Pages

Tuesday, April 12, 2011

WANAONIONEA WIVU WALIE TU-TAMBWE



\Mkuu wa kitengo cha plopaganda wa chama cha mapinduzi Taifa, Tambwe Hizza amesema wanaonionea wivu labda mabadiriko yaliyofanywa katika chama hicho yatanikumba na mimi walie tu kwa kuwa mimi ni muajiliwa.
Akiongea na TEMEKEPAMOJA.BLOGSPOT.COM, Tambwe amesema kuwa mabadiriko katika chama ni ya kawaida na sasa atakuwa akifanya kazi chini ya kijana msomi mwenye upeo mkubwa Nape Nnauye badara ya Chiligati kama ilivyokuwa awali.
Aidha akimzungumzia Katibu Mkuu mpya wa CCM amesema ni mtu muadilifu na mchapakazi na amewahi kukitumikia chama katika nafasi mbalimbali kama mkuu wa itikadi ya uenezi pamoja na kufanyakazi katika sekta mbalimbali Serikalini.
Hata hivyo amekili maumivu yaliyokuwa yakipata chama kutokana na Kashfa za kifisadi "kwa sasa itakuwa imebaki history kwani mwenyekiti wangu ambaye huwa hakulupuki katika kufanya mambo yake ametumia busara na hekima katika mabadiriko hayo" alisema.
Tambwe alitakiwa kutoa maoni yake kuhusu mabadiriko ndani ya CCM hasa nafasi ya katibu Mkuu kutokana na madai kuwa aliwekwa na Mzee Yusuph Makamba kutokana na kuwepo kwa uhusiano wa wote kutoka mtaa mmoja
Hata hivyo Tambwe amekanusha kuwa nafasi hiyo amepewa na aliyekuwa katibu Mkuu wa CCM Taifa Mzee Yusuph Makamba " Hakuna kitu kama hicho bali ni utendaji na uadilifu wangu katika chama ndio ulionifikisha hapa nilipo isiwe dhambi makamba na mimi kutoka katika mkoa mmoja kwani mimi nilikuwa nafanya kazi chini ya Katibu mwenezi John chiligati"alisema huku akionyeshwa kukelwa na maneno hayo.

2 comments:

  1. Tumekusikia Mheshimiwa Tambwe, tunasubiri kitachoendelea.

    CCM DAMUDAMU

    ReplyDelete
  2. Rekebisheni sarufi zenu katika lugha. sisi wenye lugha yetu tunakerekwa kutumia RA, badala LA na I badala H mfano unaposema ameajiliwa au mabadiriko si sahihi au ndio English medium school.
    tunawapenda jirekebisheni.

    MDAU MOMBASA

    ReplyDelete