ardhi na kuwafukuza wananchi katika maeneo hayo bila ridhaa ya wenye mali au makubaliano ?

Je? Kufanya hivyo Serikali itakuwa inavunja "sheria za utwaaji Ardhi Na.47 ya mwaka 1967 na Sheria ya Mipango Mji Na.8 ya mwaka 2007."

Sheria za utwaaji Ardhi sura ya 118 inauhusu upangaji vizuri na ujenzi wa makazi tu na siyo viwanda, maofisi,maghorofa ma tahasisi za Umma!

Sasa kama sheria ndiyo hii ,Wananchi wa maeneo yaliyotajwa na Waziri Anna Tibaijuka kwa nini waondelewe pale ? harafu wawekwe akina nani?

Sheria hii hairuhusu Serikali kuleta watu wengine ili kuwaendeleza kwa kisingizio chochote kile hata cha uwekezaji. Ardhi ikitwaliwa chini ya sheria hii itagawanywa kwa wakazi walewale waliokuwapo baada ya kutenga maeneo ya ardhi kwa ajili ya miundombinu.

Wizara ya Ardhi isijinye kichwa ngumu katika kuvunja sheria hizi na kuwa wasiri wa kuwastukiza wanachi baadala ya kuwashirikisha katika miradi ya maendeleo, Sheria ya Mipango Miji Na.8 ya mwaka 2007 hisitumike kama mwanya wa kuwanyang'anya Ardhi wananchi na kuigawa na itakayobaki kuwapa marafiki au wawekezaji,kufanya hivyo ni kuwadhurumu wapiga kura na wananchi wa maeneo usika. ni vema taratibu za kisheria zifuate kuliko Wizara Ardhi kutumia Ubabe.kwa sababu kifungu namba 8 cha sheria hiyo kinataka kabla ya kutangazwa eneo kuendelezwa lazima wananchi waitwe na waelezwe na kukubali mpango au mradi huo.  Kinyume cha ni kuvunja sheria!

Tangazo la serikali la 24 Oktoba 2008 kwenye gazeti la Serikali Na. 43 Vol. 89 lilikuwa na taarifa ya  amri ambayo ilianisha mipaka ya eneo litakalokumbwa na ujenzi wa mji mpya kuwa ni kata tano  za Somangila, Kigamboni, Vijibweni, Kibada na Mji Mwema.

Tumsikilize Rais Kuhusu Kigamboni youtube.com/UaviGdsJJNI na youtube.com/Jh2jQcnWcQo

Imewasilishwa na Jackob Buberwa